Hana lolote huyo na haeleweki anachotaka. huku Russia anasema peace talk wakati Gaza anataka kuleta vita.
Trump bado haeleweki anataka nini kwa dunia.
Mkuu, wewe ndiye humwelewi Trump.
Jamaa amenyooka kama rula na yuko wazi mno tangu vita vianze, kuhusu nini anachotaka.
Mahaba yake kwa Urusi ni makubwa kwa vile Russia amekuwa mstari wa mbele tangu awali kusisitiza suala la mazungumzo ya amani.
Ameonekana kuwa tofauti kabisa na Zelenskyy na vifiwaza (warmongers) wa NATO kwa sababu jamaa wanataka vita viendelee kwa manufaa yao wenyewe.
Yeye kama kiranja wa dunia, lazima awe msuluhishi.
Huu ndio wajibu unaopaswa kufanywa na taifa, jamii au mtu yeyote mwenye nguvu kuliko wengine.
Tunaweza kusema Trump anajaribu kuirudisha Marekani kwenye reli, lengo na msingi wake - ambao haufahamiki kwa wengi kwa vile sivyo ambavyo tumeizoea kuona ikifanya siku zote.
Kwenye kampeni zake za urais, Trump aliwahi kusema kwamba endapo angeshinda, angefanya mambo ya kuwashangaza wengi kwa sababu siyo matarajio yao wala hayakuzoeleka kwao.