SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

Naheshimu sana mawazo yako siku zote , je hapa nini kifanyike kufanya tuwatue hawa speedaf
Idea si mbaya mkuu sababu inapunguza muda, nchi nyingi duniani wanafanya hivi wanakusanya mizigo yote inakuja pamoja.

Ila hilo suala la kuwaachia wabongo mali za watu na kuendesha biashara kienyeji litawacost. Wafanye kama posta tu, mzigo unachukua na Kitambulisho na no ya simu.
 
Nimeanzisha mada ili tupaze sauti ninaimani kabisa hawa kikuu waliochangamka wanasoma ujumbe wetu humu ndani
 
Shida nyingine ilyopo ni coverage yao, utalazimika kusafiri ili kuwaendea na kitambulisho chako. Kobe akiinama anatunga sheria. Wakati mwingine huwa naona huruma labda bado wanachekecha akili jinsi ya kuendesha biashara yao. Huenda pia hawakufanya tathmini kabla ya kuchukua mkopo.

Sent from my cupboard using mug
 
dronedrake Hapo ukute ulimuagizia mtu iwe binamu au jirani yako wewe utakausha na kuondoka mikono nyuma sawa je huyo uliyemuagizia utamkabili vipi akubali kupotezea 500K yake kirahisi hivyo?
kwanza simuagizii mtu, nitamuelekeza aagizie mwenyewe

pili, kwa 500k siwezitumia courier uchwara, naongezea fee nitumie aramex, fedex au dhl

tatu, kuna watu wawili hapo, muuzaji na msafirishaji, kama item umeitrack na inaonekana imefika, muuzaji hahusiki hapo na kung'ang'ania refund ni kukosa busara
 
Speedaf ni wapuuzi sana, niliagiza kioo cha redmi note 10 5g ndani ya siku 4 kilikuwa tz. Kesho yake tracking ikasoma Dodoma, baada ya siku 3 agent akawa amesign kuderivery mzigo. Kama siku 4 mbele mzigo ukawa signed na agent na namba yake ya simu ikaonekana. AliExpress wakanitumia delivery note ya mzigo kuwa nimeupokea wakati sijauona, nikaenda posta kuangalia kama ulifikia kwao nao hawakuuona.

Ile namba niliipigia zaidi ya wiki na haipatikani, nikawasiliana na muuzaji akanitumia namba ya makao makuu Tanzania ile namba hata haipokelewi.
Wakati nimekata tamaa nikaijaribu kuipigia ikapokelewa nikamuuliza kuhusu kupokea mzigo wangu akanielekeza niufuate nyumbani kwake na ni nje kidogo ya mji. Kiukweli alinikera huyo jamaa na hapo nyumbani kwake alikuwa na mizigo mingi ya watu wengine.
 
Asee kwahiyo msipodindia mnakula za uso.
Yaani jamaa anafungua kabisa homeshop hapo kwake
 
Wameshaanza uhuni siku hizi kwa baadhi ya mikoa ili uchukue mzigo lazima upite TRA

Ukifika TRA unadondoshewa rungu la "IMPORTATION FEES" asilimia 18!.
Duh[emoji50]‍[emoji100]
 
Mkuu, huyo agent aliwezaje kuingia kwenye account yako na kuthibitisha kama umepokea mzigo wako?
Hapa Bado sijaelewa.
 
Mkuu, huyo agent aliwezaje kuingia kwenye account yako na kuthibitisha kama umepokea mzigo wako?
Hapa Bado sijaelewa.
Ukipokea mzigo kuna document huwa una sign, zile taarifa ulizojaz na uka sign ndiyo wanazotumia kujaza kwenye tracking system baada ya hapo kule AliExpress itaonyesha mzigo umefika na umepokelewa na jina la alieupokea linakuwepo
 
Ukipokea mzigo kuna document huwa una sign, zile taarifa ulizojaz na uka sign ndiyo wanazotumia kujaza kwenye tracking system baada ya hapo kule AliExpress itaonyesha mzigo umefika na umepokelewa na jina la alieupokea linakuwepo
Speedaf unaweka signature juu ya mzigo husika kama inavyoonekana pichani then wanapiga picha ndio imeisha hiyo
View attachment 2439200
 
Unique Air Cargo ndio mashivo a.k.a Ma Master wa hizi mambo za Usafiri.

Hawajawahi kuniangusha na ni watu serious sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…