LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hili tukio ilibidi waonyeshe mfano ingelisaidia huko mbeleni wanajeshi wa Ukraine wajue kupigana na Russia unakwenda machinjoni!

Wangefanya matukio ya kuogofya sehemu kama 3 au 4 au hata 5 Zelensky mwenyewe angepambana kukaa mezani.

Na jinsi Putin anavyoendesha hii Operation usidhani kwamba viongozi wenzake na wakuu wa majeshi wanapendezwa na maamuzi yake la hasha!

Wengi hawapendi, ila kwa vile ni rais hawana namna!
 
Ninaamini kwa tabia ya trump ya kupenda kuropokaropoka kila wakati,kama angekuwa amechukizwa kuhusu kile alichokifanya Biden siku mbili hizi kuhusu vita ya Ukraine na urusi,basi Jamaa angekuwa ameshajitokeza waziwazi na kuukemea uongozi wa Biden huku akiapa kuyamaliza yote pindi atakaposhika usukani..,kwa mambo yanayohusu sera za kigeni marekani Huwa Wana mshikamano sana
 
shambulio la kigaidi limepita kimya kimya, budanov na wajinga wenzake mpaka leo wanakula bata UKRAINE.
View attachment 3156932
Putin amekuwa mtu wa matamko mengi!

Sasa hivi amekuwa mtu wa matamko mengi kama mwaandishi wa habari!

Akitoka hapo Lavrov ataungumza! Akimaliza Lavrov atakuja Maria!

Waache wenzake wamshikishe adabu pengine ataamka kutoka usingizini.

Au kama vita haiwezi arudishe watoto wa watu kwa sababu anawaua kwa upuuzi wake hali ya kuwa wenzake wamejitolea kuipambania nchi!
 
Hahahahaha. Dah
 
Wewe unataka afanye nini.kwani NATO na Marekani wameingia kwenye ardhi ya Urusi na izo silaha?.

 
Hawa magaidi wa Nato wanafanya ugaidi wanajificha kwenye kichaka cha Islamic state , halafu wapumbavu hata hawa connect dots na kujua kwamba Islamic state na makundi mengine ya kigaidi ni projects za hawa washenzi miaka mingi

Warusi sio wajinga mpaka kutoa hiyo conclusion ,wanajua gaidi ni nani
 
British Storm Shadow missiles 12 zimerushwa kwenda Kursk jioni hii,Putin Yuko tu bize na mikwara.
Ukraine alikuwa amefungwa mikono,Sasa kafunguliwa anatembeza kichapo balaa🀩😍🀩😍🀩😍
 
Daah!
Mtu asieelewa kinoendelea huko Ukraine kama wewe yabidi kukuachia tu uandike kama hivyo.

Russia inashinda vita wapo uwanja wa vita wakisonga mbele.

Hatua ya Marekani na NATO kuruhusu makombora ya ATACMS na UK kufuata kuruhusu Storm Shadows hakutabadili matokeo ya uwanja wa vita. Jack Sullivan amekiri kwamba Ukraine haina manpower isipokuwa yahitaji zaidi silaha soma hapa: MSN, hizo ni lazima ziwe ordered na ziwe delivered miezi hadi miwili.

Hizo ATACMS tano kati ya sita zote ziliharibiwa na Russia na moja ikaanguka na kusababisha moto lakini hakuna madhara yoyote makubwa yalosababishwa na makombora hayo na hata Ukraine hawana ushahidi wa hilo.

Hayo makombora ni ghali sana na si kwamba ni leo yamepelekwa Ukraine yapo pale kitambo kwenye maghala na yakiisha hayo Ukraine itakosa makombora zaidi kwani Trump tayari atakuwa ameapishwa, ATACMS yanagharimu kiasi cha dola milioni 1.5 (kombora moja) wakati Storm Shadow ni pauni milioni 2 kwa kombora soma hapa : Atacms: What we know about missile system Ukraine could use to strike Russia

Kinoonekana ni kwamba hatua hizi za Biden na NATO ni hatua za "panic room" na kule Marekani tayari wazungumzia kumfanyia "impeachment" raisi Biden kwa kuruhusu mabomu hayo yatupwe kwenda ndani ya "territory" ya Russia, uamuzi ambao ulitakiwa ujadiliwe na Bunge la Senate.
 
Ukraine alikuwa amefungwa mikono,Sasa kafunguliwa anatembeza kichapo balaa🀩😍🀩😍🀩😍
Hizo silaha zimetumika hapo kabla wakumbuka daraja la Kerch lililipuliwa na bomu la Storm Shadow na hizo ATACMS zimetumika kupiga Crimea zikaharibu meli za kivita pale Sevastopol kiasi cha kuifanya Russia kuhamisha mali zote za kijeshi.

Hizo silaha ni ghali mno (ATCMS ni dola milioni 1.5 kwa kombora na Storm Shadow ni pauni milioni 2 kwa kila kombora soma hapa: Atacms: What we know about missile system Ukraine could use to strike Russia ) ndo maana waliziweka akiba na zikiisha hizo hakutakuwa na zingine.

Isitoshe Russia ataendelea kuzidungua na huku akiendelea na SMO kama kawaida maana wamesema matumizi ya silaha hizo hayatabadili mwelekeo wa vita yaani Russia kuchukua maeneo zaidi.
 
Upo sahihi, Putin kumuelewa inahitaji Four-Dimension critical thinking. Hata hivyo, Trump simuamini Hata kidogo!!!
Biden anafahamu kwamba Trump atabadili kila kitu na kwamba bidene pia amekosea kuruhusu mabomu hayo kutumika ndani ya Russia ni kosa kwa Biden na Republicans wameanza kuzungumzia "impeachment"

Pia Marekani tayari wameingiwa wasiwasi kwani Zelennsky ameambiwa itabidi akubali kupoteza majimbo yote yalipokwa na Russia ili makubaliano ya amani yaweze kufanyika na pia kutojiunga na NATO lakini kwa kupewa "guarantees" ya usalama wake na kwamba Russia hataki mitambo ya NATO ndani ya Ukraine.
 
Zile zilitumia za masafa mafupi mzee, hizi za sasa zinaweza piga hadi km 300 ndani ya Urusi, tuanze kutegemea Moscow ikichakazwa
 
Huyo jamaa kajaa ushabiki wa kipuuzi sana, anawaza miji ya ulaya na marekani kuchakazwa, lakini ubongo wake hauwazi kuwa miji ya Urusi pia ipo uchi, yaani ni vichekesho vitupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…