MAMBO ANAYOTAKIWA KUZINGATIA MZAZI YA KUFANYA MTOTO AKIWA LIKIZO
By sir eliud lusanga
Kipindi hiki watoto wetu wamerudi kwa ajili ya Likizo ni vizuri wazazi kuzingatia haya:
1. Jipe muda wa kuzungumza na MTOTO Kila Siku
2. Muulizie juu ya Changamoto alizokutana nazo akiwa shule
3. kagua vitu anavyovitizama km picha, simu n.k
4.Jadiliana naye kuhusu matokeo yake ya mwaka mzima
5. Kuwa makini sana na aina ya marafiki anaokuwa nao ikiwezekana angalia background ya familia za marafiki zake
6. Mpe muda wa kwenda kwa wazazi wa pande mbili ajifunze mahusiano na familia
7. Hakikisha anapata muda wa kiroho kushiriki ibada na vikundi vya kanisani pia muombe pamoja
8. Usimpe Kila anachotaka mpe kwa sababu ni muhimu
9. Usimdekeze afanye kazi za mikono hata Kama una dada au kaka wa kazi aoshe vyombo, asafishe Nyumba, atandike chumba chake, afue nguo mwenyewe na hata kuhudumia kazi za uzalishaji hapo nyumbani
10. epukeni magomvi ya Mara kwa Mara yatakayomfanya aathirike kisaikologia
11. Kama mmeachana na mzazi mwenzako Hakikisha MTOTO anapata nafasi ya kumsalimia mzazi mwenzako
12.Usiruhusu MTOTO kushinda peke yake chumbani akicheza game mpe nafasi ya kusociliaze lakini kuwe na mipaka
13.Kama Kuna kazi za kijamii kama kutembelea yatima mpe muda afanye charity work itampa tabià ya kujali wengine
14.Epuka Sana kuonyesha kuwa una muogopa na analosema utatekeleza mahali fulani lazima kuwa strictly
15.Mpangie revision kwa kiwango Ili akili ipumzike
16.Anza kujadiliana naye kipawa chake na ndoto zako
17.Mueleze Changamoto zilizopo kama UKIMWI, USHOGA na tabia hatarishi
18.Mfundishe unyenyekevu na kuheshimu wengine
19.Mtie moyo ukimjengea uwezo wa kuwa anaweza
20.Jadiliana naye hali ya uchumi ilivyo katika familia ajue katika maisha Kuna up and down na mfundishe Umuhimu wa kushare Changamoto alizonazo.