LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
1645695114076.png

Watu saba wanaaminiwa kufariki katika shambulio la bomu llililofanywa na vikosi vya Urusi, Polisi wa Ukraine wanasema.

Maafisa wanasema shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Podilsk, nje ya mji wa Odessa liliwaua watu sita na kuwajeruhi wengine saba. watu 19 hawajulikani waliko huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki katika Mariupol, waliongeza kusema.

Huku hayo yakijiri Wizara ya Ulinzi ya Urusi imenukuliwa na shirika la habari la Urusi -Interfax ikisema kuwa "Ulinzi wa anga wa vikosi vya jeshi la Ukraine umekandamizwa".

Wizara inaongeza kuwa "vikosi vya mpakani vya Ukraine havikupinga vitengo vya Urusi".

Hakujawa na uthibitisho wa madai haya.
 
Wakuu, Baada ya Russia kupeleka jeshi kubwa mno kwenye mpaka wake na Ukraine, mataifa makubwa Duniani yalihamaki yakiongozwa na Marekani.

NATO ilisema wazi kwamba haitaiacha Ukraine ikiwa yatima,na tayari muungano huo wa kujihami wa Ulaya magharibi na Marekani umeimarisha vikosi vyake Poland na Estonia.

Russia imepeleka zaidi ya wanajeshi 130,000 kwenye mpaka wake na Ukraine na wakati wowote wanasubiria amri ya Rais Putin Kuivamia Ukraine.

Baada ya Russia kuimega Crimea na Dunia kukaa kimya,Putin alidhani itakuwa rahisi pia Kuivamia Ukraine na kufanya lolote sasa mambo yamekuwa Tofauti.

Uingereza imepeleka shehena kubwa mno ya silaha mbalimbali Ukraine na makomandoo wa kikosi maalumu cha SAS.

Canada nayo imesema haitaiacha pekee yake Ukraine itaipa misaada yote ya kijeshi dhidi ya uvamizi wa Russia. Kwa hiyo Russia inafikia hatua wanaogopa wakijua wazi kwamba kushinda vita kwao itakuwa ngumu mno.

Na hakika Russia ikijaribu kuivamia Ukraine haitashinda hii vita zaidi ya kuharibikiwa kiuchumi. Russia ni nani hasa hata ashinde vita dhidi ya Marekani, Uingereza, Canada na mataifa mengine mengi ambayo yanaisaidia Ukraine bila kuitangazia Dunia.

Mengine yabakie ushabiki tu, lakini Russia haitashinda hii vita na wao wameshaliona hilo.

View attachment 2119949
kama huijui Urusi basi fumbua macho hutoamini utakacho kiona
 
What if Ukraine wana secret nuclear warhead wakaamua kufanya suicide wakapiga Moscow??... 😀 😀
Moscow huwezi piga Bomu lolote, wana intercept za maana sana pale. Umefikiria kama mtu usiyepita shule au kufuatilia mambo ya kivita.
 
Wakuu, Baada ya Russia kupeleka jeshi kubwa mno kwenye mpaka wake na Ukraine, mataifa makubwa Duniani yalihamaki yakiongozwa na Marekani.

NATO ilisema wazi kwamba haitaiacha Ukraine ikiwa yatima,na tayari muungano huo wa kujihami wa Ulaya magharibi na Marekani umeimarisha vikosi vyake Poland na Estonia.
Mkuu umeshaamka kwenye ndoto yako ya mchana?

Kama hujaamka tambua kuwa Putin wa Russia anachapa miundombinu ya kijeshi ya Ukraine tena nchini kooote anagonga.

 
Back
Top Bottom