Namheshimu zaidi mbunge wa Rochdale, George Galloway.
Mwaka 2005 aliitwa na kamati ya Senate US akituhumiwa kujinufaisha na mpango wa UN wa mafuta kwa chakula nchini Iraq. Baada ya mahojiano waliomwita walijutia uamuzi wao kwa jinsi alivyowaumbua.
Alifukuzwa uanachama chama cha Labour kutokana na misimamo yake, hasa kupinga vita ya Iraq, lakini alishinda ubunge tena kupitia chama alichoanzisha cha Respect.
Mwezi wa Februari mwaka huu ameshinda kwa kishindo ubunge wa Rochdale katika uchaguzi mdogo, akigombea kupitia chama cha Workers party alichoanzisha. Kwa aibu, Rish Sunak alisema ushindi huo wa kishindo ulitokana na wingi wa wapigakura waislamu katika jimbo hilo.
Msikilize hapo chini akiongea na mwanahabari baada ya kushinda ubunge jimbo la Rochdale.
View attachment 2983230