LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mkuu wanaposema Russia have lost more than 700,000 soldiers hawamaanishi wamekufa wote ,huwa wanajumuisha na ambao wamejeruhiwa vibaya ,jeshini ukishajeruhiwa kiasi kwamba ukatolewa uwanja wa mapambano jeshi linahesabu kama limepoteza nguvu kazi.
 
Wanaodhani kuna super power mwingine ataibuka zaidi ya NATO kuitawala Dunia siku zijazo hasomi bibilia na tayari maandalizi ya NATO yamekamilika kwa asilimia kubwa.Ukisoma danieli sura ya 8 yote utapata majibu,Marekani itaangamia katika harakati za kuisimamisha NATO , Russia na China wataangamizwa kabisa na umoja wao utapotezwa kabisa,yataibuka mataifa manne ambayo ndiyo yatakua nguzo ya NATO kwa wakati huo mataifa hayo yatakua German,UK, Italy na France wakati huo USA itakua imeangamizwa katika vita kubwa baina ya NATO na mataifa yatakayoongozwa na Russia na China ,ila NATO itaibuka mshindi katika vita hivyo huku ukiwa imempoteza baba Yao mpendwa U.S.A maana atakua ameangamizwa vibaya ,China na Russia nazo zitafutiliwa mbali ,uchumi wa Dunia utaanguka vibaya,mamilion ya binadamu wataangamia kutokana na silaha nzito zitakazotumika kipindi hicho, NATO itakuja kuangamizwa na Yesu tuu pekee ,hakuna tena utawala utakaotawala baada ya NATO ,zaidi ya ufalme wa mbinguni.mwenye ufahamu na afahamu
 
Unaota baada ya shibe ya Ubwabwa maharage. Yaani akina Moldova na Estonia ndo waichakaze Rusia hadi China bila Marekani. Kwa habari yako NATO ndo Marekani, hakuna NATO nje ya Marekani. Siku marekani akisema anatoka NATO ndo imeisha hiyo. Marekani alichofanya ni kuyakusanya makoloni yake ndani kapu moja akaliita NATO.
 
Lavlov na Blinken walichojadiliana huko Urusi ni Siri, Ila matokeo yanaanza kuonekana.
 
Mzee mtarimbo amka ndotoni kumeishakucha.Vita ya NATO na RUSSIA/CHINA ni mwisho wa Dunia yetu tunayoijua.Hawa washenzi wanamiliki manuklia makubwa ambayo hata wakirushiana wenyewe athari zake kwa Dunia bado ni mbaya mno.Hawa watapigana proxy war na sio direct war.
 
Utakuwa mfalme Zumaridi
 
Kasome vizuri biblia yako
 
Ndio maana nimesema kutatokea maafa makubwa sana ambayo hayajawahi kutokea ,kasome Daniel sura yote ya kumi ila ukianzia 8 ndio utapata picha , Daniel aliona kondoo dume mwenye pembe ,(huyo kondoo anawakilisha mataifa yanayopinga ubeberu ,zile pembe mbili ni mataifa mawili ambayo ni China na Russia,)
Kondoo huyo ataelekea kuzikabili nchi za magharibi lakini Daniel anasema aliona beberu mkubwa mwenye pembe moja akitokea magharibi(beberu huyu anawakilisha NATO na ile pembe yake moja anayoitegemea ni U.S.A).Kisha beberu huyo atapambana na yule kondoo dume na atamshinda ,pamoja na kushinda atakua amepoteza ile pembe yake moja ambayo ni U.S.A hivyo NATO itashinda Vita dhidi ya China na Russia na washirika wao ila itampoteza U.S.A kwan atakua ameharibiwa kabisa na makombora ya nukes,NATO itazidi kujitanua kwa speed na kutawala dunia yote na maisha yatakua magumu sana maana Ulimwengu utakua umeangamizwa na makombora kwa sehemu kubwa.Soma Daniel yote 10.asiye amini na asiamini hulazimishwi kuamini
 
Kasome vizuri biblia yako
Ndio maana nimesema kutatokea maafa makubwa sana ambayo hayajawahi kutokea ,kasome Daniel sura yote ya kumi ila ukianzia 8 ndio utapata picha , Daniel aliona kondoo dume mwenye pembe ,(huyo kondoo anawakilisha mataifa yanayopinga ubeberu ,zile pembe mbili ni mataifa mawili ambayo ni China na Russia,)
Kondoo huyo ataelekea kuzikabili nchi za magharibi lakini Daniel anasema aliona beberu mkubwa mwenye pembe moja akitokea magharibi(beberu huyu anawakilisha NATO na ile pembe yake moja anayoitegemea ni U.S.A).Kisha beberu huyo atapambana na yule kondoo dume na atamshinda ,pamoja na kushinda atakua amepoteza ile pembe yake moja ambayo ni U.S.A hivyo NATO itashinda Vita dhidi ya China na Russia na washirika wao ila itampoteza U.S.A kwan atakua ameharibiwa kabisa na makombora ya nukes,NATO itazidi kujitanua kwa speed na kutawala dunia yote na maisha yatakua magumu sana maana Ulimwengu utakua umeangamizwa na makombora kwa sehemu kubwa.Soma Daniel yote 10.asiye amini na asiamini hulazimishwi kuamini
 
Soma vizuri usikurupuke kujibu mkuu nimesema katika vita vya NATO dhidi ya China na Russia NATO itashinda ila Marekani atakua naye ameangamizwa kabisa haitakua vita ya kitoto,kama Daniel alivyotabiri yule beberu atashinda ila pembe yake moja ya kipekee itavunjika,hivyo sijamaanisha kama unavyofafanua ukitaka madini zaid niinibox nikupe full package ya mwisho wa zama hizi
 
Unaota baada ya shibe ya Ubwabwa maharage. NATO ndo Marekani, hakuna NATO nje ya Marekani. Siku marekani akisema anatoka NATO ndo imeisha hiyo. Marekani alichofanya ni kuyakusanya makoloni yake ndani kapu moja akaliita NATO.
hizi hekaya zako za Kisabato hebu achana nazo.
 
Kuna Ndg yako alishawahiu kuleta humu kwamba huyo Beberu ni EU na ile pembe moja ni Uingereza na hivyo baada ya Uingereza kuijitoa EU ndo utabiri wa Pembe kuvunjika.

Lakini pia kuna mzee moja Mlokole kweli kweli alishaletaga hizo habari kwamba Lile sananu lenye mfinyanzi na chuma ni EU na kamwe kamwe halitaweza kuitawala dunia maana wana falsafa tofauri tofauti. EU na NATO tofauti yao ni moja tu kwamba EU beberu lao lilikuwa UK na NATO beberu lao ni USA lakini kote humo hawana falsafa moja. Ndani ya NATO wengi wameingia ili tu kupata uhakika wa kulindwa wakati wengine wakiwa mababaru halisi na hivyo lengo lao ni kutumia hicho kichaka kupora rasilimali za dunia.

Lakini pia wasabato fulani wafiasi wa falsafa za Ellen G. white walishatoaga hadi kitabu kwamba huyo mnyama alikuwa Dola la Rumi ya Kidini (Holy Roman Empire) chini ya Ujerumani na kwamba lile jeraha lake ni Kanisa katoliki la sasa chini ya Papa.

Kwa ufupi kwa haya machache ni kwamba mnatuchosha tu na Bible has nothing na kinachoendelea duniani.
 
Zumaridi likubwa wewe?
 
Hawa wanatoa utabiri kutokana na matukio ya nyakati husika. Utasikia baada ya haya miaka 30 mbele, kuna utabiri mwingine utatolewa wa kitabu hichohicho cha Ufunuo.
Ukisoma kitabu cha Vita Kuu cha Ellen G. White, ufafanuzi wake wa Kitabu cha Ufunuo ni tofauti na huyu ndugu mtarimbo.
Hii biblia itawachangaya sana.
 
Umesoma vizuri mkuu au umekurupuka ni kwamba Marekani itaangamia, Russia na China na baadhi ya nchi zinazowaunga mkono zitaanguka ila NATO itabaki vilevile na itajiimarisha zaidi na zaidi
 
Wadau niwaombe kama hamna updates za uwanja wa vita basi tusubiri hadi zitakapopatikana. Sasahivi thread hii imekuwa mbaya kwasababu ya kuweka mastori tu ya kufikirika na chambuzi ndeeeeeeeeeeeefu zisizo na maana.

Admn nashauri ianzishwe Thread inayojitegemea yenye heading ya "" Chambuzi na Maoni Mgogoro wa Ukraine ".

Halafu hili jukwaa libaki kwa ajili ya taarifa za huko kwenye mapambano.
 
Ni wazo zuri maana humu tunaelimishana mimi pia nimesoma mahali siwez kushupalia sana vitu ambavyo hata mimi sijui tuchangamshe jukwaa tuu siku ipite
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…