LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Haviwezi kuja endelea... Sababu hizo nchi za ulaya zinategemea uwepo wa Russia ili kufanya uzalishaji katika nchi zao. Urusi si ndio mzalishaji mkubwa wa gesi hapo ulaya..?? Na inasambaa nchi nyingi za ulaya..??
Ukiangalia statistics kwenye site ya worldmeter US ndio mzalishaji mkubwa
 
Daaah aisee kweli haya yanaangaliwa na NATO lakini wanaona kawaida?
Hawana Cha kufanya.
Wao hulinda maslahi ya M'NATO mwenzao of which Ukraine sio. Sema jirani na Ukraine Kuna Poland ambae ni M'NATO, so akiguswa yeye hata Kwa bahat mbaya ndo wataingia.
 
Too low....
Kwa nnavyoyafahamu maandiko yako humu ndani mkuu, hukupaswa kuandika hivi
Umeandika kishabiki sana.....
 
Yaani mtu anawaka kwenye kifua jamanii😢😢Mungu aweke muafaka mgogoro uishe
Hapa hakuna Mungu... Huyu ni shetani kazini... Putini lazima alipe..vyovyote iwavyo.. lazima achunwe ngozi akiwa hai..
 
Gharama iko kila upande..
Kule Urusi wanakamata waandamanaji wanopinga vita hii. Urusi kwenyewe baadhi ya wananchi na baadhi ya Majenerali wa zamani hawataki hii vita..
 
Putin amechanganyikiwa alidhani mambo rahisi sana..
Ukitaka kujua kwamba kachanganyikiwa tazama alivyokuwa anawaambia wanajeshi wa Ukraine wamgeuke Rais na serikali yake....tazama body language...sauti yake...he looks fucken confused....dunia imebadilika sana....
Tutafika tu
God Bless our Children.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 

Hautukatai kaka embu chukulia mfano mafuta wachukulie nje na ulaya unategemea nini kwenye soko? Price fluctuations bei itapanda sana na kumbuka nishati ya mafuta kila siku inapungua ndomana wana encourage kuingia kwenye technology ya magari ya umeme. Expect bei kupanda sana aseee mzee uchumi haupo kama unavofikiriaa wewe bei za mafuta zitapanda sana sio ulaya tu hadi africa mkuu.

Umeshaambiwa 75% ya nishati Europe inatoka russia sasa asitishe unategemea nini? Wote wataathirika na sio kwamba russia hawezi uza mafuta au gas atauza sana tu aseee coz soko lake lipo kubwa kwa sasa
 
Mbona marekani hakulipa kwa nchi alizozitendea unyama kwa ubabe wake, hatujasahu bado ya Syria, Iraq na Libya au kisa tu safari hii wanapigwa wao
Hapa hakuna Mungu... Huyu ni shetani kazini... Putini lazima alipe..vyovyote iwavyo.. lazima achunwe ngozi akiwa hai..
 
Sorry mkuu. Hamid Kharzai aliyekuwa Rais wa Afganstani alikwa chagua la wananchi au chaguo la Marekani?
The same kwa Libya. Aliyepewa nchi baada ya sheikh Ghadaffi kundolewa alikuwa ni chaguo la walibya au alikuwa ni chaguo la westen country? Hivyo hivyo kwa Iraq.
Ziliesky atadondoshwa soon. Ukraine itakaliwa kwa muda na russia. No matter how long. Hali itatulia na maisha yataendelea.
Mpaka sasa loser ni Ukraine.
 

Mkuu hv unafikiri russia kapeleka jeshi lake kamili kapeleka vibaraka tu. Na ukraine pia usiichukulie poa mzee wako vzr ila russia akiamua ni dakika tu. Na russia anajitahd kuichukua russia bila kuleta maafa makubwa. Shida media za magharibi zinawadanganya sana marekani ni propaganda tu na putin ameshawasoma vizuri.

Lile lililotabiriwa kwenye biblia naona linatimia aseee mmarekan ataanguka tu
 
vita haina macho.
tunawaomba watanzania walio kwama huko wajifiche sehemu salama.
Kiev inashambuliwa kwelikweli.
 
Alipe gharama gani..
Yeye yuko kwenye nchi yake..anongelea nchi yake..anaweza kujiunga na upande anaoutaka hii ndio maana ya sovereignty..
Hata akiongea mangapi Russia inamuhusu Nini Kama sio ubabe tu..
 
Ukraine was corrupt under Viktor Yanukovych aliyekuwa team Russia, kama unavyoona Lukashenko wa Belarus. Ukraine ilikuwa inaongozwa na remnants wa USSR wezi na hawajui modern economy wala hawawajibiki kwa raia. Ikatokea raia wakachoka kuchezewa wakafanya maandamano Maiden square (ingawa yalisaidiwa na Western countries kwa kiasi fulani). Yanukovich anakimbilia Urusi na fedha za hazina ya serikali.

Waliobaki ni walewale wamelelewa na mfumo wakaja wakapuyanga. Unamtoa Magufuli unamuweka Samia ila wote walizaliwa na kulelewa CCM. Unamtoa Samia unamuweka Januari Makamba au Nchemba ila wote ni walewale. Mwishowe rushwa haikuisha, jeshi bado likawa corrupt na disorganized, wafanyabishara wakubwa wakabaki ndio wamiliki wa kauli za serikali kupitia vibaraka wao.

Ukrainians wakagundua kumbe ukitaka kuondoa shida zote ondoa mfumo wa hizo shida usiondoe mtu pekee yake. Ukraine haikuwahi kuwa na Rais asiyepitia bungeni, baada ya kumtoa Yanukovych 2014 akakaimiwa na Spika, uchaguzi wa 2014 akashinda Petro Poroshenko akashindwa kuleta mageuzi, 2019 akatokea mchekeshaji huyu Volodymyr Zelensky akashinda. Kabadili mifumo, jeshi sio corrupt tena, hakuwahi kuwa mbunge wala mwanasiasa hivyo halindani na mtu wala hana wa kumlipa fadhila, hana team anajali utendaji, kaondoa uongozi wa jeshi uliopanda kimagumashi hata sifa hauna kaweka mkuu wa majeshi mdogo tu hata cheo kaishia Lieutenant General. Wizara zake za Ulinzi, Mawasiliano na Mambo ya Ndani naona zinapiga kazi nzuri sana. Balozi wake wa UN nimemkubali, Waziri wa Mambo ya Nje ndio usiseme.

Marekani imemwambia imkomboe imtoroshe akawajibu "Nataka silaha sihitaji usafiri". Kutoka kuwa Mpoki unavaa makatuni mpaka kuwa Rais gangwe!
 
Usiwe twisted na media za NATO, Russia wakiamua kuonesha kila kitu kinachoendelea Ukraine dunia italia yote. Kuna ka video jana akili trend kidogo ni noma. Unajua mpaka rais wa Ukraine anaamua kuomba po siyo mchezo. China kupitia Balozi wao kawaumbua UN kwa kuwaambia haungi mkono maazimio yeyote na Russia kajipiga kura ya VETO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…