Special Treads for USM ALGER VS Dar es Salaam Young Africa

Mpira ni akili kama ilivyo akili ya kuwa daktari au engineer. Ukiongea watu hawakuelewi but that is the reality. Wachezaji wetu hawana akili ya darasani wala ya mpirani. Yote haya ni zao la elimu yetu mbovu. Isiyofikirisha, isiyochunguzisha, isiyoibusha vipaji na umahiri. Elimu yetu haijengi akili. Imekaa kukata na kupaste tu na kucopy copy, kufanya mitihani na kusubiri ajira zisizokuwepo. This country is doomed. Shida unayoiona uwanjani ndio shida ipo kila sector. Tunatia huruma.
 

duh! hili neno kaka hongera sana
 
Acha ujinga.....badala ya kutuuliza tufanyeje wawakilishi wetu wametuangusha. Unaanza kukenua meno kama mwehu. Stupid
ha ha ha ha, Unenikumbusha ile clip ya yule shabiki wa Yanga aliyempiga kofi mbwa koko - Hasira za kufungwa na Simba.
 
Hakuna kitu Mtanzania anachoweza. Ukiondoa mambo ya umbaji wa MUNGU, Hivi Tanzania inatambulikaje nje ya mipaka yetu?

Mkuu hebu fafanua kidogo kuhusu "Mambo ya umbaji wa Mungu"
 

Wenzetu wana mipango ya miaka kumi ijayo huku kwetu waziri husika dk mwakyembe yupo wizarani kwa kazi maalum ya kufungia magazeti yanayomkosoa mkuu na kupiga porojo za uwekezaji kwenye michezo huku serikali haitoi hta mia
 
Ulitegemea nini timu haina robo tatu ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza?Yondan, Tshimbi, Ajibu, Ngoma, Chirwa, Tambwe,

Wamesajili wachezaji 29 kwaajili ya Ligi, kukosekana kwa hao isiwe sababu, Tatizo hata hao waliokwenda wana nidhamu ya woga. kinachosumbua Yanga ni posho/mishahara/ mafao ya wachezaji, hao ambao hawakwenda wanajitambua.
 
mpira wa Jana uliangalia wachezaji waliocheza
hivi haujui kuwa Kuna mgomo wa wachezaji kutolipwa pesa zao za mishahara
mbona mnataka kulaumu timu wakati tunajua mapito inayopitia. Binafsi naona wachezaji waliocheza Jana Ni wazalendo Na wanastahili pongezi. Kufungwa nne sio ishu hata blazil ilifungwa saba. Cha muhimu tunaoijua yanga tunajua Ni mapito Tu timu itakuja kaa sawa
 
Ulitegemea nini timu haina robo tatu ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza?Yondan, Tshimbi, Ajibu, Ngoma, Chirwa, Tambwe,
hawa wengine mkuu mpira hawafuatilii hata wachezaji waliocheza Jana hawawajui. Kazi kuponda bila mantiki
 
Tuweke kumbukumbu sawa halafu ndo tuendelee na majadiliano
 
Lilipo ingia la 3
Kwanza Niliona napoteza usingizi wangu burebure
Najisikiaga Amani Simba wakienda nje walau kidogo hatupati Aibu kama hii
kwani Simba awakuwemo katika haya mashindano
ALHAHOOD 5 SIMBA 1
LIBOLO 4 SIMBA 0
 
Tatizo ya timu zetu wanaangia katika mashindano bila ya malengo na mtarajio.
Uwezi shindana bila ya matayarisho una bajeti ya mashindano.
Yanga hadi kufikia hapo aikuwa matarajio yao imekuja kama bahati tu.
Na viongozu kusema ukweli kwao ni mwiko ni Uongo kwa kwenda mbele.

Hii timu inamilikiwa na wanachama kama kuna tataizo mnarudi kwa wenye kumiliki timu na kuwaeleza wao kama waajiliwa waone hao wanaomiliki timu watachukua uwamuzi gani?
Lakini wao viongozi wanaona kama ndio watawala na wanamaamuzi ya kila kitu.

Poor mchezo wa mpira katika nchi hii
Poor uongozi wa Yanga
Poor wanachama wa YANGA
 
Young Africa Sports Club hii ni aibu kubwa sana mchezo dhidi ya USM Alger,

Magoli ni 4-0,
Ball possession 76% kwa 24%,
Shots on target 9 kwa 1,
Shots off target 8 kwa 2 na
Total passes 750 kwa 232

Nani amewaloga?
Hawakupata Conner hata moja?
 
Mwaka jana walitolewa na MC ALGER kwa kufungwa 4-0 na wachezaji wote wapo pamoja na DIDA, KAMUSOKO, MSUVA, NIOYONZIMA, CHIRWA, NGOMA na YONDANI.

Uwanja wa Taifa Yanga 1 MC Alger 1
Algeria MC Alger 4 Yanga 0 aya matokeoa ya mwaka jana

Tatizo ni matayarisho atuna tunakukurupuka tu na kucheza mpira wa Hamasa atuwezi kufika popote labda uwe mwaka wa bahati tu.
Tuache visingizio
 
Young Africa Sports Club hii ni aibu kubwa sana mchezo dhidi ya USM Alger,

Magoli ni 4-0,
Ball possession 76% kwa 24%,
Shots on target 9 kwa 1,
Shots off target 8 kwa 2 na
Total passes 750 kwa 232

Nani amewaloga?
Bado wamebeba kesi ya Manji akilini mwao!
 
Hizo kauli zako huwa sizitaki hata kuzisikia. Unafurahia kufungwa 4-0? Yanga unaweza kuilinganisha na Brazil? Hata kwa miaka 100 huwezi kuilinganisha. Mgomo wachezaji kwasabb hawajalipwa ni sbb ya kijinga sana sitaki hata kuisikia. Si waache kucheza kwann Yanga ndiyo timu pekee? Wafrika tunasafari ndefu sana ktk uwanjwa soka.
Kuna wakati huwa naona ni upuuzi kushabikia hizi timu za nyumbani. Unafungwa 4-0 bila unajisifu?
Shubamit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…