Hii ndio inaitwa KUPIGWA mande 🤣🤣
MAREKANI - Rais wa Marekani, Donald Trump, anatarajia kuwa Waziri wake wa Fedha, Scott Bessent, ambaye alitembelea Ukraine Jumatano, atahakikisha makubaliano yanapatikana ili Washington ipate faida kutokana na mabilioni ya dola ilizowekeza kama msaada kwa Kiev.
Hivi karibuni, Trump alidai "dola bilioni 500 za madini adimu" kutoka Kiev kama malipo kwa zaidi ya "dola bilioni 300" ambazo mtangulizi wake, Joe Biden, alituma Ukraine kama msaada kwa miaka kadhaa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House Jumatano, Trump alisema alikuwa na mazungumzo ya simu na kiongozi wa Ukraine, Vladimir Zelensky, mapema siku hiyo na kwamba Kiev imekubali madai yake.
"Nina Waziri wa Fedha kwa sasa ambaye ni jasiri sana – yuko Ukraine," Trump aliwaambia waandishi wa habari. "Ameenda huko kuhakikisha tunapata hati inayoonyesha kuwa kwa namna fulani tutarudishiwa fedha zetu."
Rais wa Marekani alisema ni upumbavu kwa Washington kutohakikisha "usalama wa fedha zetu," akidai kuwa wafadhili wengine wa Kiev walifanya hivyo. "Marekani chini ya Biden haikutoa mikopo. Walikuwa wakitoa tu pesa kila wakati mtu yeyote kutoka Ukraine alipoingia. Walizitoa tu kiholela," Trump aliongeza.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Zaidi tembelea //habarileo.co.tz
#HabarileoUPDATES
#Trump #Trending #Ukraine #ElonMusk