LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hizi taarifa za media yaani ni mwendo wa kuvuruga akili zetu tu. Maana ninachokisomo naona kinaenda tofauti na tunayopata kutoja kwa jamaa zetu waliopo Ukraine na Russia. Kuna taarifa zingine kwenye Media ni Propaganda
 
Ila nakumbuka wiki mbili zilizo pita waafrika walipo Urusi na Ukraine tulipo wauliza kwamba nini kinaendelea huko ? Kwani vyombo vya Habari vinatuhabalisha habari za kushitua sana huko .

Majibu mengi yalidai mambo Ni shwari tu hakuna tatizo
 
Nimejaribu kuwafuatilia kwa muda humu nimeona wazi watu wengi wanaongozwa na mapenzi binafsi juu ya upande fulan hasa hawa wanaojionyesha NI PRO USA+NATO...unakuta mtu anakwambia eti siku ya tano leo mbona urusi hajaiteka kiyv(ambayo ndio mji mkuu wa ukraine)....HEBU WATOE HISTORY NI LINI NA WAPI MAREKANI WANAOMPIGIA CHAPUO HAPA AMEWAI SHINDA VITA KWA SIKU TANO???..wote tunafahamu humu mwaka 1950 mmarekani alishindwa vita dhidi ya taifa dhaifu kabisa la vietnam vita ile aliyopigana zaid ya miaka 4 na hakutoboa...unakuta mtu anakwambia mbona huyo putin kashindwa kuifanya ukrain majivu...ukweli ni kwamba URUSI HATAKI UKRAINE KUJIUNGA NA NATO NANDICHO ANAPINGA UTANUZI WA UMOJA WA NATO KUINGIZA WANACHAMA WAPYA KINYUME NA MAKUBALIANO AMBAYO AFISA WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE YA RUSSIA ALIINGIA NA NATO 1992...YOTE HII MRUSI AKIWA ANA WASIWASI KUWA WANAWEZA MFANYIA MASTERPLAN WAKAIGAWA ZAIDI RUSSIA KAMA ILIVYOTOKEA KWA USSR HUKO AWALI. na kiuhalisia mji wa kyiv hauna waasi huo mji upo mikononi mwa serikali kwa miaka mingi...mikoa ya ukraine ambayo ilikuwa inawaasi wanaopingana na serikali ya ukraine ni miwili tu LUHANSK NA DONETSK ambayo russia alishasign hati ya kuitambua kama nchi huru na ndio mikoa ya kwanza kuitwaa kabla ya kuingia hapo kyiv tokea usiku wa tarehe: 26 kuamkia tarehe:27...na lengo la urusi si kutake over all the ukraine country ni kumega mikoa hiyo iliyokuwa inakaliwa na waasi na pia kumdhoofisha ukraine ili aachane na mikakati ya kujinga na nato...na mpaka sasa mikoa hiyo ya luhansk na donetsk imeshachukuliwa kutoka mikononi mwa ukraine na

Hadi ile tareh:25 mwezi huu rais wa ukraine aliomba msaada kutoka kwa wajumbe 27 wa nato na wote hawakuwa na dhamira ya msaada na kutoa jibu la moja kwa moja wataisaidia vipi ukraine na kitu icho ndo kimefanya rais wa ukraine kukataa msaada aliotak kupewa na biden kutoka kwenye simu aliyopokea tareh:27 asubuhi kutoka kwa biden...na kwa kitendo icho TAYARI KIMEONYESHA DHAMIRA YA RAIS HUYO KUWA HATAKUWA TAYARI KUJIUNGA TENA NA NATO MARA BAADA YA MZOZO HUU KUISHA MAANA AMEGUNDUA NI WANAFIKI NA NDIOMAANA "ALIANZA KUHIMIZA VITA HII TUTASHINDA NA KILA RAIA WA KIUME UKRAINE WA UMRI KUANZIA MIAKA 18 HADI 60 ASHIKE SILAHA KUIPAMBANIA NCHI YAO WENYEWE"...na ukweli ndo huo marekani na washirika wake wa nato ni wanafiki maana inakuwaje mtu mnayemhimiza ajiunge nanyie nato anavamiwa hadi Mikoa yake ya mipakani LUHANSK NA DONETSK inachukuliwa na amewaomba msaada hamkurespond na baadae ndo mnajifanya kumpigia simu na kumwambia mumsaidie financial wakati mtu anapigwa?...iyo itamsadia nin??...nandio maana rais wa ukraine akakataa hadharani kwenye akaunti yake ya insta hii ilimfanya marekani+nato waonekane hawana nia ya kuisave ukraine...na hatua hii ndo imepelekea USA kujinasibu kuwa itawasaidia ukraine ANTI-AIRCRAFT MISSILE STINGER ...huku nato walikutana kwa dharura na kukubaliana kuongeza SEVERE ECONOMIC SUNCTIONS KWA URUSI NA MAKAMPUNI YAKE....kitu ambacho hata korea kaskazin waliwekewa hivyo vikwazo miaka nenda rudi na bado wanasurvive freshy tu...sikatai itamdhohofisha putin kiuchumi lakini haitofanya lengo lake alitakalo kukamilika kiuhalisia that guy is a COWARD...yaan haogopi ivyo vikwazo na bila shaka alisha asses iyo risk kabla ya kuianza iyo vita hivyo alishacalculate wapi nato watakimbilia before.

UKITAKA KUJUA NATO+USA NI WANAFIKI RAIS WA UKRAINE ALIPOST HII.

IKIWA RAIS WA TURKEY BWANA EDORGAN ANAWEKA WAZI KUWA NATO WANAMFELISHA UKRAINE WEWE NI NANI HUMU JF kuwasifu nato na marekani kama msaada wa ukraine kwenye hii battle???

Ifahamike kuwa russia hajafanya full scale invasion kwa ukraine kama alivyofanya pale syria dhidi ya waasi wa asadi...angefanya ivyo maana ake angetumia kila silaha aliyonayo na ukraine isingekuwa salama hadi ivi sasa...maana inafahamika wazi kiuwezo wa kijeshi Ukraine bado sana kwa russia kwa msiojua labda.

Nato hawana meno direct dhidi ya mgogoro huu...ukilinganisha na madhara ambayo anayapata ukraine!...mitizamo ya watu walio wengi WALITAZAMIA KUMSAIDIA UKRAINE DIRECT KWA KUTUMA ARMED-TROOPS ZIKAMPIGE MRUSI PALE UKRAINE LAKINI CHAKUSHANGAZA KILA ANAYEJITOKEZA KUSAIDIA AKIWEMO CANADA NA UINGEREZA ANATOA MSAADA WA SILAHA KITU AMBACHO SIO GENUINELY KWENYE FIELD OF WAR MAANA WHAT IF WANAJESH WA UKRAINE HAWANA 100% EFFICIENCY YA KUTUMIA HIZO SILAHA ZA MISAADA MAANA HAWAKUWA WAKITRAIN NAZO TOKEA HAPO AWALI NA ZIMEKUJA WAKATI HUU KAMA MSAADA.

Watu waliowengi PRO USA+NATO WANATAZAMIA AIBU AMBAYO ATAIPATA RUSSIA ASIPOWIN HII VITA...WANASHINDWA KUJUA RUSSIA AMESHAPATA 80% YA MALENGO YAKE YAANI AMESHATWAA MIKOA YA LUHANSK NA DONETSK iliyokuwa inashikiliwa na waasi waliyoipinga serikali ya ukraine kama alivyofanya hivyo huko nyuma kwenye rasi ya Crimea iliyokuwa sehemu ya ukraine 2014 na hivisasa ni urusi...kilichobaki ni ukraine kutokubali kuingia NATO tu.

Tokea jana zipo taarifa kutoka kwa rais wa ukraine kuwa kuna mazungumzo kati ya ukraine na maafisa wa urusi yatakayofanyika mpakani mwa jirani yao Belarus...ikumbukwe mkutano huu haujaitishwa na urusi...ni rais wa belarus ndo amefanya juhudi hizi kuwakutanisha majirani zake.

Japo rais mwenyew wa ukraine anasema hana imani kama maongez hayo yatazaa matunda...beleive it makubaluano hayo yanaweza kuwa na kifungu cha kumlimit yeye ukraine kwa maandishi kwamba hatojiunga nato siku za usoni wala hapo miaka ya baadae...sasa itakuwa ni juu yake kukubali au kukataa na kufanya vifo vya watu wasio na hatia viendelee kutokea nchini kwake.
 
Nimejaribu kuwafuatlia kwa muda humu nimeon wazi watu weng wanaongozwa na mapenzi binafsi juu ya upande fulan hasa hawa wanaojionyesha NI PRO USA+NATO...unakuta mtu anakwambia eti siku ya tano leo mbon urusi hajaiteka kiyv(ambayo ndio mji mkuu wa ukraine)....HEBU WATOE HISTORY NI LINI NA WAPI MAREKANI WANAOMPIGIA CHAPUO HAPA AMEWAI SHINDA VITA KWA SIKU TANO???..wote tunafahamu humu mwaka 1950 mmarekani alishindwa vita dhidi ya taifa dhaifu kabisa la vietnam vita ile alopigana zaid ya miaka 4 na hakutoboa...unakuta mtu anakwambia mbona huyo putin kashindwa kuifanya ukrain majivu...ukweli ni kwamba URUSI HATAKI UKRAINE KUJIUNGA NA NATO NANDICHO ANAPINGA UTANUZI WA UMOJA WA NATO KUINGIZA WANACHAMA WAPYA KINYUME NA MAKUBALIANO AMBAYO AFISA WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE YA RUSSIA ALIINGIA NA MAAFISA WA NATO 1992...YOTE HII MRUSI AKIWA ANAWASIWASI KUWA WANAWEZA MFANYIA MASTERPLAN WAKAIGAWA ZAIDI RUSSIA KAMA ILIVYOTOKEA KWA USSR HUKO AWALI. na kiuhalisia mji wa kyiv hauna waasi huo mji upo mikononi mwa serikali kwa miaka mingi...mikoa ya ukraine ambayo ilikuwa inawaasi wanaopingana na serikali ya ukraine ni miwili tu LUHANSK NA DONETSK ambayo russia alishasign hati ya kuitambua kama nchi huru na ndio mikoa ya kwanza kuitwaa kabla ya kuingia hapo kyiv tokea usiku wa tarehe: 26 kuamkia tarehe:27...na lengo la urusi si kutake over all the ukraine country ni kumega mikoa hiyo iliyokuwa inakaliwa na waasi na pia kumdhoofisha ukraine ili aachane na mikakati ya kujinga na nato...na mpaka sasa majimbo hayo ya luhansk na donetsk yameshachukuliwa mikononi mwa ukraine na

Hadi ile tareh: 25 mwezi huu rais wa ukraine aliomba msaada kutoka kwa wajumbe wa 27 wa nato na wote hawakuwa na dhamira ya msaada na kutoa jibu la moja kwa moja wataisaidia vipi na kitu icho ndo kimefanya rais wa ukraine kukataa msaada aliotak kupewa na biden kutok kwenye simu aliyopokea tareh:27 asubuhi kutoka kwa biden...na kwa kitendo icho TAYARI KIMEONYESHA DHAMIRA YA RAIS HUYO KUWA HATAKUWA TAYARI KUJIUNGA TENA NA NATO MARA BAADA YA MZOZO HUU KUISHA MAANA AMEGUNDUA NI WANAFIKI NA NDIOMAANA "ALIANZA KUHIMIZA VITA HII TUTASHINDA NA KILA RAIA WA UKRAINE WA UMRI KUANZIA MIAKA 18 HADI 60 ASHIKE SILAHA KUIPAMBANIA NCHI YAO WENYEWE"...na ukweli ndo huo marekani na washirika wake wa nato ni wanafiki maana inakuwaje mtu mnayemhimiza ajiunge nanyie nato anavamiwa hadi Mikoa yake ya mipakani LUHANSK NA DONETSK yanachukuliwa na amewaomba msaada hamkurespond na baadae ndo mnajifanya kumpigia simu na kumwambia mumsaidie financial wakati mtu anapigwa?...iyo inamsaada gani??...nandio maana rais wa ukraine akakataa hadharani kwenye akaunti yake ya insta hii ilimfanya marekani+nato waonekane hawana nia ya kuisave ukraine...haibiu hii ndo imapelekea USA kujinasibu kuwa itawasaidia ukraine ANTI-AIRCRAFT MISSILE STINGER ...huku nato walikutana kwa dharura na kukubaliana kuongeza SEVERE ECONOMIC SUNCTIONS KWA URUSI NA MAKAMPUNI YAKE....kitu ambacho hata korea kaskazin waliwekewa hivyo vikwazo miaka nenda rudi na bado wanasurvive freshy tu...sikatai itamdhohofisha putin kiuchumi lakini haitofanya lengo lake alitakalo kukamilima kiuhalisia that guy is a COWARD...yaan haogopi ivyo vikwazo na bila shaka alisha asses iyo risk kabla ya kuianza iyo vita hivyo alishacalculate wapi nato watakimbilia before.

UKITAKA KUJUA NATO+USA NI WANAFIKI RAIS WA UKRAINE ALIPOST HII.

IKIWA RAIS WA TURKEY BWANA EDORGAN ANAWEKA WAZI KUWA NATO WANAMFELISHA UKRAINE WEWE NI NANI HUMU JF kuwasifu nato na marekani kama msaada wa ukraine kwenye hii battle???

Ifahamike kuwa russia hajafanya full scale invasion kwa ukraine kama alivyofanya pale syria dhidi ya waasi wa asadi...angefanya ivyo maana ake angetumia kila silaha aliyonayo na ukraine isingekuwa salama hadi ivi sasa...maana inafahamika wazi kiuwezo wa kijeshi Ukraine bado sana kwa russia kwa msiojua labda.

Nato hawana meno direct dhidi ya mgogoro huu...ukilinganisha na madhara ambayo anayapata ukraine!...mitizamo ya watu walio wengi WALITAZAMIA KUMSAIDIA UKRAINE DIRECT KWA KUTUMA ARMED-TROOPS ZIKAMPIGE MRUSI PALE UKRAINE LAKINI CHAKUSHANGAZA KILA ANAYEJITOKEZA KUSAIDIA AKIWEMO CANADA NA UINGEREZA ANATOA MSAADA WA SILAHA KITU AMBACHO SIO GENUINELY KWENYE FIELD OF WAR MAANA WHAT IF WANAJESH WA UKRAINE HAWANA 100% YA KUTUMIA HIZO SILAHA ZA MISAADA MAANA HAWAKUWA WAKITRAIN NAZO TOKEA HAPO AWALI NA ZIMEKUJA WAKATI HUU KAMA MSAADA.

Watu waliowengi PRO USA+NATO WANATAZAMIA AIBU AMBAYO ATAIPATA RUSSIA ASIPOWIN HII VITA...WANASHINDWA KUJUA RUSSIA AMESHAPATA 80% YA MALENGO YAKE YAANI AMESHATWAA MIKOA YA LUHANSK NA DONETSK iliyokuwa inashikiliwa na waasi waliyoipinga serikali ya ukraine...kilichobaki ni ukraine kutokubali kuingia NATO tu.

Tokea jana zipo taarifa kutoka kwa rais wa ukraine kuwa kuna nazungumzo kati ya ukraine na maafisa wa urusi yatakayofanyika mpakani mwa jirani yao Belarus...ikumbukwe mkutano huu haujaitishwa na urusi...ni raisi wa belarus ndo amefanya juhudi hizi kuwakutanisha majirani zake.

Japo rais mwenyew wa ukraine anasema hana imani kama maongez hayo yatazaa matunda...beleive it makubaluano hayo yanaweza kuwa na kifungu cha kumlimit yeye ukraine kwa maandishi kwamba hatojinga nato siku za usoni wala hapo miaka ya baadae...sasa itakuwa ni juu yake kukubali au kukataa na kufanya vifo vya watu wasio na hatia viendelee kutokea nchini kwake.
umesema ww ni waziri wa wapi wa mambo ya nje?
 
Weka ushahidi wa hayo madai yako kuwa genocide haizingatii idadi kubwa ya watu kufa.
View attachment 2133985
Baada ya hilo, bado hujajibu maswali haya yalokolezwa wino:

Kwa hiyo makombora yoote yalipigwa makazi ya watu (kama unavyodai) ndio yameua raia 352 tu wanaoripotiwa na wizara ya ulinzi ya Ukraine? Basi Wanajeshi wa Russia walikuwa hawana shabaha nzuri.

Sasa hao raia 352 walokufa ndio mauaji makubwa ya genocide? Kwa hiyo ulitegemea raia wa Ukraine wapewe silaha wapambane na majeshi ya Russia halafu majeshi hayo ya Russia yawaangalie tu pasi na kuwapa kipigo cha mwizi?

Vifo vya wanajeshi wa Ukraine kwa mujibu wa serikali ya Ukraine ni kuwa havizidi 700. Ila wao wanadai wameua wanajeshi wa Russia zaidi ya 4000. Sasa kwa nini walikuwa wakiomba msaada kwa raia wa kawaida na pia raia toka nchi nyingine duniani?

Ukraine ieleze ukweli juu ya idadi ya vifo vya wanajeshi wake na raia waliopewa risasi wapambane na Russia ktk mavazi ya kiraia (ngao ya vita)

Kwako wewe neno "large" unalielewa vipi, ndani ya siku nne uue watu 352 kwa kuwapiga mabomu ndani ya makazi yao, hiyo unaona sio large?
 
Mzee issue ya Russia siyo kuteka Kiev. Ukraine na Russia ni ndugu kabisa. Lengo la Russia ni kumzuia Ukraine kujiunga NATO. Na hii imefanikiwa kwa 100%. Na tayari maafisa ya Ukraine wapo Belarus kuitikia wito wa Russia.

Usiichukulie Russia kama manzese.
Wapo kwenye Mpaka wa Ukraine na Beralue mbona mnataka kupotosha? Ukraine iligoma kwenda Belarus Kama Putin alivyopendekeza awali.

Hata hivyo nashangaa,hivi Kabla ya Vita si huyo huyo Putin aliyekataa kwamba hazungumzi na Ukraine Bali anataka kuwekeana Mikataba na USA? Na akapeleka Mapendekezo yake na Masharti Kule Marekani ambayo yote yalipigwa Chini?

Viongozi wengi walitiririka kwenda Moscow kumtaka asiivamie Ukraine Bali atumie Diplomasia lakini akaamua Kuvamia.

Leo amekubali kukutana na Ukraine,Kweli Ushujaa ni Mhimu hata Kama uko dhaifu kiasi gani.
 
Russia imesema kwa muda mrefu haitaki kuona Ukraine yatumiwa kuwa kichaka cha NATO na Marekani.

Kumbuka mafahali wawili huwezi kuwaweka zizi moja.

Russia hataki Marekani asogee karibu kupitia mgongo wa Ukraine.

Ukraine ingeruhusiwa kuingia NATO basi ingepewa Air defence systems za kuzuia mashambulizi ya Russia na Russia ingekuwa haina uwezo wa kuzishambulia nchi zote majirani na ingevamiwa.

Ndo maana Russia ikaiwahi Crimea na sasa yaitaka Ukraine.

Poland, Latvia na Romania ndio majirani pakee ambao Russia hana shida nao kwa upande wao magharibi na kusini magharibi.

Estonia ambako vipo vikosi vya majeshi ya UK na wengine nao Russia hana shida nao.

Russia haitaki kuona NATO na Marekani upande wa mashariki na kusini mashariki hadi bahari nyeusi.
 
Kwenye media hii vita urusi anachezea kichapo kweli kweli ila kwenye uwanja wa vita ukraine maji yamemfika shingoni
img_1_1646047648693.jpg
 
Ukishughulisha ubongo kidogo utaelewa, Mrusi anarusha makombora yake kwenye makazi ya watu, hayo ni mauaji ya kimbari....
Ukraine wamezindua tovuti yenye taarifa za kila mwanajeshi wa Urusi aliyeuawa, Warusi wameombwa waingie humo na kutafuta taarifa za watu wao.
Kwaio na wewe unaiamini io tovuti kwa kila kitu.? Yani mzaliwa wa chato burigi akatambuliwe jina na mkenya wa kisumu huko kiraisi raisi tu.? Maiti zinaungua moto hovyo uo utambuzi wanatumia njia gani kuwatambua.? Au ndio unaamini propaganda za kua warusi 5000+ wameuwawa na ao kiev.? Unaamini data za kiev au urusi ambae hajatangaza hata idadi ya wanajeshi walioko huko wala walio kufa.?

Punguza kua mjuaji ktk mambo ya wanaume.
 
Leo vita imesimama kupisha majadiliano ,kama majadiliano wasipopatana kesho vita itaendelea,na misaada ya kijeshi inazidi kumiminika kwa ukraine kutoka member wa nato
sijui sana mambo yavita yanaendaje ila kwanilichoexperience ndani ya siku 3 hizi urusi nikama wanaattack sana usiku kukipambazuka hawafanyi heavy millitary operation yeyote zaidi yakumove kutoka eneo moja nakusonga mbele....nadhani leo wanaweza wakashambulia zaidi usiku kama maafikiano hayatafikiwa kwasababu jana usiku pia walishambulia sana licha ya ukraine kukubali kufanya mazungumzo
 
Salaam Wakuu,

Thread hii ya Mwendelezo, itatumika kuangazia hali ya Usalama na matokeo yake katika Mzozo wa Ukraine na Urusi.
Tuzujane hapa kianachojiri..

Mvutano kati ya Ukraine na Urusi umefika kiwango cha zaidi kwa miaka mingi, lakini juhudi za kidiplomasia pia zinafanya kazi kwa bidii kutafuta suluhisho la mzozo huo. Kuna masuala mengi nyuma ya mzozo huo ambao ulianza miongo kadhaa iliyopita na kuhusisha nchi katika eneo zima. Hapa tunaangalia kile tunachojua kuhusu mgogoro huo.

Ulianzaje?
Mizizi ya hatua ya hivi punde kati ya nchi hizo mbili inaanzia Oktoba 2021. Hapo ndipo uwekaji mkubwa wa majeshi ya Urusi kwenye mpaka wa Ukraine ulipoanza. Ripoti za picha za satellite na kijasusi zimefichua kuwa zaidi ya wanajeshi 100,000 sasa wako karibu na eneo hilo. Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia imetoa picha za mazoezi ya kijeshi. Vifaa vinavyohusika ni pamoja na bunduki za kujiendesha, mizinga ya vita, magari ya mapigano.

Ukraine imeibua wasiwasi juu ya majeshi hayo ya Urusi karibu na mpaka wake ingawa serikali yake pia ilisisitiza kuwa haiamini kuwa Urusi bado iko katika nafasi ya kuchukua hatua za kijeshi.

Msimamo wa Urusi ni kwamba kutumwa kwao kijeshi sio tishio kwa Ukraine na inasema ina haki ya kufanya chochote inachotaka na jeshi lake ndani ya eneo lake. Wengine wanasema huenda likawa jeshi kubwa zaidi la Urusi lililopelekwa karibu na Ukraine tangu Vita Baridi.

"Ukraine inataka kuimarisha usalama wake kwa sababu inahisi shinikizo kubwa kutoka kwa jeshi la Urusi, kwenye mipaka na pia ndani ya eneo la Kiukreni katika sehemu zinazokaliwa za Ukraine," anasema Orysia Lutsevych, mkuu wa Jukwaa la Ukrainia Chatham House huko London. Na njia moja ambayo inatazamia kufanya hivyo ni "kupitia muungano wa pamoja na Nato," anasema Lutsevych.

Lakini Urusi inaamini kwamba uwezo wa kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wake ni haki ya uhuru. "Wako katika eneo la Urusi, hakuna anayeiambia Marekani mahali pa kuweka vikosi vyake katika eneo la Marekani," anasema Elena Ananieva, kutoka Taasisi ya Ulaya (RAS) yenye makao yake makuu mjini Moscow. "Kwa mataifa mengine inapaswa kuwa sawa"

"Kama nchi za Magharibi zinavyosema, kila nchi ina haki ya kuchagua jinsi ya kulinda usalama wake." "Lakini, tatizo kuu kwa mtazamo wa Russia ni tishio la Ukraine kujiunga na NATO na miundombinu ya kijeshi ya Nato kukaribia Urusi," anasema Ananieva.

Hii inatupeleka kwenye swali letu linalofuata.

Je, NATO itajipanua zaidi na kuijumuisha Ukraine kama mwanachama mpya?
Kando kupelekwa kwa wanajeshi katika mpaka wa nchi hizo mbili kumekuwa na kutoelewana kwa kidiplomasia kati ya Urusi na muungano wa kijeshi wa magharibi Nato.

"Upanuzi zaidi wa Nato kuelekea mashariki na kupelekwa kwa silaha, ambayo inaweza kutishia Shirikisho la Urusi, haikubaliki," kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov.

Urusi inapinga vikali uwezekano wa upanuzi wa Nato na inataka hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na Nato. Ni msimamo unaoshirikiwa na mshirika wake wa karibu China. Lakini madai haya yamekataliwa na Nato na nchi wanachama wake. Kwa sasa kuna nchi wanachama 30 katika Nato, lakini nchi nyingine zinaweza kujiunga. Ukraine si sehemu ya muungano bali ni 'nchi mshirika'.

"Jamii ya Kiukreni na vyama vya kisiasa vinaamini kwamba hakuna njia bora ya kulinda Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi kuliko kuwa sehemu ya muungano wa pamoja wa usalama," Lutsevich anasema lakini pia anaongeza kuwa uanachama wa Ukraine kwa Nato unaweza usitokee katika siku za usoni.

Huko nyuma katika miaka ya 1990, baada ya kumalizika kwa Vita Baridi na kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti, Nato ilitafuta njia za kujenga uhusiano wa karibu na mataifa mapya ya Ulaya ya Kati na Mashariki yaliyojitegemea.

Huu ndio wakati muungano huo ulipopanuka kuelekea mashariki zaidi, kumaanisha uwezo wake wa kijeshi na silaha umekaribia mpaka wa Urusi.

Kwa miongo kadhaa Kremlin imedai mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi zilivunja ahadi ya kutopanua Nato. Madai hayo yanarejelea mazungumzo ya mwaka 1990, kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James A. Baker na kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev.

Lakini viongozi wa Magharibi hawakubaliani na kusema hakukuwa na mpango wowote rasmi kuhusu kutopanua Nato hadi Ulaya Mashariki zaidi na kwamba muungano huo unashikilia 'sera ya mlango wazi.'

Ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato (kwa sasa haijatuma maombi ya uanachama), "italeta tishio zaidi kwa Urusi" kulingana na Rais Vladimir Putin.

Mnamo Novemba 2021, alisema kuwa uwepo wa Ukraine katika muungano, na uwezekano wa kutumwa kwa makombora yoyote ya masafa marefu yenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi au mifumo ya ulinzi ya makombora, sawa na ile ya Poland na Romania, itakuwa suala la "mstari mwekundu" kwa Moscow.

Lakini Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg aliweka wazi kuwa "Urusi haina kura ya turufu au kusema" kuhusu uwezekano wa upanuzi wa muungano huo.

Akizungumza na BBC, mtaalam wa Urusi Ananieva, alielezea wasiwasi juu ya uwezekano wa upanuzi wa Nato. "Miundombinu ya NATO inasonga karibu na mpaka wa Urusi. Nato inapaswa kuzingatia kanuni ya kutogawanyika kwa usalama," alisema.

"Hakuna uwezekano kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano. Nato inapaswa kufikiria mara mbili kuhusu usalama wake ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano."

Wakati juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea, utafutaji wa njia mbadala wa zabuni ya Nato ya Ukraine umeibuka.

'Finlandisation' ni nini na ina uhusiano gani na Ukraine?
Miongoni mwa viongozi wengi wa kisiasa wanaojaribu kutafuta suluhu la mzozo huo ni Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari alitaja neno la enzi ya Vita Baridi "Finlandisation" kwa waandishi wa habari wakati wa safari ya Moscow.

Iliripotiwa kwamba alipendekeza "Finlandisation ya Ukraine", kama sera iwezekanavyo ili kupunguza mvutano katika kanda.

Lakini baadaye, tarehe 8 Februari, Macron alikanusha kutoa maoni hayo yenye utata.

Neno hilo hurejelea hadhi ya Ufini kama jimbo lisiloegemea upande wowote wakati wa Vita Baridi. Nchi hiyo ilikuwa na mpaka mrefu na Muungano wa Sovieti lakini haikuegemea upande wowote.

Msimamo huu ulimaanisha kuwa Helsinki hangekuwa mwanachama wa Nato na Umoja wa Kisovieti haungeona Ufini kama tishio linalowezekana na Ufini ilitia saini mkataba mnamo 1948 na Moscow ilikubali kukaa nje ya Nato.

Hata hivyo, mkataba huo ulimalizika mwishoni mwa Vita Baridi na serikali ya Finland sasa inasema maamuzi kuhusu kujiunga na mashirika ya kimataifa kama vile Nato yanapaswa kuwa mikononi mwake pekee na si kwa nchi nyingine.

Ukraine imesema kwamba pia haitakuwa tayari kuambatana na sera ya "Finlandisation" ambayo ingezuia sera zake za kidiplomasia.

"Nadhani ni jambo lisilokubalika kabisa kwa Ukraine" Lutsevych anasema.

"Ukraine ilishambuliwa ilipokuwa nchi isiyoegemea upande wowote, na pili Putin haheshimu mamlaka ya Ukraine, iwe haina upande wowote au la.

"Ukraini inakataa wazo hili kwa sababu ni sehemu ndogo ya uwezo wa Urusi kudhibiti Ukraine."

Je, kweli Urusi inaweza kuivamia Ukraine?
Kwanza kabisa, Urusi imesema mara kwa mara haina mpango wa kufanya hivyo, lakini kwa baadhi ya taarifa hizi hazijawatia moyo. "Tayari wamevamia," anasema Lutsevych akirejelea mwaka wa 2014 wakati Urusi ilipotwaa rasi ya Crimea ya kusini mwa Ukraine, na kuwaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Urusi walioteka sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.

"Kuna zaidi ya watu 14,000 waliofariki, zaidi ya 33,000 wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Jumuiya ya Ukraine tayari inalipa gharama kubwa kwa uvamizi wa Urusi."

Nato haikuingilia moja kwa moja katika mojawapo ya matukio hayo, lakini jibu la muungano huo lilikuwa kupeleka wanajeshi wa ziada katika nchi za Ulaya Mashariki kwa mara ya kwanza, zikiwemo Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Romania.

Nato pia iliimarisha ulinzi wake wa anga/uwezo wa polisi katika mataifa ya Baltic na Ulaya Mashariki.

Moscow inataka vikosi hivi vya ziada kuondolewa katika nchi hizo.

Lakini kwa sasa, Nato inasema haina nia ya kufanya hivyo.

Nini kitatokea sasa?
Juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea ili kufikia makubaliano ya amani na kupunguza mvutano huo. Mnamo tarehe 9 Februari, katika mahojiano na BBC, Balozi wa Urusi katika Umoja wa Ulaya, Vladimir Chizhoz aliweka wazi mapendekezo ya Urusi ya kupunguza mvutano kuhusu Ukraine.

Alionyesha kuwa Moscow inaweza kujibu vyema ikiwa Ukraine ingekuwa nchi isiyoegemea upande wowote. Hata hivyo, Ukraine na Nato hapo awali walisema hawako tayari kukubaliana na hili. Katika hatua nyingine ya hivi majuzi, gazeti la Uhispania El Pais lilichapisha waraka uliovuja wa Marekani ukieleza msimamo wake wa mazungumzo.

Katika waraka huo, ilisema: "Marekani ilikuwa tayari kujadili... ahadi za kujiepusha na kupeleka mifumo ya makombora ya kurushwa ardhini na vikosi vya kudumu na misheni ya kivita katika eneo la Ukraine."

Wanadiplomasia na viongozi wa Ulaya pia wamekuwa wakichunguza njia za kufufua mpango wa kusitisha mapigano wa 2015 kwa mikoa ya Ukraine inayodhibitiwa na watu wanaotaka kujitenga. Mkataba unaoitwa Minsk kati ya Kyiv na Moscow haujawahi kutekelezwa kikamilifu.

Mtaalamu wa Ukraine Lutsevych anasema "Kyiv hatakuwa tayari kutekeleza mpango huo isipokuwa kutakuwa na upunguzaji wa kasi na usitishaji mapigano." "Urusi inataka kutumia makubaliano haya kuunda klabu yenye silaha ndani ya Ukraine ambayo ina raia wa Urusi," anaongeza.

"Suluhu la mgogoro huo ni umoja wa Magharibi na Ukraine. Kilicho hatarini ni uhuru wa Ukraine."

NATO inatishia majibu gani?
Mnamo Februari 7, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema katika mkutano na Rais wa Marekani Joe Biden kwamba Ujerumani 'imeungana' na Marekani katika kuweka vikwazo dhidi ya Urusi ikiwa itaivamia Ukraine.

Vikwazo vinavyowezekana vilivyopangwa vya Washington vitamaanisha kulenga benki kuu za Urusi na kupiga marufuku Urusi kutoka kwa mfumo wa malipo wa kimataifa wa SWIFT ambao ni muhimu kwa miamala ya kimataifa. Uingereza ilisema itawawekea vikwazo watu binafsi na biashara karibu na Kremlin.

"Urusi ilistahimili vikwazo vya Magharibi" anasema mtaalamu wa Urusi Ananieva alipoulizwa kuhusu athari zake kwa Urusi. "Imegeukia uingizwaji wa bidhaa kutoka nje. Katika baadhi ya sekta za vikwazo vya uchumi wa Urusi vimeongeza uzalishaji, na kilimo. Wakulima wangependa vikwazo vya Urusi virefushwe," anasema.

Nato haijapendekeza kuwa ingetumia nguvu za kijeshi kukabiliana na uvamizi wa Urusi. Ingawa mazungumzo ya kimataifa yanaendelea kwa sasa hakuna njia wazi ya jinsi pande hizo mbili zitakavyofikia makubaliano.

Nani mwenye uwezo iwapo vita vitatokea?
===

Chanzo cha mvutano wa kijeshi kati ya Urusi na Ukraine na uwezekano wa vita kamili

Tangu mwaka Mpya wa 2022 uanze,vyombo vingi vya kiusalama vya kimataifa vimekuwa vikiripoti juu ya tishio la nchi ya Urusi Kuvamia kijeshi nchi ndogo jirani ya Ukraine,ambayo zamani ilikuwa katika muungano wa umoja wa kisoviet (USSR),Kabla ya kusambaratika vibaya Sana kwa umoja huo mwishoni mwa miaka ya 1990.

NINI CHANZO CHA MGOGORO HASA?
Mnamo mwaka 2014, Urusi iliyafadhili kijeshi makundi ya vuguvugu Mashariki mwa Ukraine katika majimbo ya CRIMEA,DONBASS,DONETSK na LUHANSK ambayo wakazi wengi wa majimbo hayo wana asili ya Urusi na wanazungumza Kirusi kwa ufasaha.

Katika mapambano hayo,Majeshi ya waasi kwa msaada wa Urusi walifanikiwa kuyateka majimbo hayo kutoka kwenye mikono ya Serikali ya Kyiv. Jimbo la CRIMEA liliamua kuitisha kura ya maoni (Referendum) ya kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.

Majimbo mawili (Donestk na LUHANSK) yaliendeleza mapambano makali dhidi ya Majeshi ya Ukraine na kuchukua udhibiti KAMILI wa majimbo hayo. Katika Jimbo la DONBASS Majeshi ya Ukraine yalipambana Sana na hivyo waasi kushindwa kuliteka Jimbo Hilo kikamilifu.

MGOGORO KAMILI?
Tangu mwaka 2014,Ukraine ilianza kupokea msaada wa vifaa vya kijeshi kutoka kwa washirika wa NATO. Ikumbukwe kuwa,Ukraine sio mwanachama wa NATO wala Umoja wa Mataifa. Vifaa vingi vya kijeshi vilitoka nchi za Marekani,Uturuki na Uingereza. Jeshi la Ukraine liliimarika zaidi baada ya kununua DRONES za kisasa kutoka Uturuki.

DRONES hizi zinajulikana Sana hasa zilipofanya vizuri kwenye mgogoro wa kijeshi Kati ya Armenia na Azerbaijan. Mwishoni mwa mwaka 2021 mwezi Desemba, Majeshi ya Ukraine yalianza kuyateka upya maeneo ya DONBASS kwa kutumia mashambulizi ya Anga kutoka kwenye DRONES. Majeshi ya Ardhini ya Ukraine yakashinda Nguvu Majeshi ya waasi na kuliteka Jimbo lote la DONBASS. Baada ya ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine katika Jimbo la DONBASS,ndipo Ukraine ikaanza mashambulizi ya Anga kwenye Jimbo la LUHANSK.

Baada ya Ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine,ndipo Majeshi ya Ukraine yakaingia Frontline ili kuwasaidia waasi. Pia,kikundi Cha Majeshi ya kukodiwa kutoka Urusi maarufu Kama WAGNERS kiliamua kuanzisha mashambulizi dhidi ya Majeshi ya Ukraine. Hata hivyo,Majeshi ya Urusi,Waasi na WAGNERS kwa pamoja yalishindwa kudhibiti mashambulizi ya DRONES za Ukraine.

Tarehe 24 Desemba 2021, Majeshi ya Urusi yalianza kuingiza mifumo ya Ulinzi wa Anga-ANT AIRCRAFT MISSILES (S-300 na S-400). Ujio wa Mifumo hiyo ya Ulinzi wa Anga ulisababisha DRONES za Ukraine kushindwa kufanya mashambulizi ya Anga. Hali hiyo ilitoa upenyo wa Majeshi ya Urusi na waasi kuchukua udhibiti upya wa majimbo ya DONBASS na LUHANSK.

JE, ENDAPO URUSI IKIAMUA KUVAMIA NANI ATAIBUKA KIDEDEA?
Kutokana na Uwezo mkubwa wa kijeshi wa Urusi ukilinganisha na Ukraine,bila Shaka Urusi itaibuka kidedea na kuyateka maeneo mengi ya Ukraine Kama itataka hivyo. Ushindi huo wa Urusi hautakuja kwa urahisi,Urusi inaweza kushuhudia kulipuliwa kwa vifaru vyake vingi ambavyo vitaingia kwenye ardhi ya Ukraine kuliko vifaru 140 ambavyo Urusi alivipoteza wakati wa Uvamizi wa nchi ya GEORGIA. Hii ni kutokana na Ukraine kupokea msaada wa Siraha za kulipua vifaru (ANT-TANK MISSILES) Zaidi ya Tani 80 kutoka Uingereza. Mwaka 2014 Ukraine haikuwa na Siraha hizi.

JE,URUSI INAWEZAJE KUZUIA KUPOTEZA VIFARU VYAKE VINGI?
Kutokana na Ukraine kutokuwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga (ANT-AIRCRAFT MISSILES) ya Uhakika, Basi Urusi ana nafasi ya kutumia ndege za kivita kushambulia Mifumo yote ya Ukraine ya kulipulia Vifaru Kabla ya vifaru hivyo kuanza kuingia kwenye Ardhi ya Ukraine kwa Urahisi zaidi.

Kutokana na Ukraine kulijua hili,imeamua kupeleka Mifumo yake ya kulipulia Vifaru karibu na mpaka wa Poland upande wa Magharibi. Makombora haya yanaweza kushambulia vifaru vyote vya Urusi ambavyo vitaingia Ukraine upande wa kaskazini wa Ukraine kutokea Belarus. Je,Urusi ataweza kushambulia kwa ndege za kivita Mifumo hii ya Ukraine ya kulipulia Vifaru ambavyo viko kwenye mpaka wa Poland? Jibu ni Hapana.

Kwasababu Marekani imeonya kwamba, endapo ndege za kivita za Urusi zitakaribia kwenye mipaka ya NATO(Poland ni Mwanachama wa NATO) Basi Marekani hatasita kuzitungua ndege Hizo. Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2017, ndege ya Kivita Ya Urusi iliyokuwa inafanya mission ya kuwashambulia waasi wa ISLAMIC STATE ilitunguliwa na Mifumo ya Anga ya Uturuki ilipokaribia Anga la Uturuki kwenye Mpaka wa Uturuki na Syria. Hili tukio liliharibu uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Uturuki na Urusi.

PIA SOMA
1. Mzozo wa Urusi na Ukraine wafukuta zaidi
2. Historia Iliyojificha Kuhusu Ukraine na Urusi
===
UPDATES

YALIYOJIRI FEBRUARI 21
Marekani yadai ina orodha ya wanaopaswa kuuawa na Urusi itakapoivamia Ukraine
Taarifa za kuaminika za Marekani zimesema Urusi inaandaa orodha ya watu watakaowaua au kupelekwa Kambini baada ya kuvamia Ukraine kutokana na mzozo unaoendelea.

Barua iliyotumwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) imeonesha miongoni mwa wanaolengwa ni wapinzani wa Kisiasa, watu wa Dini na makabila ya wachache. Moscow imekanusha kuwa na mpango wa kushambulia Ukraine, lakini inatafuta hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na NATO.

YALIYOJIRI FEBRUARI 23
Urusi kukabiliwa na vikwazo kutokana na mzozo na Ukraine
Urusi iko hatarini kukabiliwa na vikwazo kutoka Nchi za Magharibi kufuatia mgogoro unaoendelea kufukuta kati yake na Ukraine

Wakuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula Von der Leyen na Charles Michel wamesema Umoja huo unatafakari kuwekea vikwazo Benki za Urusi zilizo na Matawi katika Majimbo yanayodhibitiwa na waasi wa Ukraine ya Luhansk na Donetsk. Hata hivyo, vikwazo hivyo vitahitaji ridhaa ya Nchi Wanachama zote 27

Bunge la Urusi limepitisha agizo la Rais Vladimir Putin kutambua Uhuru wa maeneo ya waasi Mashariki mwa #Ukraine, siku moja baada ya Rais Putin kulisaini na kuamuru Wanajeshi kuingia maeneo hayo

YALIYOJIRI FEBRUARY 24
Ukraine yatangaza hali ya hatari
Bunge la Ukraine limepitisha azimio la nchi hiyo kuwa katika hali ya hatari kwa siku 30 kutokana na mzozo uliopo kati ya Nchi hiyo na Urusi.

Mamlaka nchini humo zimeruhusiwa kuzuia raia kutoka, kuzurura na kuzuia Mikutano ya Vyama vya Siasa na Taasisi kwa maslahi ya Taifa. Pia, Serikali imewalazimisha kujiunga na jeshi wanaume wote waliofikia umri wa kwenda vitani.

UN yaitaka urusi kuondoa wanajeshi Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amemtaka Rais wa Urusi, Vladimir Putin kurudisha Wanajeshi aliowapeleka Ukraine, akisema watu wengi wameshapoteza maisha na ni wakati wa kuipa nafasi Amani

Aidha, Rais Joe Biden amesema Urusi itabeba lawama kwa madhara yatakayotokea katika mzozo unaoendelea, akisisitiza Marekani pamoja na Washirika wake watajua cha kufanya

Papa Francis atangaza machi 2 kuwa siku ya kufunga na kuiombea Ukraine
Kufuatia kile kinachoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema hatari ya vita ilmesababisha maumivu makali moyoni mwake

Ametoa wito kwa watu wote kutumia siku ya Machi 2, 2022 ambayo ni Jumatano ya Majivu, kufunga na kuiombea Ukraine

Ripoti zinaonesha tayari Russia imeanza kuishambulia Ukraine. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema watashinda vita hivyo.

Putin: Atakayeingilia mzozo wa ukraine atapata pigo la kihistoria
Baada ya kutangaza mashambulizi dhidi ya Ukraine, Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametoa onyo kwa Mataifa ya Magharibi kuingilia kinachoendelea baina ya Nchi hizo

Mara baada ya milipuko kuripotiwa katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv Putin alinukuliwa akisema, "Kwa yeyote atakayeingilia kutoka nje, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo katika historia"

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha Kikao cha Dharura mara baada ya Urusi kuanza mashambulizi

Watu 10 na wanajeshi 40 wafariki katika shambulio lililofanywa na Urusi
akriban Raia 10 na Wanajeshi 40 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Anga yaliyofanywa na Urusi leo Februari 24, 2022 katika Mji wa Odessa

Taarifa ya Vifo hivyo imetolewa na Msaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alipozungumza na Waandishi.

Ukraine: Rais kumpatia silaha kila raia anayetaka kuipiga Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewahamasisha Raia kuwa tayari kupigania Nchi yao, na kusema silaha zitatolewa mtu yeyote anayetaka kushiriki katika vita dhidi ya Urusi.

Kufuatia uamuzi wa Urusi kuvamia Ardhi yake, Ukraine imekatiza rasmi uhusiano wake wa Kidiplomasia na Taifa hilo. Picha kadhaa za Mitandaoni hivi karibuni zilionesha Raia wa Ukraine wakipewa Mafunzo ya Msingi ya Kijeshi taharuki ya mzozo huo ilipopanda.

Schalke o4 kuondoa nembo ya kampuni ya Urusi kwenye jezi
Klabu ya Schalke O4 imethibitisha kuwa itaondoa mara moja kwenye jezi zake nembo ya Kampuni ya Gazprom inayomilikiwa na Serikali ya Urusi

Kampuni hiyo inayofanya biashara ya mafuta na gesi ndio mdhamini mkuu wa klabu hiyo. Sehemu ilipokuwa inakaa nembo hiyo yatawekwa maneno yatakayosomeka ‘Schalke 04’. Hatua hii inakuja baada ya Urusi kuivamia na kuishambulia Ukraine kivita

UK: Mbunge ataka Abramovich azuiwe kumiliki Chelsea
Chris Bryant amehoji iwapo Roman Abramovich ataendelea kuwa mmiliki wa Klabu ya Chelsea huku akitaka kuzuiwa kwa mali zake kama sehemu ya vikwazo dhidi ya Urusi

Ameeleza kuwa Abramovich amewahi kukubali Mahakamani kuwa alihusika kulipa fedha kwa ajili ya ushawishi wa Kisiasa na kuwa ana uhusiano na Serikali ya Urusi

Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa Abramovich amezuiliwa kuishi Uingereza na maafisa wa uhamiaji wamepewa maelekezo ya kuhakikisha Abramovich hakai Uingereza

Hatua hii inakuja baada ya Urusi kuivamia na kuishambulia Ukraine kivita huku nchi kadhaa ikiwemo England zikiangalia namna ya kuiwekea vikwazo Urusi

YANAYOJIRI FEBRUARI 25

Mashirika ya ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua Urusi
Mashirika ya Ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua katika Viwanja vya Ndege vya Urusi pamoja na kupita kwenye Anga lake

Uamuzi huo unafuatia uamuzi wa Uingereza kupiga marufuku Shirika la Ndege la Urusi, Aeroflot kutua Nchini Uingereza. Marufuku ya Uingereza ni sehemu ya vikwazo vilivyowekwa ili kukabiliana na Uvamizi wa Nchini Ukraine.

UEFA: Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya haitafanyika Urusi
Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) limehamisha fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka Urusi kwenda Paris, Ufaransa baada ya Urusi kuishambulia Ukraine.

Fainali hiyo itakayofanyika Mei 28, 2022 itafanyika katika Uwanja wa Stade de France wa Ufaransa badala ya ule ulioko Urusi wa Gazprom Arena jijini Saint Petersburg.

Mara ya mwisho Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuchezwa katika Dimba la Stade de France ilikuwa miaka 16 iliyopita wakati Barcelona ilipoifunga Arsenal.

Serikali: Watanzania walio Ukraine wawe watulivu
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imewataka Watanzania walioko Ukraine ikiwemo Wanafunzi, Wafanyakazi na Wafanyabiashara kuwa watulivu kipindi hiki cha mzozo wake na Urusi na kushauriwa kufuata maelekezo yanayotolewa

Wanafunzi wametakiwa kufuata maelekezo ya uongozi wa Vyuo, na kuendelea kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania Nchini Sweden kwa kuwa ndio unawakilisha Ukraine. Serikali inaendelea kufuatilia hali za Watanzania walio huko, ikielezwa hadi sasa hakuna aliyepata madhara yoyote.

Ukraine yaomba msaada wa majeshi yenye nguvu
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ameomba Washirika wa Nchi za Magharibi waisaidie Nchi hiyo kukomesha mashambulizi ya Urusi

Amelalamika Mataifa yenye nguvu kuiacha Ukraine ijipambanie huku wakitizama kwa mbali. Amesema hata vikwazo vilivyowekwa havijamshawishi Rais Vladimir Putin kuacha kufanya mashambulizi

YALIYOJIRI FEBRUARI 26
UKraine yataka mazungumzo na Urusi
Rais Volodymyr Zelensky ametoa wito wa mazungumzo kati yake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ili kunusuru Raia wasio na hatia.

Viongozi wa China wamesema Urusi ipo tayari kwa mazungumzo. Walitoa kauli hiyo baada ya Rais Putin kuzungumza kwa njia ya simu na Rais Xi Jinping. Rais Putin ameonesha utayari wa kutuma wawakilishi kwa ajili ya mazungumzo.

Ukraine: Mbunge asema wanawake watapigana kama wanaume
Kira Rudik amechapisha picha akiwa ameshika bunduki na kuandika anajifunza kuitumia ili kutetea ardhi yake dhidi ya Urusi. Mbunge huyo amesema Wanawake watatetea ardhi ya Nchi yao kama Wanaume.

Rais wa Ukraine avaa gwanda na kuingia uwanja wa vita
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amevaa Gwanda za Jeshi na kuingia "Uwanja wa Vita" kutetea nchi yake. Majeshi ya Urusi yameripotiwa kuzidi kuingia katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv. Awali, kulikuwa na tetesi kuwa Rais huyo amekimbia nchi, ambapo alijitokeza na kuomba Wananchi wapuuzie taarifa hizo.

Poland waungana na Sweden kukataa kucheza na urusi mechi ya kufuzu kombe la dunia
Poland imesema itakataa kucheza mchezo wao wa Machi 25, 2022 dhidi ya Urusi baada ya Nchi hiyo kuivamia Ukraine

Chama cha Soka cha Poland pia kimetoa msaada wa kuwa mwenyeji wa michezo yote ambayo Ukraine ilitakiwa kuwa mwenyeji ila itashindwa kutokana na vita.

Ukraine itakutana na Scotland katika mchezo wake wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia, kabla ya kukutana na mshindi kati ya Wales au Austria.

Ukraine: Mashambulizi yapelekea maelfu kukimbilia nchi jirani
Zaidi ya Raia 150,000 wa Ukraine wamevuka Mipaka kuingia Mataifa jirani katika upande wa Magharibi kutafuta usalama, wakati Urusi ikishambulia Mji Mkuu wa Nchi hiyo pamoja na Miji mingine kwa mashambulizi ya angani.

Idadi kubwa ya waliowasili katika mataifa jirani ni Wanawake, Watoto na Wazee baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kuwapiga marufuku Wanaume wenye umri wa kujiunga na Jeshi kuondoka.

Yaliyojiri February, 27
Ukraine: Wafungwa wenye uzoefu wa kijeshi kuachwa huru
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Ukraine ametangaza kuwaachia wafungwa wote wenye uzoefu wa kijeshi ili wasaidie kuipigania Nchi yao.

Baadhi ya wafungwa wameshaanza kuachiwa ili kuweza kupambana na majeshi ya Urusi ambayo yameendeleza mashambulizi dhidi ya Taifa hilo. Wanawake wamesema hawataweza kwenda vitani lakini watapambana kwa kuchangia damu ili kuwanusuru majeruhi wa vita.

Ukraine yakubali kukutana na Urusi kwa mazungumzo
Ukraine imeonesha utayari wa kufanya mazungumzo na Urusi mpakani mwa nchi hizo mbili ili kupunguza athari kwa raia wasio na hatia

Hatua imekuja baada ya Urusi kuonesha kuwa angeweza kutumia Bomu la Nyuklia kuipiga Ukraine. Aidha, ripoti zimesema Japan inaweza kuweka vikwazo vya kifedha kwa Urusi kama itaendelea na mashambulizi yake.

Umoja wa Ulaya (EU) wapiga marufuku ndege za Urusi
Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza marufuku dhidi ya Ndege za Urusi, ikisema inafunga Anga lake kwa Ndege zinazomilikiwa na zilizosajiliwa na Urusi. Inamaanisha Ndege hazitoweza kutua, kuruka au kupita juu ya anga la Nchi yoyote ya EU

Umoja huo pia umesema utapiga marufuku Vyombo vya Habari vya Sputnik na Russia Today vinavyomilikiwa na Serikali ya Urusi. Pia, umeweka vikwazo dhidi ya Rais Vladimir Putin na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Lavrov.

Yaliyojiri February 28, 2022
(UNHCR) limesema idadi ya wanaokimbia Vita Nchini Ukraine imefikia Watu 368,000
UKRAINE: Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema idadi ya wanaokimbia Vita Nchini #Ukraine imefikia Watu 368,000

Kamishna Mkuu wa Shirika hilo amesema idadi imekuwa ikibadilika kila wakati ambapo makadirio ya Jumamosi pekee zaidi ya Watu 150,000 wamekimbilia Poland, na Mataifa mengine ikiwemo Hungary na Romania

Poland imesema zaidi ya Wakimbizi 156,000 wameingia katika mipaka ya Taifa hilo.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiamuru Urusi kucheza Mechi bila Bendera na Wimbo wa Taifa
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiamuru Urusi kucheza Mechi bila Bendera na Wimbo wa Taifa katika viwanja visivyoegemea upande wowote, ikionya huenda Nchi hiyo ikaondolewa kwenye mashindano ikiwa hali ya Ukraine haitaimarika.

FIFA imesema Timu ya Taifa haitashiriki kama Urusi, bali kama Shirikisho la Soka la Urusi (RFU) na Michezo yote ya nyumbani itafanyika bila mashabiki kwenye eneo lisiloegemea upande wowote.

Aidha, Shirikisho hilo limelaani mabavu yaliyotumika kuivamia Ukraine na kusema hakuna Mechi ya Kimataifa itachezwa Nchini Urusi
Watu mnaishabikia sana Russia na kusahau kuwa hiyo Russia inasapotiwa ki maneno na Ukraine inasapotiwa kivitendo.
Msitegemee kuona washirika wake wakijiingiza ktk hiyo Vita ya kipuuzi.
Rejeleeni mgogoro wa Russia na Georgia ulianza km huu wa Ukraine mara Russia akapoteza kwa Georgia na hamtoamini hi itajirudia Tena.
Ht uwe na nguvu vipi ukipingwa na mataifa ya Ulaya pamoja na America ushapoteza.
 
Nimejaribu kuwafuatlia kwa muda humu nimeon wazi watu weng wanaongozwa na mapenzi binafsi juu ya upande fulan hasa hawa wanaojionyesha NI PRO USA+NATO...unakuta mtu anakwambia eti siku ya tano leo mbona urusi hajaiteka kiyv(ambayo ndio mji mkuu wa ukraine)....HEBU WATOE HISTORY NI LINI NA WAPI MAREKANI WANAOMPIGIA CHAPUO HAPA AMEWAI SHINDA VITA KWA SIKU TANO???..wote tunafahamu humu mwaka 1950 mmarekani alishindwa vita dhidi ya taifa dhaifu kabisa la vietnam vita ile alopigana zaid ya miaka 4 na hakutoboa...unakuta mtu anakwambia mbona huyo putin kashindwa kuifanya ukrain majivu...ukweli ni kwamba URUSI HATAKI UKRAINE KUJIUNGA NA NATO NANDICHO ANAPINGA UTANUZI WA UMOJA WA NATO KUINGIZA WANACHAMA WAPYA KINYUME NA MAKUBALIANO AMBAYO AFISA WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE YA RUSSIA ALIINGIA NA NATO 1992...YOTE HII MRUSI AKIWA ANA WASIWASI KUWA WANAWEZA MFANYIA MASTERPLAN WAKAIGAWA ZAIDI RUSSIA KAMA ILIVYOTOKEA KWA USSR HUKO AWALI. na kiuhalisia mji wa kyiv hauna waasi huo mji upo mikononi mwa serikali kwa miaka mingi...mikoa ya ukraine ambayo ilikuwa inawaasi wanaopingana na serikali ya ukraine ni miwili tu LUHANSK NA DONETSK ambayo russia alishasign hati ya kuitambua kama nchi huru na ndio mikoa ya kwanza kuitwaa kabla ya kuingia hapo kyiv tokea usiku wa tarehe: 26 kuamkia tarehe:27...na lengo la urusi si kutake over all the ukraine country ni kumega mikoa hiyo iliyokuwa inakaliwa na waasi na pia kumdhoofisha ukraine ili aachane na mikakati ya kujinga na nato...na mpaka sasa mikoa hiyo ya luhansk na donetsk imeshachukuliwa kutoka mikononi mwa ukraine na

Hadi ile tareh: 25 mwezi huu rais wa ukraine aliomba msaada kutoka kwa wajumbe 27 wa nato na wote hawakuwa na dhamira ya msaada na kutoa jibu la moja kwa moja wataisaidia vipi ukraine na kitu icho ndo kimefanya rais wa ukraine kukataa msaada aliotak kupewa na biden kutoka kwenye simu aliyopokea tareh:27 asubuhi kutoka kwa biden...na kwa kitendo icho TAYARI KIMEONYESHA DHAMIRA YA RAIS HUYO KUWA HATAKUWA TAYARI KUJIUNGA TENA NA NATO MARA BAADA YA MZOZO HUU KUISHA MAANA AMEGUNDUA NI WANAFIKI NA NDIOMAANA "ALIANZA KUHIMIZA VITA HII TUTASHINDA NA KILA RAIA WA UKRAINE WA UMRI KUANZIA MIAKA 18 HADI 60 ASHIKE SILAHA KUIPAMBANIA NCHI YAO WENYEWE"...na ukweli ndo huo marekani na washirika wake wa nato ni wanafiki maana inakuwaje mtu mnayemhimiza ajiunge nanyie nato anavamiwa hadi Mikoa yake ya mipakani LUHANSK NA DONETSK inachukuliwa na amewaomba msaada hamkurespond na baadae ndo mnajifanya kumpigia simu na kumwambia mumsaidie financial wakati mtu anapigwa?...iyo itamsadia nin??...nandio maana rais wa ukraine akakataa hadharani kwenye akaunti yake ya insta hii ilimfanya marekani+nato waonekane hawana nia ya kuisave ukraine...na hatua hii ndo imepelekea USA kujinasibu kuwa itawasaidia ukraine ANTI-AIRCRAFT MISSILE STINGER ...huku nato walikutana kwa dharura na kukubaliana kuongeza SEVERE ECONOMIC SUNCTIONS KWA URUSI NA MAKAMPUNI YAKE....kitu ambacho hata korea kaskazin waliwekewa hivyo vikwazo miaka nenda rudi na bado wanasurvive freshy tu...sikatai itamdhohofisha putin kiuchumi lakini haitofanya lengo lake alitakalo kukamilima kiuhalisia that guy is a COWARD...yaan haogopi ivyo vikwazo na bila shaka alisha asses iyo risk kabla ya kuianza iyo vita hivyo alishacalculate wapi nato watakimbilia before.

UKITAKA KUJUA NATO+USA NI WANAFIKI RAIS WA UKRAINE ALIPOST HII.

IKIWA RAIS WA TURKEY BWANA EDORGAN ANAWEKA WAZI KUWA NATO WANAMFELISHA UKRAINE WEWE NI NANI HUMU JF kuwasifu nato na marekani kama msaada wa ukraine kwenye hii battle???

Ifahamike kuwa russia hajafanya full scale invasion kwa ukraine kama alivyofanya pale syria dhidi ya waasi wa asadi...angefanya ivyo maana ake angetumia kila silaha aliyonayo na ukraine isingekuwa salama hadi ivi sasa...maana inafahamika wazi kiuwezo wa kijeshi Ukraine bado sana kwa russia kwa msiojua labda.

Nato hawana meno direct dhidi ya mgogoro huu...ukilinganisha na madhara ambayo anayapata ukraine!...mitizamo ya watu walio wengi WALITAZAMIA KUMSAIDIA UKRAINE DIRECT KWA KUTUMA ARMED-TROOPS ZIKAMPIGE MRUSI PALE UKRAINE LAKINI CHAKUSHANGAZA KILA ANAYEJITOKEZA KUSAIDIA AKIWEMO CANADA NA UINGEREZA ANATOA MSAADA WA SILAHA KITU AMBACHO SIO GENUINELY KWENYE FIELD OF WAR MAANA WHAT IF WANAJESH WA UKRAINE HAWANA 100% EFFICIENCY YA KUTUMIA HIZO SILAHA ZA MISAADA MAANA HAWAKUWA WAKITRAIN NAZO TOKEA HAPO AWALI NA ZIMEKUJA WAKATI HUU KAMA MSAADA.

Watu waliowengi PRO USA+NATO WANATAZAMIA AIBU AMBAYO ATAIPATA RUSSIA ASIPOWIN HII VITA...WANASHINDWA KUJUA RUSSIA AMESHAPATA 80% YA MALENGO YAKE YAANI AMESHATWAA MIKOA YA LUHANSK NA DONETSK iliyokuwa inashikiliwa na waasi waliyoipinga serikali ya ukraine kama alivyofanya hivyo huko nyuma kwenye rasi ya Crimea iliyokuwa sehemu ya ukraine 2014 na hivisasa ni urusi...kilichobaki ni ukraine kutokubali kuingia NATO tu.

Tokea jana zipo taarifa kutoka kwa rais wa ukraine kuwa kuna nazungumzo kati ya ukraine na maafisa wa urusi yatakayofanyika mpakani mwa jirani yao Belarus...ikumbukwe mkutano huu haujaitishwa na urusi...ni raisi wa belarus ndo amefanya juhudi hizi kuwakutanisha majirani zake.

Japo rais mwenyew wa ukraine anasema hana imani kama maongez hayo yatazaa matunda...beleive it makubaluano hayo yanaweza kuwa na kifungu cha kumlimit yeye ukraine kwa maandishi kwamba hatojinga nato siku za usoni wala hapo miaka ya baadae...sasa itakuwa ni juu yake kukubali au kukataa na kufanya vifo vya watu wasio na hatia viendelee kutokea nchini kwake.

umeandika 🚮🚮🚮🚮 kanywe maji ulale
 
Kwenye media hii vita urusi anachezea kichapo kweli kweli ila kwenye uwanja wa vita ukraine maji yamemfika shingoni
View attachment 2134045
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hii vita mitandaoni URUSI askari wanauawa kama M23. Ila sasa wenyewe UKRAINE muda wote wanaomba msaada wa vifaa, askari na hata kugawa silaha kwa Raia wao, wafungwa nk. URUSI wameteka miji kibao ya UKRAINE lkn huku ndani wanasema wamepigwa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nimejaribu kuwafuatilia kwa muda humu nimeona wazi watu wengi wanaongozwa na mapenzi binafsi juu ya upande fulan hasa hawa wanaojionyesha NI PRO USA+NATO...unakuta mtu anakwambia eti siku ya tano leo mbona urusi hajaiteka kiyv(ambayo ndio mji mkuu wa ukraine)....HEBU WATOE HISTORY NI LINI NA WAPI MAREKANI WANAOMPIGIA CHAPUO HAPA AMEWAI SHINDA VITA KWA SIKU TANO???..wote tunafahamu humu mwaka 1950 mmarekani alishindwa vita dhidi ya taifa dhaifu kabisa la vietnam vita ile aliyopigana zaid ya miaka 4 na hakutoboa...unakuta mtu anakwambia mbona huyo putin kashindwa kuifanya ukrain majivu...ukweli ni kwamba URUSI HATAKI UKRAINE KUJIUNGA NA NATO NANDICHO ANAPINGA UTANUZI WA UMOJA WA NATO KUINGIZA WANACHAMA WAPYA KINYUME NA MAKUBALIANO AMBAYO AFISA WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE YA RUSSIA ALIINGIA NA NATO 1992...YOTE HII MRUSI AKIWA ANA WASIWASI KUWA WANAWEZA MFANYIA MASTERPLAN WAKAIGAWA ZAIDI RUSSIA KAMA ILIVYOTOKEA KWA USSR HUKO AWALI. na kiuhalisia mji wa kyiv hauna waasi huo mji upo mikononi mwa serikali kwa miaka mingi...mikoa ya ukraine ambayo ilikuwa inawaasi wanaopingana na serikali ya ukraine ni miwili tu LUHANSK NA DONETSK ambayo russia alishasign hati ya kuitambua kama nchi huru na ndio mikoa ya kwanza kuitwaa kabla ya kuingia hapo kyiv tokea usiku wa tarehe: 26 kuamkia tarehe:27...na lengo la urusi si kutake over all the ukraine country ni kumega mikoa hiyo iliyokuwa inakaliwa na waasi na pia kumdhoofisha ukraine ili aachane na mikakati ya kujinga na nato...na mpaka sasa mikoa hiyo ya luhansk na donetsk imeshachukuliwa kutoka mikononi mwa ukraine na

Hadi ile tareh:25 mwezi huu rais wa ukraine aliomba msaada kutoka kwa wajumbe 27 wa nato na wote hawakuwa na dhamira ya msaada na kutoa jibu la moja kwa moja wataisaidia vipi ukraine na kitu icho ndo kimefanya rais wa ukraine kukataa msaada aliotak kupewa na biden kutoka kwenye simu aliyopokea tareh:27 asubuhi kutoka kwa biden...na kwa kitendo icho TAYARI KIMEONYESHA DHAMIRA YA RAIS HUYO KUWA HATAKUWA TAYARI KUJIUNGA TENA NA NATO MARA BAADA YA MZOZO HUU KUISHA MAANA AMEGUNDUA NI WANAFIKI NA NDIOMAANA "ALIANZA KUHIMIZA VITA HII TUTASHINDA NA KILA RAIA WA KIUME UKRAINE WA UMRI KUANZIA MIAKA 18 HADI 60 ASHIKE SILAHA KUIPAMBANIA NCHI YAO WENYEWE"...na ukweli ndo huo marekani na washirika wake wa nato ni wanafiki maana inakuwaje mtu mnayemhimiza ajiunge nanyie nato anavamiwa hadi Mikoa yake ya mipakani LUHANSK NA DONETSK inachukuliwa na amewaomba msaada hamkurespond na baadae ndo mnajifanya kumpigia simu na kumwambia mumsaidie financial wakati mtu anapigwa?...iyo itamsadia nin??...nandio maana rais wa ukraine akakataa hadharani kwenye akaunti yake ya insta hii ilimfanya marekani+nato waonekane hawana nia ya kuisave ukraine...na hatua hii ndo imepelekea USA kujinasibu kuwa itawasaidia ukraine ANTI-AIRCRAFT MISSILE STINGER ...huku nato walikutana kwa dharura na kukubaliana kuongeza SEVERE ECONOMIC SUNCTIONS KWA URUSI NA MAKAMPUNI YAKE....kitu ambacho hata korea kaskazin waliwekewa hivyo vikwazo miaka nenda rudi na bado wanasurvive freshy tu...sikatai itamdhohofisha putin kiuchumi lakini haitofanya lengo lake alitakalo kukamilika kiuhalisia that guy is a COWARD...yaan haogopi ivyo vikwazo na bila shaka alisha asses iyo risk kabla ya kuianza iyo vita hivyo alishacalculate wapi nato watakimbilia before.

UKITAKA KUJUA NATO+USA NI WANAFIKI RAIS WA UKRAINE ALIPOST HII.

IKIWA RAIS WA TURKEY BWANA EDORGAN ANAWEKA WAZI KUWA NATO WANAMFELISHA UKRAINE WEWE NI NANI HUMU JF kuwasifu nato na marekani kama msaada wa ukraine kwenye hii battle???

Ifahamike kuwa russia hajafanya full scale invasion kwa ukraine kama alivyofanya pale syria dhidi ya waasi wa asadi...angefanya ivyo maana ake angetumia kila silaha aliyonayo na ukraine isingekuwa salama hadi ivi sasa...maana inafahamika wazi kiuwezo wa kijeshi Ukraine bado sana kwa russia kwa msiojua labda.

Nato hawana meno direct dhidi ya mgogoro huu...ukilinganisha na madhara ambayo anayapata ukraine!...mitizamo ya watu walio wengi WALITAZAMIA KUMSAIDIA UKRAINE DIRECT KWA KUTUMA ARMED-TROOPS ZIKAMPIGE MRUSI PALE UKRAINE LAKINI CHAKUSHANGAZA KILA ANAYEJITOKEZA KUSAIDIA AKIWEMO CANADA NA UINGEREZA ANATOA MSAADA WA SILAHA KITU AMBACHO SIO GENUINELY KWENYE FIELD OF WAR MAANA WHAT IF WANAJESH WA UKRAINE HAWANA 100% EFFICIENCY YA KUTUMIA HIZO SILAHA ZA MISAADA MAANA HAWAKUWA WAKITRAIN NAZO TOKEA HAPO AWALI NA ZIMEKUJA WAKATI HUU KAMA MSAADA.

Watu waliowengi PRO USA+NATO WANATAZAMIA AIBU AMBAYO ATAIPATA RUSSIA ASIPOWIN HII VITA...WANASHINDWA KUJUA RUSSIA AMESHAPATA 80% YA MALENGO YAKE YAANI AMESHATWAA MIKOA YA LUHANSK NA DONETSK iliyokuwa inashikiliwa na waasi waliyoipinga serikali ya ukraine kama alivyofanya hivyo huko nyuma kwenye rasi ya Crimea iliyokuwa sehemu ya ukraine 2014 na hivisasa ni urusi...kilichobaki ni ukraine kutokubali kuingia NATO tu.

Tokea jana zipo taarifa kutoka kwa rais wa ukraine kuwa kuna nazungumzo kati ya ukraine na maafisa wa urusi yatakayofanyika mpakani mwa jirani yao Belarus...ikumbukwe mkutano huu haujaitishwa na urusi...ni raisi wa belarus ndo amefanya juhudi hizi kuwakutanisha majirani zake.

Japo rais mwenyew wa ukraine anasema hana imani kama maongez hayo yatazaa matunda...beleive it makubaluano hayo yanaweza kuwa na kifungu cha kumlimit yeye ukraine kwa maandishi kwamba hatojinga nato siku za usoni wala hapo miaka ya baadae...sasa itakuwa ni juu yake kukubali au kukataa na kufanya vifo vya watu wasio na hatia viendelee kutokea nchini kwake.

Anachotaka kufanya urusi Kwa akili yako ni sahihi ??? Huwezi kumchagulia ex wako Bwana wa kuishi naye 😊
 
Back
Top Bottom