Kwamba kuna misaada ya siri ambavyo mimi na wewe hatuijuwi?......
Kama hivyo ndivyo, Russia naye anapokea misaada ya siri ambavyo mimi na wewe hatuijuwi.
Najua wewe hua ni mbishi wa kukubali ukweli.
Iko hivi,kwa mujibu wa uliemjibu ni kwamba.
"Ukraine anapata misaada kutoka west inayowekwa hadharani na misaada mingine inatolewa kwa Siri."
Sasa wewe Kwa kupenda kwako ubishi unasema hata Urusi nae anapewa misaada kwa Siri.
Sawa.
Kwa hiyo bado hoja inabali pale pale kua, Ukraine inapewa misaada kwa uwazi na usiri.
Lakini hakuna ushahidi kwa Urusi kua anapewa misaada kwa uwazi,hadharani ama inayojulikana.
Sasa Mimi nakuambia hivi,
sijawahi kuona ama kusoma ama kuisikia popote pamefanyika mikutano ya ama wakuu wa kijeshi wa nchi nyingi kwa pamoja wakijadili kuisaidia Urusi kwa pamoja kama wanavyokaa wakuu wa kijeshi wa NATO na west wakijadili kuisaidia Ukraine Kwa silaha, fedha na maarifa.
Pia sijaona wala kusoma wala kusikia wakuu wa nchi,au mawaziri wa nje,au wa ulinzi wa nchi nyingi kwa pamoja wakijadilia kuisaidia Urusi kama wanavyokaa wakuu wa nchi za NATO na west,G7,EU n.k kujadili kuisaidia Ukraine.kwa silaha,fedha na maarifa.
Sijawahi kusoma wala kusikia wala kuona nchi nyingi kwa pamoja zikihimizana kupeleka michango ya fedha ama silaha ama kuiwekea na kuiongezea vikwazo Ukraine kama wanavyofanya kwa Urusi.
Sijawahi kuona ama kusikia ama kusoma nchi zikiiwekea vikwazo ama kuitenga Ukraine kama inavyowekewa na kutengwa Urusi.
Kwa hiyo, hizo ndizo tofauti za misaada anayopewa Ukraine na kile ambacho wewe unasema kua Urusi nae anapewa misaada.
Najua utazungumzia drone za Iran,
Je hizi dron zilikua ni misaada ama Iran ilitaka kujaribu drone zake?
ama Iran ilifanya biashara na Urusi?
Mimi sijui,
je Kwa wakati Iran inatoa dron hizo Urusi ilikua Ina uhitaji wa dron hizo?
Au Urusi haikua na dron kabisa?
Je Urusi ilikua imezidiwq halafu droni za Iran zikaja kuongeza nguvu?
Ama Urusi ilikua inasonga mbele halafu droni za Iran zikaja kuongeza nguvu?
Je unaweza kulinganisha au kufananisha drone za Iran alizompa Urusi (kama misaada),dhidi na silaha,fedha, intelligence,ushauri,vikwazo kwa Urusi,masanaries,mafunzo na misaada mingine yote anazopewa Ukraine na NATO west toka vita ianze?
Naomba tuwe wakweli.