===============
Hii vita imeigharimu mno Urusi kuliko vita nyingine yeyote tangu kumalizika WW2.
T14 Armata TUJITEGEMEE
Watu sijui kwa Nini mmekua na vichwa vigumu namna hii.
Hamtaki kufanya analysis kisomi na kitaalam.
Hamtaki kukubali ukweli.
Ukweli ni kwamba Urusi imezidhalilisha mno nchi za Magharibi,imeidhalilisha mno NATO na imeidhalilisha mno USA.
Urusi imeiharibu Ukraine vibaya sana.
Hebu jiulize tokea vita hiii imeanza ni misaada ya sh ngapi imeenda Ukraine na imesaidia Nini?
Ni misaada ya kiasi Gani ya silaha imepelekwa Ukraine na imefanya Nini?
Hayo ma silaha yote yaliyotoka nchi za west Kila siku yameenda wapi? Na kwa Nini wapeleke masilaha Kila siku?
Kama yanasaidia kwa Nini waongeze mengine Kila siku?
Kwa kifupi ni kwamba west wamepata hasara kubwa mno ya silaha na fedha lkn kwa kua zinatoka kwa nchi zaidi ya 59 huwezi kuona kama ni hasara kubwa Kwa sababu zimetolewa na nchi nyingi
Watu kwa aibu zenu mnapinga kua west na NATO Kwa pamoja eti hawashiriki vita hii moja kwa moja,mnadai kua eti Ukraine Iko peke yake,lakini FACTS zinawaumbua.
Facts kua NATO na west
wanashiriki:-
Ushiriki wa west au NATO uko hivi:
Wote mnakubali kua Kuna baadhi ya silaha anazotomia Ukraine zinahitaji satellite ya nchi ambako silaha hizo zimetengenezwa,mfano
-Storm Shadow satellite ni UK,
-ATTACMS satellite ni USA n.k.
Kwa sababu wanaochakata taarifa za satellite kuweka data na kuprogram makombora yapige wapi ni wanajeshi wa nchi makombora yanakotoka.
je hizii sio fact kwamba NATO wanshiriki?
US officials say President Biden has given Ukraine permission to fire long-range ATACMS missiles into Russian territory.
It is thought that the UK and France could follow suit by saying that Storm Shadow missiles can also be used against targets inside Russia.
Silaha zilizoletwa mapema kama Patriot na ADS nyingine zimekua operated na wanajeshi wa nchi zilikotengenezwa,mfano USA ,UK German n.k hii ni fact kua NATO wanshiriki
Taarifa za ki intelligencia hii nayo ni fact nyingine kua NATO wanshiriki.
Washaurii,wakufunzi na makamanda wanaouliwa kwenye mahandaki ya control,vyuo na makambi mbalimbali baadhi Yao wanatokea nchi za NATO, hii nayo ni fact kua NATO wanshiriki.
Nchi za west zote zimeiwekea vikwazo Urusi lkn bado inadunda na haioneshi dallili za kuanguka.
Sasa jamani hata Kwa akili ya kawaida TU nchi moja inakabiliana na nchi zote hizo huoni kua nchi hiyo ni ngangari kweli kweli?
Kwa kumalizia Urusi imeonesha uwezo wa ajabu na WA Hali ya juu mno tofauti na hata tulivyokua tukiifahamu kabla ya vita hii.