Kusema tuangalie vita kama muvi ni kwamba tusijihusishe sana mpk inafikia hatua watu wanakua na uhasama humu kisa vita visivyotuhusu unakuta watu wanazinguana wanapeana maneno makali wengine wanatukanana n.k
Sio vita vya Russia na Ukraine vifanye leo nikiona comment ya
Joannah au
T14 Armata kwenye uzi mwingine niwe bado nina ukakasi moyoni kwamba alishawahi kunitusi kwenye uzi wa vita vya Russia na Ukraine [emoji3][emoji3][emoji3] sisi tutoe tu maoni yetu tu turelax huo mtanange ni wao.
Amini kwamba wengine humu wanachangia kwa jokes wala hawako serious so tusichukulie too personal.
Tunajua kuna madhara ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja kutokana na vita kila mtu mwenye uelewa hilo lazma alione ila ni kwamba baadhi ya watu wana upande wanaotaka ushinde vita hii kwa sababu zake binafsi iwe mapenzi juu ya nchi flan/chuki juu ya nchi flan n.k. na wengine hawataki kusikia upande upi ushinde vita wao wanachotaka vita iishe waendelee na biashara zao mfano wapo wafanya biashara hapa tz wameathirika sana na vita hiyo walikua wanapeleka mboga mboga Ukraine so watu wana mitazamo tofauti.
View attachment 2139444