Amalizane kwanza na Ukraine ambaye ni weak mbele ya kina Poland na Finland. Russia uwezo wake uko exaggerated tukubali tu, vita atashinda ila weakness ashaonesha.
Ila nadhani inachangiwa na kupigania mjini, uko kwingine aliwashinda walikuwa hawajajipanga na hawakuchukulia serious kama watavamiwa. Haya mambo ya urban warfare Israel ndio wameishi nayo muda mrefu na silaha zao ziko kwa ajili ya urban pamoja na desert warfare. Urusi silaha zake ni za kupigania porini kwenye vast lands maeneo ya Siberia uko. Akitoka hapa atafanya modifications ya silaha na kujipanga dhidi ya vitu kama IEDs vilivyosumbua Wamarekani Uarabuni. Una kifaru kina armour ya kuzuia HEAT shell kikipigwa na rocket kinahimili, ila mpishi wa Ukraine anakirushia chupa ya petrol kinawaka moto, hajatumia hata TSH. 2000.
Kupigana na jeshi linaloungwa mkono na raia ni kazi sana. Kwanza wanoko, ukipitisha vifaru CCTV zao mtaani wanasoma wanawaambia wanajeshi wao mko wapi mnapigwa ambush. Mpaka Urusi baadhi wakavaa sare za Ukraine kufanya infiltration ila mambo magumu bado