Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeelewa kilichoandikwa kweli?View attachment 2131235
Ngoma usiku wa Leo
Kuichukua Ukrain ni ndoto ya asubuhi...Swala la kuungwa mkono sio issue,hata hapa kwetu sidhani kama viongozi wa CCM huwa wana shinda but at the end huwa wanaongoza.Lakini pia Urusi bado ana option ya kuichukui Ukraine nzima na kuifanya sehemu ya Urusi.
Mkuu hizo haziwezi kupigwa, tutasubiri sana..Kwahiyo Putin ashindwe vita ili hali ana silaha ya nuclear?
Hatujafika huko badoTangu vita ianze hizi silaha zimeshatumika?View attachment 2131517View attachment 2131518
Mkuu achana na mashabiki badala ya wanaotumia uhalisia. China ambaye ana strong ties na Russia, mwenye silaha nyingi na teknolojia kutoka Russia, mwenye miradi kibao, anayenunua gesi na mafuta zaidi kutoka kwao kakataa jana kagoma kukaa kwenye baraza la Usalama la UN na kashasema yuko neutral.
Kwahiyo kwa idea yako wewe hayo mabomu yana ukubwa sawa na miji yote hiyo ina ukubwa sawa?Ni kweli Urusi ina Nguvu kubwa Sana za Kijeshi Tena Sana. Lakini hawezi hata siku moja kuthubutu kutumia kombola la Nyuklia kwenye Vita. Kombola la Nyuklia ni kwa ajili ya Duterrence(Kutishia). Kinachosababisha mpaka Sasa NATO washindwe Kuingia vitani kuisaidia Ukraine ni kwasababu Russia ana Nyuklia Waepons ambazo zikitumika Basi NO WINNER,All are LOSSERS.
Urusi ina Makombora 7500 ya Nyuklia kwa takwimu za NIT. Makombora 2500 yako tayari kufyatuliwa kuelekea Endeo lolote Lile Duniani litakapotumwa. Marekani ina Miji mikubwa 358 na Majimbo 54. Kombora Moja linaugeuza mji kuwa Majivu kabisa. Kama Mrusi akituma Makombora yote 2500 kuelekea Marekani,Basi ndani ya dakika 30 hakutakuwa na USA Duniani.
Kwa Upande Mwingine,Marekani ina Makombora ya Nyuklia 6800. Kati ya hayo, 3500 yako tayari kufyatuliwa ndani ya Dakika 5 wakipokea Order na Direction ya kuyafurumusha. Urusi ina Miji mikubwa 43. Endapo USA akiona Russia kashatuma Makombora Yake kuelekea Marekani na hakuna jinsi Basi ndani ya Dakika 5, Makombora 3500 ya Marekani yatakuwa njiani kuelekea Urusi kuteketeza Miji 43,Ndani ya Nusu saa hakutakuwa na Urusi Tena. Hiyo inaitwa MUTUAL ASSURED DESTRUCTION(MAD).
Haya Sasa,Tuseme wewe ni Raisi wa Russia,utarusha hayo Makombora kuelekea Marekani au utafanya juhudi za majadiliano?
Mwishoni mwa Vita baridi kabisa (1988) Nchi za Marekani na Urusi Zilikuwa na Akiba ya Makombora 127,000 (Laki moja na elfu ishirini na Saba). Kati ya hayo, 58,000 ya Urusi na 69,000 ya USA. Embu fikilia. Kombora Moja linafuta mji mmoja wa Dar. Je,Dunia ina Miji 127,000? Jibu ni Hapana.
Kwahiyo ndugu yangu usiwe na tempa unapokuwa unachangia hizi maada,tumia Logic utaelewa tu.
Urusi na Marekani wanajuana,wakikutana Anga Furani Kila mmoja anaangalia Nani anamaslahi makubwa na anamwachia ili kuepusha Vita.
Georgia Mwaka 2008 Marekani hakuingiza mguu kusaidia Nchi hiyo dhidi ya Uvamizi wa Russia kwasababu Marekani anajua hapo Russia ana maslahi Makubwa.
Iraq mwaka 2003 Russia hakutia Mguu kwasababu Marekani alikuwa na Maslahi Makubwa.
Libya mwaka 2011 Russia hakutia Mguu kwasababu USA alikuwa na Maslahi Makubwa.
Venezuera Marekani aliogopa Msululu wa wakimbizi kumiminika nchini Marekani hata Kama angeliamua Vita Urusi angelipisha Coz pale ni Maslahi Makubwa ya kiusalama kwa USA.
Syria pale Wote Urusi na USA wanamaslahi na ndio maana mpaka Sasa wameigawana kijanja. Urusi inamhitaji Assad kwasababu Anamdai pesa ndefu. Marekani anahitaji Mafuta ndio maana mpaka leo Majeshi ya Marekani yapo Syria kulinda Visima vya Mafuta.
Kuhusu Ukraine,hata Marekani anajua kabisa Maslahi ya Urusi ni Makubwa kwahiyo lazima akae pembeni. Atashiriki tu kijanja lakini sio moja kwa moja.
Kuhusu NORTH KOREA,Yeye Ana Mabomu 10 TU ya Nyuklia kwahiyo hata akiacha atupe Mabomu yake Marekani atateketeza Miji 10 ya Marekani Kati ya 358. Kwa upande mwingine,NORTH KOREA ana miji 7 Mikubwa. Marekani akituma Makombora Yake ya Nyuklia 3500 nadhani unaona kabisa Makombora Mengine hayana pa Kupiga kabisa.
MTz 255Dar.
Hizo za juu ni S300 au s400Tangu vita ianze hizi silaha zimeshatumika?View attachment 2131517View attachment 2131518
Jamaniii nimelia☹️😟😒😢😢😢
Daaah aisee kweli haya yanaangaliwa na NATO lakini wanaona kawaida?
Hapa uliuliza jana, ila hadi sasa hazijaisha. Tukiwaambia Russia imeonesha weakness wanaleta visingizio. Imagine Russia inamiliki anga la Ukraine, imeshambulia airbases na inafly air sorties free bila upinzani ingawa inasemekana (sijapata ushahidi wa picha, ndege kubwa haipotei tu hewani ilidondosha) Ilyushin Il-76 transport aircraft imedondoshwa jana na inasemekana ilikuwa na wanajeshi. Nimeona clip yenye roud bang na explosion na debris kubwa zikidondoka ila hakuna ushahidi kama ni transport aircraft, yaweza kuwa jet ilikuwa na mabomu mengi.
Russia inamiliki bahari nzima kuzunguka Ukraine inafyatua makombora ikijisikia, inafanya cyber attack kutokea Belarus. Kwenye ground ambako Russia ndio huwa ina nguvu sana bado inapata upinzani mkali. Sasa imagine uikutanishe na nchi zenye Navy, Airforce na cyber warfare imara. Achana na nuclear weapons hapa hazina matumizi
Mkuu una points. Ila chanzo mgogoro sio Raisi bali mikataba ya nyuma ya kujilinda mara tu baada ya kusambarika kwa USSR.Shida kubwa nayoiona kwenye huu mgogoro ni rais wa Ukraine. Jamaa anaonekana hana sifa zozote za kiuongozi zaidi ya kuwa maarufu kwenye comed na Burudani nyingine za hovyo.
Huyu ni aina ya Watu kama George Weah na kina Bob Wayne. Ambao walikata kupewa madaraka makubwa wakati hawawezi kuongoza hata mkoa. Watu kama hawa ukiwapa nchi kwa sababu tu ni maarufu, matokea yake ndio hayo. Angetumia busara. If u can't fight them join them. Kashaiingiza nchi kwenye tabu kubwa na siku ya mwisho lazima akimbie na nchi kuwaachia warussia ambao wataweka vibaraka wao pale. Kwa siku ya 3 sasa Ukrane sio ile tena.
Kwa sasa wanazalisha wakimbizi, Miundo mbinu inaharibiwa, watu wanakufa, majengo yanabomolewa.
Kifupi serekali yq Ukraine imeshadondoshwa. Au tuseme imepinduliwa. Ukishaona rais anahutubia akiwa vichochoroni tena kwa kujificha basi jua kazi ishakuwa ngumu.
Huu ndo ukweli, kujifanya kushangilia Vita wakati hata tairi ya baiskeli ikipasuka unakimbia ni Uzuzu.Hakuna vita rahisi, wote sisi humu ni mashabiki maandazi tunaosubiria misaada..