Mkuu,
kp kipanya44 , wewe hakika unachekesha sana. Mbona unajitoa ufahamu au kusahau kwamba huyo ^mbuzi^ ni wa Ukreni, na wala si wa Urusi?
Zelensky alishaambiwa mubashara kwamba yeye hana karata na wala hawezi kupambana na Urusi - hata akiwa na msaada wa Marekani na NATO. Hili nalo umesahau?
Namna pekee ya Ukreni kuwa salama ni kukubali ardhi yake imegwe na ikaliwe na Urusi, kuiachia Marekani rasilimali zake, na kuzikacha ndoto zake za kujiunga NATO.
Trump anachofanya sasa ni kuwaliwaza tu ili huo mkataba wa madini usainiwe. Kumbuka kwamba Russia na Marekani ndio walianza kukaa meza moja huko Saudia, na wala Ukreni na NATO hawajui kilichojadiliwa.
Mimi nina hakika kwamba kwenye ule mkutano, Urusi na Marekani walikubaliana kuifanya Ukreni kama ambavyo Afrika ilifanywa kutokana na mkutano wa Berlin 1884-5.
Kama Marekani sasa hana masihara na nchi kama Kanada jirani yake kabisa, sembuse Ukreni ambayo kimsingi ni Warusi walewale wanaochukiwa na Marekani?
Mwambieni Zelensky na NATO furaha yao ya kuona Ukreni kuendelea umwagaji damu wa watu wao, bila shaka inaelekea mwisho.