Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mdogomdogo TU tutaelewana,hatimae NATO out.
 
Aisee naangalia hapa Al jazeera KHARKIV kumebaki magofu. Jmn hii vita sio tena ya kuombea UKRAINE ashambuliwe, ni muda sasa wa kumuomba PUTIN asitishe maana ni hasara sana kwa UKRAINE.
Nimejikuta nawaonea huruma hawa UKRAINE. Pia mji wa MARIUPOL umebakia magofu kabisa, tuache utani na ushabiki maandazi, URUSI sio wa kuvheza nao.
 
basi uko sahihi,ukraine anashinda hii vita mapema kabisa,muda utasema...
 
Maafisa wa kijeshi wa Marekani watoa neno kuhusu kombora la haipasoniki ambalo Russia kalitumia kuangamiza ngome ya kijeshi magharibi mwa Ukraine.

Maafisa hao wanasema kuwa nchi yoyote yenye makombora ya haipasoniki inakuwa na nafasi nzuri ktk mashambulizi kwa kuwa makombora haya huweza kupenya mfumo wowote ule wa kulinda anga unaotumika ktk zama za sasa.


 
Mkuu turudi vitani kidogo, vp UKRAINE anashida hii vita?
Kushinda ni swali la ufafanuzi. Ukraine haina uwezo wa kuvamia Urusi. Wakizuia Urusi kuteka sehemu kubwa za Ukraine pamoja na Kiev, inaweza kutosha maana itakuwa aibu kubwa kwa Urusi na kumlazimisha Putin kumaliza mashambulizi. Ila itagharamia Ukraine sana.

Ni dhahiri pia Putin atatafuta hali ambako anaweza kusema "Tumeshinda" au angalau "tumetimiza shabaha yetu" kwa namna fulani. Inamgharamia sana vilevile.

Natumaini kwamba pande zote zitatumia ujanja unaowaruhusu kumaliza hata kama watahitaji kujidanganya wenyewe. Jambo hili baya mno.

Binafsi nahisi Putin angestahili kupelekwa mahakamani kwa jinai za kivita. Lakini isingekuwa busara maana hatma ya wanajeshi pande zote mbili na watu raia wa Ukraine inataka kumaliza haraka na hoja la kumweka Putin mahakamani ingeongeza ugumu wa kumaliza.
 
Apelekwe mahakamani wakati huo OBAMA na BUSH wapo uraiani??
 
Sorry. Nikweli nimeku qoute kimakosa. Ilikuwa imfikie Pietro aliyekuwa akipambana kama vile kuna tuzo angepata. Sorry
 
Tunaomba link ya vyanzo vyako
 
Baada ya jana Kutumia Hpersonic missiles....
Leo imethibitika kuwa Russia ameanza kutumia makombora ya Thermobaric, ambayo yanasifa yakunyonya hewa yote around, na kutengeneza Vaccum.

Hii video ni ya majaribio
Your browser is not able to display this video.


Na hii ni ikiwa kwenye real Use, Ukraine.
Your browser is not able to display this video.


Nimeanza kuelewa kwanini alikuwa anasita kushambulia, na kwanini yeye ndio alikuwa analazimisha Humanitarian corridors.
TUIOMBEE UKRAINE, TUWAOMBEE VIONGOZI WA UKRAINE WAPATE FAHAMU, WAKUBALI YAISHE.
 
Kwa matumizi ya silaha hizo Urusi imepata faida gani? kile walichoharibu waliweza kuharibu pia kwa kutumia makombora ya kawaida (na wamefanya kwenye magharibi ya Ukraine, ingawa walipiga mahali pachache hadi sasa). Kombora ya hypersonic aina uharibifu mkubwa kuliko crusie missile ya kawaida. Fauda yake ni inaweza kuepukana na silaha za kuangusha makombora kwa sababu ni haraka mno.

Sielewi vema mantiki kufichua silaha hizo ambazo hadi sasa zilikuwa siri yao. Sasa yameanza kupimwa na kuchunguliwa na NATO. Ila hata cruise missile za kawaida, uwezo wa Ukraine kuzizuia si kubwa maana wanatumia zile SS3 za zamani walizorithi wakati wa uhuru. Kwa hiyo sioni faida ya kijeshi katika vita hii.
Labda walitaka kuonyesha NATO eti muone tuna vitu gani. Ila nahisi NATO watafurahi zaidi wakipata nafasi kuona na kupima zaidi silaha hizo zilizokuwa mpya na tabia zake haijulikani bado.
Itachukua muda kidogo hadi Marekani watapata silaha hizo pia. Hadi wakati wataendelea na tishio la nyuklia. Maana hata Warusi kama wangejaribu kuwashambulia NATO kwa makombora hayo ya kasi zikibeba mabomu ya nyuklia (inayowezekana) wangefaulu kpata mafanikio zaidi mwanzoni. Ila mara vita ya nyuklia inaanza, pande mwingine ina makombora ya kutosha kwenye maficho chini ya ardhi na milima na chini ya bahari yatakayommaliza mshambuliaji. Halafu kama ni kubwa, pamoja na Afrika ya Mashariki (nimeeleza habari za mnururisho na nuclear winter awali).
Kwa hiyo naombea punje ya hekima kwa viongozi pande zote mbili wakumbuke hayo na wasiendelee mbali kuliko mabaya yanayotokea sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…