Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

Itawezekana tu kama kila shule itakuwa na ikama halisi ya walimu na viwezeshi katika uwezeshaji wa wanafunzi.
Ualimu si sawa na kazi yoyote ile duniani. Ikitokea mwalimu kapewa jukumu lingine na kipindi kikipita, basi hiyo hasara ni ya milele.
Huwezi kusema kipindi kijacho nitafundisha yote mawili. Kinachofuata ni kutafuta muda usio wa masomo ndo ufidie kipindi kilichopotea.
Masomo ya muda wa ziada (hasa kwa shule za msingi za serikali) husababishwa na mambo kadhaa.

Kwanza shule nyingi hazina walimu wa kutosha hivyo vipindi vingi kupotea bila watoto kupewa haki yao.

Pili, hata hao walimu wachache waliopo, kuwasimamia ni vigumu kwa kuwa serikalini kumejaa utovu wa nidhamu, unafiki na dharau dhidi ya walimu wakuu kiasi kwamba mwalimu akijifanya mfuatiliaji sana kitamkuta cha kumkuta. Mwalimu mkuu hana fully authority juu ya mwalimu anayetakiwa amsimamie ili afanye kazi inayotakiwa.

Tatu, walimu waajiriwa wa serikali kwa msahahara walio nao, wakibweteka watakufa njaa. Ndo maana muda mwingi huwatumia wanafunzi kuuza ubuyu, mihogo, vitumbua, ice-cream na viburudisho vingine. Je mtoto huyu atasoma na kufanya/kufanyishwa biashara?

Nne, huku vijijini kuna maeneo maji ni kuvizia. Ratiba ya siku haiwezi kukamilika bila kuvunja vipindi viwili kwa ajili ya wanafunzi kwenda kuwachotea maji walimu. Vipindi hivyo vitafidiwa vipi kama si muda wa likizo?

Tano, mada za masomo kwa mitaala ya Tanzania ni nyingi mno. Kwa bahati mbaya katika siku 195 za masomo, hakuna muda wa ziada uliowekwa. Hapo ni masomo tu. Hakuna muda wa kutosha kufanya tathimini. Kwa umri wa watoto wetu wa shule za msingi sasa, wengi hawamudu mchakamchaka huu. Mwalimu anajikuta anaburuza wanafunzi awahi kukamilisha tu muhtasari wa somo. Content haizingatiwi.

Sita, kuna watoto wanakosa vitabu vya masomo hadi anamaliza mwaka mzima baada
ya mabadiliko ya mtaala.

Nikatishe mada kwa kusema, Ndalichako akitaka aondoe masomo wakati wa likizo, ahakikishe kila shule ina walimu kulingana na mahitaji, vyumba vya madarasa vya kutosha na vitendea kazi vya kutosha,atafanikiwa. Vinginevyo atabaki kuwa waziri wa masifuri.
 
Nikatishe mada kwa kusema, Ndalichako akitaka aondoe masomo wakati wa likizo, ahakikishe kila shule ina walimu kulingana na mahitaji, vyumba vya madarasa vya kutosha na vitendea kazi vya kutosha,atafanikiwa. Vinginevyo atabaki kuwa waziri wa masifuri[emoji1545][emoji1545][emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…