LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
bwana Hammaz unalikumbuka hili tukio, hapa ndipo nilianza kuziona huruma za ajabu alizonazo putin.
wahuni wakiongozwa na kadyrov pamoja na shoigu walitaka kuchoma moto panya wote waliomo ndani ya kiwanda lakini mzee akakataa mpango huo.
View attachment 3156926
View attachment 3156927
unamuoneaje huruma kiongozi wa nchi aliyetunga sheria ya kupiga marufuku mazungumzo nawe.
sometime huwa nasema ni bora PUTIN apigwe tu.

Hili tukio ilibidi waonyeshe mfano ingelisaidia huko mbeleni wanajeshi wa Ukraine wajue kupigana na Russia unakwenda machinjoni!

Wangefanya matukio ya kuogofya sehemu kama 3 au 4 au hata 5 Zelensky mwenyewe angepambana kukaa mezani.

Na jinsi Putin anavyoendesha hii Operation usidhani kwamba viongozi wenzake na wakuu wa majeshi wanapendezwa na maamuzi yake la hasha!

Wengi hawapendi, ila kwa vile ni rais hawana namna!
 
Ninaamini kwa tabia ya trump ya kupenda kuropokaropoka kila wakati,kama angekuwa amechukizwa kuhusu kile alichokifanya Biden siku mbili hizi kuhusu vita ya Ukraine na urusi,basi Jamaa angekuwa ameshajitokeza waziwazi na kuukemea uongozi wa Biden huku akiapa kuyamaliza yote pindi atakaposhika usukani..,kwa mambo yanayohusu sera za kigeni marekani Huwa Wana mshikamano sana
 
shambulio la kigaidi limepita kimya kimya, budanov na wajinga wenzake mpaka leo wanakula bata UKRAINE.
View attachment 3156932
Putin amekuwa mtu wa matamko mengi!

Sasa hivi amekuwa mtu wa matamko mengi kama mwaandishi wa habari!

Akitoka hapo Lavrov ataungumza! Akimaliza Lavrov atakuja Maria!

Waache wenzake wamshikishe adabu pengine ataamka kutoka usingizini.

Au kama vita haiwezi arudishe watoto wa watu kwa sababu anawaua kwa upuuzi wake hali ya kuwa wenzake wamejitolea kuipambania nchi!
 
Ukweli wengi wetu tunaona Putin anatuangusha kwa sababu tulitarajia kuiona kiev ikiwa kama Allepo au gaza. Au kufanywa kama kile wanachofanywa lebanon na mazayuni kule kusini mwa beirut.
Putin kwa kitendo cha ukrain kushambulia kwa makombora ya masafa marefu ndani ya russia ilibidi majibu yake yawe makali na mara 100 zaidi. Kama walirusha makombora 6 kiev ipigwe kwa makombora 100+ hii itawafanya waogope kurudia huu usenge waliofanya.
Ila Putin anatuangusha sana
Hahahahaha. Dah
 
Wewe unataka afanye nini.kwani NATO na Marekani wameingia kwenye ardhi ya Urusi na izo silaha?.

Putin kama hataonyesha msimamo wa maneno yake kwenye hili RUSSIA itapoteza ushawishi wake ulimwenguni,
Dunia ilitarajia Russia kubalance mzani wa ubabe.
Kauli zimekua nyingi kuliko vitendo.
Mkishakuwa kwenye vita hamna busara,,,
Hakunaga urafiki kwa adui

Dunia nzima inaifatilia hii vita
Kama kutakuwa kimya na maneno mengi Putin atathibitisha HE IS NOT A SOVIET MATERIAL
 
Hawa magaidi wa Nato wanafanya ugaidi wanajificha kwenye kichaka cha Islamic state , halafu wapumbavu hata hawa connect dots na kujua kwamba Islamic state na makundi mengine ya kigaidi ni projects za hawa washenzi miaka mingi

Warusi sio wajinga mpaka kutoa hiyo conclusion ,wanajua gaidi ni nani
 
Hili lilikuwa wazi mda mrefu
West ndio wali organize mauaji yale.
Juzi wametega bomu kwa mkuu wa kambi.
West wapo kwenye utayari wavita na russia kuliko Russia alivyotayari.
Ukiacha nuclear west wapo fit kwambinu na hila za kutosha
Hata nuclear Russia atakuwa na target nyingi kuliko west watakavyokuwa.

Ngoma sio50% 50%
Kama ilivyokuwa kwa Soviet .
Labda russia awe na kitu kipya cha siri.
Putin analijua ilo kuliko sisi
Labda sio busara.
Daah!
Mtu asieelewa kinoendelea huko Ukraine kama wewe yabidi kukuachia tu uandike kama hivyo.

Russia inashinda vita wapo uwanja wa vita wakisonga mbele.

Hatua ya Marekani na NATO kuruhusu makombora ya ATACMS na UK kufuata kuruhusu Storm Shadows hakutabadili matokeo ya uwanja wa vita. Jack Sullivan amekiri kwamba Ukraine haina manpower isipokuwa yahitaji zaidi silaha soma hapa: MSN, hizo ni lazima ziwe ordered na ziwe delivered miezi hadi miwili.

Hizo ATACMS tano kati ya sita zote ziliharibiwa na Russia na moja ikaanguka na kusababisha moto lakini hakuna madhara yoyote makubwa yalosababishwa na makombora hayo na hata Ukraine hawana ushahidi wa hilo.

Hayo makombora ni ghali sana na si kwamba ni leo yamepelekwa Ukraine yapo pale kitambo kwenye maghala na yakiisha hayo Ukraine itakosa makombora zaidi kwani Trump tayari atakuwa ameapishwa, ATACMS yanagharimu kiasi cha dola milioni 1.5 (kombora moja) wakati Storm Shadow ni pauni milioni 2 kwa kombora soma hapa : Atacms: What we know about missile system Ukraine could use to strike Russia

Kinoonekana ni kwamba hatua hizi za Biden na NATO ni hatua za "panic room" na kule Marekani tayari wazungumzia kumfanyia "impeachment" raisi Biden kwa kuruhusu mabomu hayo yatupwe kwenda ndani ya "territory" ya Russia, uamuzi ambao ulitakiwa ujadiliwe na Bunge la Senate.
 
Ukraine alikuwa amefungwa mikono,Sasa kafunguliwa anatembeza kichapo balaa🤩😍🤩😍🤩😍
Hizo silaha zimetumika hapo kabla wakumbuka daraja la Kerch lililipuliwa na bomu la Storm Shadow na hizo ATACMS zimetumika kupiga Crimea zikaharibu meli za kivita pale Sevastopol kiasi cha kuifanya Russia kuhamisha mali zote za kijeshi.

Hizo silaha ni ghali mno (ATCMS ni dola milioni 1.5 kwa kombora na Storm Shadow ni pauni milioni 2 kwa kila kombora soma hapa: Atacms: What we know about missile system Ukraine could use to strike Russia ) ndo maana waliziweka akiba na zikiisha hizo hakutakuwa na zingine.

Isitoshe Russia ataendelea kuzidungua na huku akiendelea na SMO kama kawaida maana wamesema matumizi ya silaha hizo hayatabadili mwelekeo wa vita yaani Russia kuchukua maeneo zaidi.
 
Upo sahihi, Putin kumuelewa inahitaji Four-Dimension critical thinking. Hata hivyo, Trump simuamini Hata kidogo!!!
Biden anafahamu kwamba Trump atabadili kila kitu na kwamba bidene pia amekosea kuruhusu mabomu hayo kutumika ndani ya Russia ni kosa kwa Biden na Republicans wameanza kuzungumzia "impeachment"

Pia Marekani tayari wameingiwa wasiwasi kwani Zelennsky ameambiwa itabidi akubali kupoteza majimbo yote yalipokwa na Russia ili makubaliano ya amani yaweze kufanyika na pia kutojiunga na NATO lakini kwa kupewa "guarantees" ya usalama wake na kwamba Russia hataki mitambo ya NATO ndani ya Ukraine.
 
Zile zilitumia za masafa mafupi mzee, hizi za sasa zinaweza piga hadi km 300 ndani ya Urusi, tuanze kutegemea Moscow ikichakazwa
Hizo silaha zimetumika hapo kabla wakumbuka daraja la Kerch lililipuliwa na bomu la Storm Shadow na hizo ATACMS zimetumika kupiga Crimea zikaharibu meli za kivita pale Sevastopol kiasi cha kuifanya Russia kuhamisha mali zote za kijeshi.

Hizo silaha ni ghali mno (ATCMS ni dola milioni 1.5 kwa kombora na Storm Shadow ni pauni milioni 2 kwa kila kombora soma hapa: Atacms: What we know about missile system Ukraine could use to strike Russia ) ndo maana waliziweka akiba na zikiisha hizo hakutakuwa na zingine.

Isitoshe Russia ataendelea kuzidungua na huku akiendelea na SMO kama kawaida maana wamesema matumizi ya silaha hizo hayatabadili mwelekeo wa vita yaani Russia kuchukua maeneo zaidi.
 
Tatizo ninaloliona humu JF wengi sisi ni wajuaji kuliko wanaohusika na hivyo vita vya Ukraine . Naona na wewe umeandika gazeti.. Yaani wewe unajua kuliko USA na Washirika wake. Yaani Marekani inafanya jambo fulani halafu mswahili wa Bunju unajidai unajua athari atakazozipata. Mswahili wa Tegeta kwa Ndevu anajua kuliko Pentagon na CIA.
Huyo jamaa kajaa ushabiki wa kipuuzi sana, anawaza miji ya ulaya na marekani kuchakazwa, lakini ubongo wake hauwazi kuwa miji ya Urusi pia ipo uchi, yaani ni vichekesho vitupu
 
Back
Top Bottom