LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Ndio maana nakuambia kwa uelewa wako wa haya masula ya kijeshi sikutegemea ya kwamba ungekuwa unatoa hoja dhaifu kiasi hichi.

Mkuu kwani ujui ya kwamba vita sio kitu rahisi kwenye vita kupoteza ni razima hata uwe na nguvu kiasi gani.

Marekani na washirika wake zaidi ya kumi tena wenye nguvu za kijeshi duniani walitumia miezi 7 kufika mji mkuu wa Iraq na wakiwa wamesha poteza maelfu ya wanajeshi.
Ila Urusi iliyo weza kufika mji mkuu ndani ya masaa 48 una muona sio kitu?

Alafu tukiongelea ule hualisia kwenye hivi vita Urusi ina tumia nguvu ya kawaida sana na ndio maana hata vifo ni vichache ukilinganisha na vita vya Iraq ambavyo ndani ya siku moja ya uvamizi maelfu ya watu waliuwa.

Kinacho ifanya isitumie nguvu kubwa inaogopa kuharibu miundo mbinu ya kiraia kwa sababu ndio itabeba dhima ya kujenga hiyo miundo mbinu baada ya kuiteka nchi hiyo.

Kingine wanacho kiogopa ni Marekani kutumia raia wengi watakao uawa kama propaganda ya kueneza chuki dhidi ya Russia.
 
Swala la kuungwa mkono sio issue,hata hapa kwetu sidhani kama viongozi wa CCM huwa wana shinda but at the end huwa wanaongoza.Lakini pia Urusi bado ana option ya kuichukui Ukraine nzima na kuifanya sehemu ya Urusi.
Kuichukua Ukrain ni ndoto ya asubuhi...
Kufananisha yanayoendelea Urusi na Ukrain na siasa za Kwetu ni kichekesho..
 

Kazakhstan mwenye mpaka Baykonul cosmodrome inayotumika na Russia kufyatua rockets angani na kutuma satellites zote za kijeshi na kiraia kakataa.
Uturuki aliyeuziwa S-400 na Urusi yuko analaumu NATO kuwa wazembe kuidhibiti Urusi. North Korea hawana shobo na mambo yasiyowahusu miaka yote.

Wanaomuunga mkono ni Syria, huyu hata ungekuwa wewe ungekubali huna namna. Belarus pale Lukashenko ni kibaraka wa Russia na anategemea Urusi kulinda utawala wake. Same applied na Venezuela
 
Kwahiyo kwa idea yako wewe hayo mabomu yana ukubwa sawa na miji yote hiyo ina ukubwa sawa?

Kwamba kila bomu liko designed kuumaliza mji mmoja?

Hizi idea za kwamba bomu moja linamaliza mji wote mnazitoa wapi?
 
Shida kubwa nayoiona kwenye huu mgogoro ni rais wa Ukraine. Jamaa anaonekana hana sifa zozote za kiuongozi zaidi ya kuwa maarufu kwenye comed na Burudani nyingine za hovyo.

Huyu ni aina ya Watu kama George Weah na kina Bob Wayne. Ambao walikata kupewa madaraka makubwa wakati hawawezi kuongoza hata mkoa. Watu kama hawa ukiwapa nchi kwa sababu tu ni maarufu, matokea yake ndio hayo. Angetumia busara. If u can't fight them join them. Kashaiingiza nchi kwenye tabu kubwa na siku ya mwisho lazima akimbie na nchi kuwaachia warussia ambao wataweka vibaraka wao pale. Kwa siku ya 3 sasa Ukrane sio ile tena.
Kwa sasa wanazalisha wakimbizi, Miundo mbinu inaharibiwa, watu wanakufa, majengo yanabomolewa.

Kifupi serekali yq Ukraine imeshadondoshwa. Au tuseme imepinduliwa. Ukishaona rais anahutubia akiwa vichochoroni tena kwa kujificha basi jua kazi ishakuwa ngumu.
 

Anapata upinzani mkubwa na Yupo nje ya mji wa kiev?
Huko alikopita amepitaje? Huoni fact ipo wazi kuwa Ukraine anatumia human shields? Na Russia ndicho anacho jaribu kukiepuka ( civilian casualities).....
Resistance anayotoa Ukraine kiev ni kwa Russian saboteur groups sio kwa main force.....
Human shields ndicho kilichoiweka kiev mpaka sasa.....
Kuwafundisha watu kutengeneza motolov cocktail....
Kugawa riffles kwa raia......
General mobilization na nyingine nyingi anazofanya ni mbinu za kuwaingiza raia wa kawaida kwenye Vita iliyotengenezwa na Upuuzi wa raisi wao.
 
Mkuu una points. Ila chanzo mgogoro sio Raisi bali mikataba ya nyuma ya kujilinda mara tu baada ya kusambarika kwa USSR.
 
Serikali ya Ukraine yatia hatarini uhai wa raia wake kwa kuwapa bunduki na vilipuzi na kuwataka wapambane na majeshi/vifaru vya Russia na huku raia hao wakiwa ktk nguo za kiraia na pengine wanajificha kwenye makazi yao.

Majeshi ya Russia yakiwaua raia hao, rais wa Ukraine alalamika kuwa majeshi ya Russia yanaua hadi raia wa Ukraine!
======


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…