Kwa miaka mingi, alisifiwa kama shujaa. Kwa wengine, bado yuko hivyo. Sasa mambo yake yamefichuliwa.
Hii hapa historia ya Ukraine na Volodomyr Zelenskyy ambayo hutoisikia kwenye vyombo vya habari.
Kamwe Zelenskyy hajawahi kuwa na karata ya maamuzi. Yeye si kiongozi fulani jasiri afanyaye maamuzi.
Bali ni mtu aliyekata tamaa, anayeng'ang'ania madaraka katika utawala unaoanguka - unaotegemezwa kwa fedha, silaha na propaganda za Magharibi.
Na huku Ukraine ikipoteza vita vya umamluki & vita halisi, basi anazidi kutaharuki.
Ukraine haikuwa mhusika huru katika vita hivi. Madalali halisi wako Washington, Brussels na London, wakicheza michezo yao ya siasa za dunia.
Vita hivi vilitengenezwa ili kuidhoofisha Urusi. Ili kuelewa hilo, unahitaji kuifahamu historia ambayo kamwe hawatokwambia.
Ukraine na Urusi zimefungamana pamoja kwa zaidi ya miaka 1,000.
Kiev, mji mkuu wa Ukraine, ambayo wakati fulani ilikuwa moyo wa Warusi wa Kiev - nchi kubwa ya kwanza ya Waslaviki - iliweka misingi ya Urusi yenyewe.
Jina lenyewe la Ukraine humaanisha ^nchi ya mpakani^ - ikiwa na maana ya mpaka wa Urusi.
Kwa karne nyingi ilikuwa sehemu muhimu ya Himaya ya Urusi, siyo taifa fulani ^lililokandamizwa.^
Hata wakati wa enzi ya Sovieti, Ukraine haikutawaliwa - ilikuwa ni kiini cha USSR.
Hata kiongozi wa Sovieti Nikita Khrushchev alikuwa Myukreni.
Wakati USSR ilipoanguka, Ukraine ilijitegemea na Washington ikajiingia humo - siyo kuisaidia Ukraine, bali kuitumia kama silaha dhidi ya Urusi.
Marekani na NATO walimdanganya Gorbachev, wakimwahidi kwamba hawangejitanua hata ^inchi moja kuelekea mashariki.^
Hata hivyo NATO ikajiingiza Polandi na katika Mataifa ya Baltiki.
Ukraine ilikuwa tuzo ya mwisho ya NATO.
Nchi za Magharibi zikamwaga mabilioni ya fedha Ukraine—kufadhili vikundi vya kisiasa vinavyounga mkono NATO, NGOs na vyombo vya habari ili kuunda taifa linaloipinga Urusi.
Mnamo 2004, CIA ikaunga mkono ^Mapinduzi Mkakati,^ ikipindua uchaguzi uliomstahabu mgombea anayeunga mkono Urusi.
Mapinduzi halisi yakatokea mnamo 2014.
Rais wa Ukraine aliyechaguliwa kidemokrasia, Viktor Yanukovych, aliukataa mkataba wa kibiashara wa Umoja wa Ulaya ambao ungeuharibu uchumi wa Ukraine.
Jambo hilo halikukubalika Washington. Kwa hiyo wakamwondoa kupitia mapinduzi ya kutengenezwa.
Kile kilichoitwa ^Mapinduzi ya Maidan^ hazikuwa harakati za maandamano ya umma.
Yalikuwa ni mapinduzi yaliyochochewa na CIA—yaliyoratibiwa na maafisa kama Victoria Nuland.
Washington ilikuwa jeuri mno kiasi kwamba Nuland alinaswa hata kwenye simu iliyovuja, akimteua kiongozi anayefuata wa Ukraine hata kabla Yanukovych hajaondoka.
Umati wenye vurugu ulioiteka Kiev hawakuwa waandamanaji wa amani.
Walikuwa wakiongozwa na vikundi vya Wanazi mamboleo kama Azov Battalion—vikundi vinavyosherehekea waziwazi washirika wa Kinazi na kuvaa nembo za SS.
Makundi hayahaya ndiyo sasa yanapokea silaha za Magharibi.
Kisha huo utawala uliofuata baada ya mapinduzi ukapiga marufuku lugha ya Kirusi - ukiwashambulia moja kwa moja mamilioni ya Waukraine wazungumzao Kirusi washio ukanda wa mashariki.
Huo ndio wakati ambapo Donbass & Crimea zikasema sasa imetosha.
Crimea ikapiga kura za maoni - zaidi ya 90% wakapiga kura kurudi Urusi. Donbass nayo ikapiga kura ya kuwa huru.
Watu wa Donbass wakaikataa Kiev - lakini Kiev haikutaka kuwaruhusu waende.
Badala yake, wakaanzisha vita vya kikatili dhidi ya watu wao wenyewe, wakiwafyatua raia hao kwa miaka minane.
Je, hasira ya Magharibi tuionayo leo ilikuwa wapi wakati huo? Haikuonekana popote!
Na vipi kuhusu Zelenskyy? Yeye ni nani? Je, ni kiongozi asilia ambaye hakutokea popote au alipandikizwa?
Imeripotiwa kwamba mnamo 2020, Zelenskyy alikutana kisiri na mkuu wa MI6 Richard Moore.
Kwa nini rais wa nchi nyingine akutane na jasusi mkuu wa Uingereza badala ya waziri mkuu wake?
Je, Zelenskyy ni mali ya Uingereza?
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, yeye binafsi analindwa na Waingereza, wala siyo wanausalama wa Ukraine.
Alipoitembelea Vatikani, alimkacha Papa na kukutana na askofu wa Uingereza.
Unaweza kumkisia nani mwingine aliyekuwa hapo? Richard Moore wa MI6 tena! Lazima hilo liwe mgongano ulioje wa matukio. Au siyo?
Kabla ya siasa, Zelenskyy alikuwa mchekeshaji na mwigizaji - kimsingi akivaa uhusika wa rais kwenye maonesho ya luninga.
Ndipo, kwa msaada wa timu za Magharibi za mahusiano ya umma, nadharia hiyo ikawa ukweli.
Kampeni yake ilifadhiliwa na kibosire Ihor Kolomoisky, aliyekuwa akimiliki kampuni kubwa zaidi ya mafuta na benki nchini Ukraine.
Akiwa madarakani, kipaumbele cha Zelenskyy hakikuwa kupambana na ufisadi - ilikuwa ni kuhakikisha makampuni ya BlackRock & benki za Magharibi zinateka uchumi wa Ukraine.
Wakati huohuo, alihamishia mamilioni kwenye akaunti za nje ya nchi, na inadaiwa alinunua jumba la kifahari la dola 34M huko Miami pamoja na ghorofa huko London lenye thamani ya paundi nyingi.
Hakuna kitu chochote ambacho kingeshangaza iwapo alifanya hivyo.
Kufikia mwaka 2022, NATO ilikuwa imeipa Ukraine silaha hadi kiwango kilichokubuhu, na Kiev ilikuwa imekusanya vikosi karibu na Donbass.
Urusi ilikuwa na chaguo la kufanya:
Iache Donbass ikabiliwe na usafishaji wa kimbari;
Iache NATO iigeuze Ukraine iwe kambi la kijeshi;
Au,
Iingilie kati.
Waliingilia kati, kama ambavyo mataifa mengine yangeingilia katika hali hizo.
Vyombo vya habari vikapiga kelele ^amevamia bila kuchokozwa.^
Lakini kujitanua kwa NATO, mapinduzi ya 2014, miaka minane ya vita dhidi ya Donbass - vita hivi vilisababishwa na uchokozi katika kila hatua njiani.
Ukraine ilitegwa kama chambo.
Huku Ukraine ikipoteza vita sasa, Zelenskyy anatelekezwa.
Donald Trump alimwambia: ^Wewe huna karata.^ Na yuko sahihi.
Vita hivi vilitengenezwa. Ukraine ilihitaji Magharibi iingilie kati ili kushinda na hilo lingemaanisha kwamba VV3 visingeepukika.
Ni wakati wa dunia kuzinduka ili kuutambua ukweli huo.
Vita Ukraine vilitokana na chokochoko za makusudi za nchi za Magharibi.
Zelenskyy ni kibaraka mwingine tu—muda wake unayoyoma... na Trump anajua hilo.