LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Changamoto zipo! Baadhi ya miundombinu zimeharibiwa, hasa viwanja vya ndege. Silaha zinaingizwa hasa kupitia Poland, magharibi mwa Ukraine.

Mbinu zinazotumika kuzisafirisha ndani ya Ukraine ni za siri kijeshi. Kinachofahamika ni kwamba, usafirishaji hauhusishi misafara mikubwa ama convoys. Pia, msafara unahusisha mifumo ya ulinzi kama stinger missiles dhidi ya ndege za kivita zinazoweza kutumwa na adui kujaribu kushambulia msafara wa kupeleka silaha eneo ambalo zitakwenda kutumika.
wewe MKUU unajua hizi njia halaf RUSSIA hawajui
kongole MKUU
 
Ngoja nikusaidie tu.

Kurusha Kombora la Nyuklia kutoka Russia Hadi Marekani itachukua dakika 30 kufika Marekani.

NUCLEAR BASED SILOS (Siraha za Nyuklia za Marekani zilizoko Chini ya Ardhi) Mfano,ATLAS MISSILES,TITAN MISSILE na MINUTEMAN MISSILES Zinaweza kufyatuliwa ndani ya Dakika 5 TU na kuanza Safari ya kuelekea Urusi. Kwahiyo,Makombola ya Urusi na Marekani yatapishana angani Kila Moja yakienda kumaliza kazi iliyotumwa. Baada ya Dakika 30 hakutakuwa na Kitu kinachoitwa Urusi Wala Marekani kwenye Uso wa Dunia. Wingu kubwa la Mionzi(NUCLEAR FALLOUT) na Vumbi litatanda angani Dunia nzima na kuzuia kabisa mwanga wa Jua kufika kwenye Uso wa Dunia. Mimea yote itakufa kwa kukosa mwanga wa jua kwa ajili ya Photosynthesis. Kwa Vile Mimea ndio hutoa Oxygen kwa ajili ya Wanyama akiwemo binadamu Basi Oxygen itapotea yote, Wanyama wote watakufa kwa kukosa Hewa. Matajiri ambao wataweza kupata Artificial Oxygen kwa kutembea na Portable Respirators nao wataanza Kufa kwa CANCER mbali mbali kutokana na Mionzi ya NYUKLIA (Radiations) kuanza kufanya IONIZATION na Kutafuna TISSUE za Miili yao.

Kwahiyo ndugu yangu ukiona mtu anashabikia Matumizi ya Siraha za Nyuklia kisa TU upande wake anaoushabikia ndio ushinde ujue ni Rayman hajui lolote kabisa. Ndio maana ni Mara chache Sana Mimi kuwajibu watu hao japo nina majibu mazuri babiesk.
Mkuu hayo madhara yanajulikana sote tumejifunza kupitia historia ya Hiroshima na Nagasaki,hoja yangu ni kuwa hizo slaa za nyuklia hazikutengenezwa kama mapambo Bali zitumike na lazima IPO siku zitatumika.
 
kwaiyo unataka kunambia angefyata mkia mwenyewe russia?

maana trump yule ni chizi kabisa angeshaanza kuichapa russia
Sifikirii kama USA ange.tia mguu zaidi ya kutoa support tu

Kwanza UVIKo19 umengusha sana chumi za izi nchi kubwa so nafikiri Congress wangefikiria mara mbili na wange kataa tena kama speaker ni huyu mama Nacy yule na Trump ideology zao zilikuwa tofauti
 
Wanachotaka kiwe ni Ukraine iwe uwanja wa vita kwaajili ya kumdhoofisha Urusi... Sasa Ukraine yenyewe wanakaza fuvu wakijua wanasaidiwa kwa nia njema
Kila Nchi ina uhuru wa kujilinda,hakuna sababu ya kulazimishwa,hapo ni kama kusema Nchi jirani ziache kuwa na majeshi au na ushirika wa kijeshi,jambo ambalo haliwezekani.

Screenshot_20220227-231924.png
 
Kama hadi kesho Kyiv itakuwa haijatekwa Urusi hataiteka, maana nimeona reinforcements
Eti ratiba yao ni hadi march 2 so huenda nguvu kubwa ikatumika ndani ya siku hizi ila sidhani kama watafaulu maana wazungu wameamua kuwasaidia Ukraine.

Screenshot_20220227-230718.png


Screenshot_20220227-230229.png


Screenshot_20220227-230158.png
 
Uharisia wa hi Vita bado Ni mgumu hadi pale risasi ya mwisho itavyopigwa,wengi wemekua wanasema urusi inaonenekana kushindwa hi Vita bila kuangalia uharisia,Kama vile mazingira ya mapigano ,uchumi,idadi ya nchi anzopigana nazo urusi kwa Sasa,
-tukianza na idadi ya nchi tunaona karibu nchi zote za magharib zimejiingiza ktk hi Vita indirectly kwa kumpa sapoti ukrain kumuongezea siraha,na kumfunga urusi kwa vikwazo ,
-kwa upande wa mazingira,hapa tunaona urusi anakua na ugumu Sana wa kufanya heavy hambushi kwa hofu ya kuuwa raia wasio na hatia ambambo ukrain imeamua kuwapa siraha wakapigane,hivyo urusi anapigana kwa tahadhari kubwa Sana inayomfanya aende kwa utaratibu,
-aina ya vikosi anavyotumia urusi,kiuhalisia urusi hawezi kupeleka askali wake muhim Kama Chambo wakati hajui aina ya Vita atavyopigana,mda na uzito,hivyo kiasi kikubwa Cha askali anaotumia Ni wale waasi wa chechenia Kama Chambo Cha kupima nguvu za adui zake hivyo Hadi Sasa Ni ngumu kujua Kama urusi ameshindwa au ameshinda,
 
Hujui kwamba Putin alidanganywa kwamba itakuwa rahisi sana kuiteka Ukraine hasa mji mkuu bila kukumbana na ukinzani mkali?

Aliamini anaungwa mkono na wanajeshi wa Ukraine ndipo alipowaambia waipindue serikali yao lakini wamegoma na wameendelea kuonesha utiifu kwa Rais wao ndo maana hadi leo siku ya tatu hajauteka mji mkuu wa Ukraine wala miji mingine mikubwa.

Raia wenyewe wameshika silaha wameingia mitaani kupambana na wanajeshi wa Urusi hadi kufikia wanajeshi wa Urusi kuvaa sare za jeshi la Ukraine ili kukwepa kutunguliwa na raia mitaani.

Hii vita usidhani ni rahisi hivyo Urusi kajiingiza kwenye balaa ambalo hakutarajia.

Marekani na Ulaya wameanza kupeleka vifaa vya kivita kumsaidia Ukraine sasa unadhani hii vita ni ya kuisha leo?
Kwahiyo urusi walikubaliana na jeshi la Ukraine kuipindua serikali yao. Hizi habari wenzetu mnaziokotaga wapi kwani
 
Back
Top Bottom