LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Uzi wako umejaa propaganga kuliko uhalisia, sema unahoja[emoji106][emoji4]
 
Wale wanaokufa na njaa kila siku. Uchumi wao unazidiwa hata na huu wa kwetu. Kiduku bure kabisa.
Ebu tuache kusikiliza propaganda za US, yaani nchi iwe na uwezo wa kutengeneza nyuklia na kuzi maintains, iweze kutengeneza silaha zake mwenyewe, magari na hata communications system yake na iweze ku survive vikwazo kwa miaka yote then useme Ina uchumi mbovu kulinganisha na nchi inayo import almost kila kitu!?
 
Wakuu, hii dunia vita ni jadi yake.

Asipopigana Urusi, atapigana Mmarekani, akipumzika huyo, Israel na Palestina wanakiwasha, hao wakichoka kuna vita somewhere in Africa.

Kuna kipindi hapa katikati palitulia kidogo nikajiuliza kulikoni, sisikii vita? Hadi kuna nchi unajiuliza kama bado zipo. Dunia ni uwanja wa vita, imekuwa hivyo siku zote.

Hii vita nayo itaisha tu kuipa nafasi nyingine, hii si mara ya kwanza Urusi kumtandika Ukraine. Nadhani Ukraine aache ukorofi na kumsikiliza sana Mmarekani anayemchochea kwa nia ya kumchokonoa Mrusi.
Vita hata kwenye biblia watu walipigana sana. Dunia haiwezi kutulia kamwe. Watu wa congo, Uganda, rwanda na burundi watupumzishe kwanza, tunataka tuone show ya vyombo vipya
 
Ukraine Konflikt | Präsident Volodymyr Zelenskyy

Rais Zelensky hajulikani aliko​

Inaelezwa kwamba aliko Rais Zelensky ni suala lililowekwa siri baada ya mwenyewe kuwaambia viongozi wa Umoja wa Ulaya kwamba ni mtu wa kwanza katika orodha ya watu wanaolengwa na Urusi.

Japokuwa rais huyo ametoa pendekezo la kutaka mazungumzo na Urusi kuhusu madai muhimu yaliyotakiwa na Moscow, ambayo ni kuitaka Ukraine itangaze kuwa haina upande na itaaachana na dhamira yake ya kutaka kujiunga na NATO.

Urusi kwa upande wake imejibu pendekezo hilo ikisema iko tayari kutuma ujumbe wake nchini Belarus kuyazungumza hayo.

Mwandishi: Saumu Mwasimba

Mhariri: Mohammed Khelef
DW Kiswahili
 
Tusidanganyane Russia kashindwa ingia Kyiv

Mji Mkuu wa Ukraine wamechakazwa hasa, labda watumie drone
 
Back
Top Bottom