LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Sviatlana Tsikhanouskaya mwanaharakati wa Belarus anafanya mobilization afanye mapinduzi amuondoe Alexander Lukashenko aliyepitisha majeshi ya Urusi kwake kuingia Ukraine.
Kuna raia 50 wa Belarus wamejitolea kuipigania Ukraine wako frontline. Urusi inaonekana haijatumia wanajeshi wazoefu imeleta wengine ni drafted
 
Mzee hiyo taarifa ni ya uongo! Ukraine wanafanya propaganda nyingi sana zinazowasaidia kipindi hiki cha vita. Warusi wakizisoma zinawachanganya na waanaandamana nchini kwao. Hivyo Putin anapata pressure ndani ya nchi.

Kingine ni morali. Ina busti morali ya jeshi na raia ndani ya nchi kupambana na Urusi. Taarifa uliyoiweka mamlaka ya Uturuki imekanusha baada ya Zelensky ku-tweet hivyo. Nusu saa iliyopita walishakanusha hiyo habari.

View attachment 2132074
Screenshot_20220226-175742_1.png
 
Wengi hawataki kukubali ukweli huu kwamba hii vita Putin kaingizwa chaka, na ajiandae kwenda kuwa mkimbizi China. Ufaransa ashaanza kutanguliza msaada wa silaha kabisa. Baada ya hilo kombora kuangushwa Poland Kitachofata itakuwa ni jeshi na sio msaada wa silaha peke yake.
Muda ni Mwl. mzuri.

Tusubiri.
 
Inasemekana ishapangwa kabisa vijana wa myahudi (jeshi la Ukraine) watafute kombora moja tu la Mrusi walivugumize Poland ili wanaume wa kazi wakiongozwa na baba yao USA waingie kazini kumalizia mission yao. Ikumbukwe kwamba Poland ni moja kati ya nchi wanachama wa NATO waliokaribu kabisa na ukanda huu wa vita. Na kwa vile sheria za NATO zinaruhusu mataifa hayo kuishambulia nchi yoyote inayomvamia mwanachama wao, basi hii ndio itakuwa njia rahisi ya wao kutimiza malengo yao walioyapanga muda mrefu. Ikumbukwe pia katika siku za hivi karibuni za mzozo huu Marekani na baadhi ya nchi wanachama wa Umoja huo wa NATO wamekuwa wakipeleka silaha nzito nzito na wanajeshi zaidi katika nchi ya Poland, Lithuania na baadhi ya nchi zingine wanachama zilizo katika ukanda huo, lengo ni kutaka kutengeneza mazingira ya kuivamia Urusi kupitia kila upande wa nchi hizo wanachama ambazo tayari kwa muda mrefu nchi hizo zina silaha na wanajeshi wa NATO karibu na mipaka ya Russia. Kitendo cha Mrusi kuivamia Ukraine ambayo bado haijawa mwanachama wa NATO wala umoja wa Ulaya huku akiziacha nchi ambazo tayari zishajiunga umoja huo muda mrefu na ni jirani zake, kimewashangaza wengi. Kama lengo ni kuzuia upanuzi wa NATO katika eneo hilo anaziachaje nchi jirani zake kama Latvia, Estonia na Lithuania ziendelee kutamba na silaha hizo za NATO badala yake anaenda kuivamia nchi ambayo bado haijafikiriwa hata kuwa mwanachama halisi wa umoja huo?

View attachment 2132090

View attachment 2132091
Oyaa acha hizo basi... [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Yaan wewe ujue huo mpango na URUSI wasijue??
 
Hivi vita kwa sasa bado ila pale warusi watakapoingia kwenye jiji kama Kiev na wanajeshi wa Ukraine kuvua magwanda na kuvaa kiraia ndio warusi wataimba kikwao.

Kule nyumbani Russia wananchi wataanzisha maandamano nchi nzima kudai askari wao warudi nyumbani baada ya kuanza kuona mifuko ya plastiki zenye maiti za wanajeshi wao zikirejeshwa nyumbani.

Huo muda unakuja na hauko mbali na tena itakuwa ni mbaya kuliko ile ya wamarekani kule Iraq.

My Take: Inaonekana huu ndio mwisho wa utawala wa mbabe Putin na atakuwa ni Hitler mwingine sidhani kama mwaka 2023 Russia itakuwa tena na Putin kama rais wao.

Ninachoona, baada ya Putin kuondoka "Post Putin Russia", nchi hiyo itabadilika sana na itakuwa kama Japan au Ujerumani kwani wataachana kabisa na mambo ya vita "Belligerency" na watajikita zaidi kwenye mambo ya maendeleo ambapo baada ya miongo kadhaa watakuja kuwa na uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.
 
Unachokataa ni nini? Hii ni taarifa ya Zelensky.

View attachment 2132087

Hii ni taarifa ya kutoka Uturuki kukanusha hiya taarifa.
View attachment 2132088
Ni juu yako! Kuchagua kuamini au kutoamini. Muda huu An-26 ya Ukraine imelipuliwa.
Ninachotaka kukuonyesha ni kwamba hakuna jambo utakalolijua wewe uliyepo huku halafu wenyevita vyao wasilijue boss. Kama unajua ni propaganda na ni kweli ni propaganda basi na russia wanajua ni propaganda.
 
Jamaa una wivu juu ya kutojua kuelewa kinachoendelea. Yani unaona umepoteza sana ndio maana emoji za kujichekesha haziishi kwako. Kuna mada za ufyatuaji matofali, kilimo cha pilipili, ufugaji wa mabata, n.k zipo unaweza enda kuchangia, humu huna tija unaongeza emoji tu.

Hujui unachopinga, hutoi facts wala huna source za info kazi kubisha. Wenzako wanatoa hoja we unapinga kisa ni "Watanzania"
Nina wivu na Russia, Eukrain au nina wivu na wewe? Una stress.
 
Urudi chini ya Putin, wamepigana Vita 7 na zote wameshinda.


In fact kwenye hostoria yote ya vita vya urusi... HAWAJAWAH KUSHINDWA.


Ni suala la muda , serikali ya Kyiv alichofanya ,nikuweka Majeshi mengi kwenye mji mkuu, ndio sababu Urudi wanapata shida .


Ila lazima watoboe..... Urudi keshapigwa vikwazo, hana tena cha kupoteza, ni kupiga tuu.

Yaan nikm Tundu Lissu alivyopigwa Risasi alafu akapona .
Urudi,urudi,urudi?????
 
Sviatlana Tsikhanouskaya mwanaharakati wa Belarus anafanya mobilization afanye mapinduzi amuondoe Alexander Lukashenko aliyepitisha majeshi ya Urusi kwake kuingia Ukraine.
Kuna raia 50 wa Belarus wamejitolea kuipigania Ukraine wako frontline. Urusi inaonekana haijatumia wanajeshi wazoefu imeleta wengine ni drafted
80% ya jeshi la Mrusi bado lipo mpakani.

Kuna wanamgambo wa majimbo yaliyojitoa Ukraine nao wanapambana.

Kuna wanamgambo 1000 kutoka Chechen jana wamejitolea kwenda kupigana kwa kuiunga mkono Urusi. Wanne kutoka Chechen tayari wameshauliwa. Wamepigwa ambush hiyo hatari.

Ukraine hii vita akitaka kuirefusha na kumsumbua Urusi apige ambush kama wapakistani. Akienda nao kimpambano huu anaokwenda nao atamalizwa. Kwa sababu Urusi ameshambulia base za Ukraine nyingi sana. Ghala za kuhifadhia silaha nyingi zimeteketezwa. Mifumo yake ya anga imekuwa ya kusuasua sana.

Amegundua mwishoni anaanza kujichanganya makazi ya raia. Swali muhimu Ukraine wanaweza wakairefusha vita kwa muda mrefu kama wapakistani? Kupigana kwa ambush?

Lakini kingine cha hatari zaidi Urusi ametumia vifaa vya zamani kupambana na Ukraine. Zana za zamani tofauti na za sasa. Za zamani athari ya mlipuko ni ndogo si kubwa. Na kufanya hivi ni kuzuia uharibu mkubwa usitokee kwenye makazi ya watu, miundombinu na kusababisha athari kwa raia wa kawaida(maafa).

Tayari Urusi imebadili mbinu wanatumia drones sasa hivi. Ikiwa hali itaendelea hivi maafa kwa Ukraine yatakuwa makubwa.
 
Tuseme chanzo ni Marekani na washirika wake kutaka kuweka silaha zao za Nuke Ukraine kwa kupitia mgongo wa Ukraine kujiunga na NATO.

Mkataba wa Minsk uliosainiwa sijui miaka mingapi iliweka wazi kwamba NATO haitaendelea kujitanua kuelekea upande wa Urusi hivyo kitendo cha NATO kutaka kupokea Ukraine ni kuvunja mkataba huo.

Hii ndiyo maana Putin amezionya Finland na Sweden nao wakijifanya kutaka kujiunga na NATO watapigwa vibay
Tuseme chanzo ni Marekani na washirika wake kutaka kuweka silaha zao za Nuke Ukraine kwa kupitia mgongo wa Ukraine kujiunga na NATO.

Mkataba wa Minsk uliosainiwa sijui miaka mingapi iliweka wazi kwamba NATO haitaendelea kujitanua kuelekea upande wa Urusi hivyo kitendo cha NATO kutaka kupokea Ukraine ni kuvunja mkataba huo.

Hii ndiyo maana Putin amezionya Finland na Sweden nao wakijifanya kutaka kujiunga na NATO watapigwa vibaya.
Mkuu wangu, soma tena hiyo Minsk agreement inasema nini. Hakuna hayo mambo ya NATO.

Minsk agreement ni kati ya Russia na Ukraine na ilisainiwa kuanzia 2014 baada ya ile vita ya 2014 ya Russia kuivamua Ukraine. Hakuna NATO kwenye mkataba huo.

Huo mkataba wa nato kukubaliana na Russia kuhusu expansion kwenda East haupo. Kama upo nionyeshe link yake. Kulikuwa na mazungumzo wakati ule wa Yeltsin kutaka USA itoe guarantee hiyo Lakini Bill Clinton alikataa. Pia rais Bush na yeye baadaye alikataa.
Soma maneno ya Clinton hapa chini.

Declassified White House transcripts also reveal that, in 1997, Bill Clinton consistently refused Boris Yeltsin's offer of a 'gentlemen's agreement' that no former Soviet Republics would enter NATO: "I can't make commitments on behalf of NATO, and I'm not going to be in the position myself of vetoing NATO expansion with respect to any country, much less letting you or anyone else do so…NATO operates by consensus."

Putin is a bully and needs to be stopped.
 
Back
Top Bottom