Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itawezekana tu kama kila shule itakuwa na ikama halisi ya walimu na viwezeshi katika uwezeshaji wa wanafunzi.Serikali yapiga marufuku masomo ya ziada
Bongo5Jun 22, 2021Soma halisi
Serikali imepiga marufuku masomo ya ziada kwa shule za Serikali na hasa wakati wa likizo, kwa kubainisha kuwa yanaongeza gharama zisizo za lazima kwa wazazi na ni kinyume na waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016,ambao unataka wanafunzi wapate likizo ama muda wa kupumzika.
Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Prof. Joyce Ndalichako wakati akitoa taarifa kwa mbunge wa Bukoba Vijijini Mh.Jasson Rweikiza aliyetaka ufafanuzi kwa waraka uliotolewa na kamishna kutoka Wizara ya Elimu uliotaka shule zote zifungwe wakati wa likizo.
Waziri Ndalichako amesema kuna baadhi ya shule za Serikali zinalazimisha wanafunzi na wazazi kuchangia gharama kwa kipindi chote cha likizo ambacho wao wanatumia kufundishwa.Hiyo si sawa na inakiuka lengo la Serikali la kutoa Elimu bila malipo kwa Wananchi.Na hii imekua ni uchochoro wa watu kujipatia pesa.Na hizi tozo zimekua kama gharama ya Elimu zinarudishwa kwa sura nyingine.
“Serikali imeweka mfumo wa kwenda likizo kwa sababu akili ya binadamu inachoka, siku 194 za masomo ambazo zimewekwa kwa mwanafunzi kusoma zinatosha, wanafunzi wanahitaji kupumzika, kukaa na familia zao na kufanya shughuli nyingine, mfano wanafunzi wa kidato cha nne wamefungua shule Januari 13,na wanatarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza mwezi wa 11,ukisema mtoto asifunge shule mwezi wa sita sio sawa.Sisi kama serikali bado tunaona na tunatambua umuhimu wa likizo”amefafanua Waziri Ndalichako.
Vile vile Waziri Ndalichako amewaelekeza maafisa Elimu Wilaya na Mikoa, kuacha kupoka mamlaka ya kuweka Sera kwa kuwa Serikali imebaini maeneo mengi shule zinafungwa kwa maagizo ya Maafisa Elimu, bila ya Waziri wa Elimu wala Tamisemi kuwa na taarifa.
Nikatishe mada kwa kusema, Ndalichako akitaka aondoe masomo wakati wa likizo, ahakikishe kila shule ina walimu kulingana na mahitaji, vyumba vya madarasa vya kutosha na vitendea kazi vya kutosha,atafanikiwa. Vinginevyo atabaki kuwa waziri wa masifuri[emoji1545][emoji1545][emoji1545]Itawezekana tu kama kila shule itakuwa na ikama halisi ya walimu na viwezeshi katika uwezeshaji wa wanafunzi.
Ualimu si sawa na kazi yoyote ile duniani. Ikitokea mwalimu kapewa jukumu lingine na kipindi kikipita, basi hiyo hasara ni ya milele.
Huwezi kusema kipindi kijacho nitafundisha yote mawili. Kinachofuata ni kutafuta muda usio wa masomo ndo ufidie kipindi kilichopotea.
Masomo ya muda wa ziada (hasa kwa shule za msingi za serikali) husababishwa na mambo kadhaa.
Kwanza shule nyingi hazina walimu wa kutosha hivyo vipindi vingi kupotea bila watoto kupewa haki yao.
Pili, hata hao walimu wachache waliopo, kuwasimamia ni vigumu kwa kuwa serikalini kumejaa utovu wa nidhamu, unafiki na dharau dhidi ya walimu wakuu kiasi kwamba mwalimu akijifanya mfuatiliaji sana kitamkuta cha kumkuta. Mwalimu mkuu hana fully authority juu ya mwalimu anayetakiwa amsimamie ili afanye kazi inayotakiwa.
Tatu, walimu waajiriwa wa serikali kwa msahahara walio nao, wakibweteka watakufa njaa. Ndo maana muda mwingi huwatumia wanafunzi kuuza ubuyu, mihogo, vitumbua, ice-cream na viburudisho vingine. Je mtoto huyu atasoma na kufanya/kufanyishwa biashara?
Nne, huku vijijini kuna maeneo maji ni kuvizia. Ratiba ya siku haiwezi kukamilika bila kuvunja vipindi viwili kwa ajili ya wanafunzi kwenda kuwachotea maji walimu. Vipindi hivyo vitafidiwa vipi kama si muda wa likizo?
Tano, mada za masomo kwa mitaala ya Tanzania ni nyingi mno. Kwa bahati mbaya katika siku 195 za masomo, hakuna muda wa ziada uliowekwa. Hapo ni masomo tu. Hakuna muda wa kutosha kufanya tathimini. Kwa umri wa watoto wetu wa shule za msingi sasa, wengi hawamudu mchakamchaka huu. Mwalimu anajikuta anaburuza wanafunzi awahi kukamilisha tu muhtasari wa somo. Content haizingatiwi.
Sita, kuna watoto wanakosa vitabu vya masomo hadi anamaliza mwaka mzima baada
ya mabadiliko ya mtaala.
Nikatishe mada kwa kusema, Ndalichako akitaka aondoe masomo wakati wa likizo, ahakikishe kila shule ina walimu kulingana na mahitaji, vyumba vya madarasa vya kutosha na vitendea kazi vya kutosha,atafanikiwa. Vinginevyo atabaki kuwa waziri wa masifuri.
Ya kuandikia ratiba ya kuoga na kuswakaPeni ya nini toilet!!!? View attachment 1845182
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]ile kalamu hayo ndio matumizi yakeMichoro hadi toilet. Sijawahi kuwaelewa wtt jamani [emoji848]View attachment 1845184
Wameona vyumbani haitoshi...hadi toilet![emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]ile kalamu hayo ndio matumizi yake
Sent using Jamii Forums mobile app