SpeedAf, Mkombozi kwa wanyonge

SpeedAf, Mkombozi kwa wanyonge

Wako vyema sana. Hai jamaa..

Ila kuna kaparcel naona kamefika bongo. Nilipompigia jamaa wa speedaf akaniambia huo mzigo umepitia posta.

Embu nisaidie mkuu naupataje happo posta?

Posta watakutumia SMS kuwa mzigo umefika, ipo inayofikia mjini na ipo inayofikia posta ya Kiji...

Kama una muda unaweza ukapita mwenyewe posta town pale upande wa parcel, ukiwapa tracking number watakuambia kama upo customs au wanao wenyewe tayari
 
Eg kitu Cha 3K

Usafiri cainiao ambao walishirikiana na speedaf unakuta 90tzs

Yanwen 980tzs

AliExpress standard shipping 3K usafiri

Kwa uzoefu wangu gharama za usafiri kwa Aliexpress standard shipping ni kama mara 2 ya Cainiao super economy, lakini sasa super economy na free shipping kuna asilimia kubwa ya mzigo kupitishwa Posta...

Na ukishapitishwa Posta basi jiandae kwa service charge isiyopungua 2500 kwa small package au zaidi kwa vitu vingine haswa electronics...

Halafu sasa kuna mizigo mingine utasukumiwa ofisi za TRA waliopo hapo hapo nao watakucharge...

Bado hujaongeza nauli na muda wa kufuata mzigo Posta...
 
Halafu sasa kuna mizigo mingine utasukumiwa ofisi za TRA waliopo hapo hapo nao watakucharge...
Hi mizigo inakuwa ya namna gani

Me kipindi mizigo inakuja posta ilikuwa naambiwa nilipie 2350tzs

Speedaf ikawa nafuu nalipaga elf moja Tena mizigo ya free shipping ilikuwa inawahi balaa na cainiao ,, kwa hio kwa sasa tuchague AliExpress standard shipping
 
Hi mizigo inakuwa ya namna gani

Nimeona wakicharge nguo, electronics...unataja thamani ya mzigo wanakupa gharama za kodi...

Me kipindi mizigo inakuja posta ilikuwa naambiwa nilipie 2350tzs

Hiyo ni kwa parcel ndogo ndogo zile...

Juzi kati hapa nimetoka kuchajiwa 5900TZS, ilikuwa ni mzigo wa electronics, bahati nzuri walipousogeza TRA, yule mama sijui kwa nini alinisamehe baada ya kumtajia bei ya manunuzi (nahisi wana kiwango wakiona bei wanakuchaji labda wazoefu zaidi wanaweza weka sawa hapa), lakini kuna jamaa alikuwa na nguo suti 2 pale, nilimuacha anajiandaa kuzilipia...

Speedaf ikawa nafuu nalipaga elf moja Tena mizigo ya free shipping ilikuwa inawahi balaa na cainiao ,, kwa hio kwa sasa tuchague AliExpress standard shipping

Speedaf hizi hand parcels nyingi huwa hazina extra charges tofauti na ile uliyolipia aliexpress...

Wao kwa electronics huwa wanacharge kama 2000 tu hivi kama malipo ya ziada...
 
Wako vyema sana. Hai jamaa..

Ila kuna kaparcel naona kamefika bongo. Nilipompigia jamaa wa speedaf akaniambia huo mzigo umepitia posta.

Embu nisaidie mkuu naupataje happo posta?
Hapo sijajua ila kama tracking number zako hazianzi na TZ hapo kuna uwezekano mkubwa mzigo wako ukapita posta hapo ndo hua kuna msala, mi niliagiza mizigo miwili, siku moja, mmoja ulikuja na SpeedAf na mwingine Posta, ilikua tar 30/10/2023 tar 17 mwezi wa 11 nilipata wa speedAf ila wa posta hadi leo tar 29/Dec/23 sijapata na ulishaingia Dar kitambo sana,
Posta ni janga mkuu.
 
Nimeona wakicharge nguo, electronics...unataja thamani ya mzigo wanakupa gharama za kodi...

Hiyo ni kwa parcel ndogo ndogo zile...

Juzi kati hapa nimetoka kuchajiwa 5900TZS, ilikuwa ni mzigo wa electronics, bahati nzuri walipousogeza TRA, yule mama sijui kwa nini alinisamehe baada ya kumtajia bei ya manunuzi (nahisi wana kiwango wakiona bei wanakuchaji labda wazoefu zaidi wanaweza weka sawa hapa), lakini kuna jamaa alikuwa na nguo suti 2 pale, nilimuacha anajiandaa kuzilipia...

Speedaf hizi hand parcels nyingi huwa hazina extra charges tofauti na ile uliyolipia aliexpress...

Wao kwa electronics huwa wanacharge kama 2000 tu hivi kama malipo ya ziada...
Mkuu huo maizo wako wa posta ulitumia shipping method ipi na ilichukua muda gani mpaka kuupata.
Na uliagiza kipindi gani.
 
Hapo sijajua ila kama tracking number zako hazianzi na TZ hapo kuna uwezekano mkubwa mzigo wako ukapita posta hapo ndo hua kuna msala, mi niliagiza mizigo miwili, siku moja, mmoja ulikuja na SpeedAf na mwingine Posta, ilikua tar 30/10/2023 tar 17 mwezi wa 11 nilipata wa speedAf ila wa posta hadi leo tar 29/Dec/23 sijapata na ulishaingia Dar kitambo sana,
Posta ni janga mkuu.
Kwanza hata kwa kuanzia sijui yaani ni week ya tatu upo bongo. Ila hakuna cha simu wala taarifa yeyote.
 
Mkuu huo maizo wako wa posta ulitumia shipping method ipi na ilichukua muda gani mpaka kuupata.
Na uliagiza kipindi gani.

Niliopt kutumia Aliexpress Standard Shipping kwa kuwa kilikuwa ni kitu cha muhimu na nahitaji kwa haraka lakini wauzaji wakaamua kuupitisha Uzbekstan Post, hivyo ukaja kwa njia ya Posta...

Order niliweka 24 Nov wakati wa offer za Black Friday, mzigo nikatumiwa SMS 18 Dec kwenda uchukua (almost mwezi)...
 
Back
Top Bottom