LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mrusi kaamua kuutokomeza ubabe wa Kimagharibi. Alichofanya Putin binafsi naona yupo sawa, kwani Magaharibi, hususan USA, wanajifanya wao ndio polisi na wababe wa dunia na wanachotaka wao lazima kiwe. Imefikia mahala, wanakuwa kama wapo Hollywood wanacheza filamu, wanawaonea mataifa madogo, lakini hata hayo mataifa mengine madogo yanawahenyesha sana lakini hawajifunzi wakatia adabu.

USA hawana ujanja wala ari ya kupigana wao wenyewe, wanawasukumizia wengine mizozo yao. Sasa hivi wamemuingiza mkenge Ukraine. Ghuba huko wamemuingiza Mkenge Saudi Arabia na nchi zingine za Kiarabu kuwa ndio "frontline" yao kwa Wa Iran na nchi zingine huko zenye watawala wasikubaliana nao.

Vietnam, waliwahenyesha, Taliban wamewahenyesha mpaka sasa hivi wanaugulia majeraha. Somalia ndio hawana hamu kabisa, wameifanya Kenya kuwa ndio frontline yao, ni heri Tanzania walistuka mapema.

Ukraine haitabaki salama mpaka isalimu amri, Na USA hataki hii vita iishe haraka kwaani ikiisha, front line yao waliokuwa wanaiunda ndio itakuwa imeshasambaratishwa na Warusi wanakuwa karibu zaidi na nchi za NATO, itazimeza moja moja, sio kwa kuzivamia bali kwa zenyewe kutii amri yao wataponyanyuliwa sauti.
umemaliza kila kitu!
 
Back
Top Bottom