Adriz,
Hiki kitabu "Khrushchev Remembers,' ninacho toka 1970s na hiyo si cover yake kimefanywa binding kukihifadhi.
Humo ndimo Khrushchev anamueleza Tito alivyoweza kuwafurahisha wananchi wake kwa kupunguza "restrictions," za Ukomunisti.
Hii ikaifanya Yugoslavia iwe tofauti sana na nchi nyingine za Ulaya ya Mashariki.
Ndiyo hayo ya Mick Jagger na Rolling Stones na mavazi kama jeans niliyogusia katika video.
Mtu akitaka kujua shida iliyowafika Warusi WWII asome kitabu hiki "The Rise and Fall of The Third Reich," vipi Red Army ilivyopambana na Manazi wa Ujerumani.
Kama si "General Winter," Wajerumani walikuwa wanaiteka Urusi sijui dunia ingekuwaje hii leo.
Anahitaji mtu kuwa na "background," hii kuweza kuelewa mgogoro huu na kwa nini baadhi ya nchi zilizokuwa katika Soviet Union ziligeuka kuangalia Magharibi.
View attachment 2131472View attachment 2131476