Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Sijui kama kuna watu wengi waliliona na kuguswa na hili. Mimi nilianza kukata tamaa na bunge la 11 mapema mwaka 2017 pale Spika, nadhani kwa maelekezo ya Rais, alipomshinikiza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara kujiuzulu nafasi yake kwa kujaribu kuibana serikali iwe 'serious' katika kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu yake ya mara kwa mara kuhusu viwanda! Binafsi, nilifadhaishwa sana na tukio hilo kwani linaashiria kuwa Bunge sasa siyo chombo chenye madaraka yaliyotokana na wananchi moja moja na dhamana ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wapiga kura. Badala yake inaelekea serikali ndiyo inayosimamia Bunge!
 
Hope team nzima ya Raia Mwema itatinga bungeni; hii battle siyo nyepesi. Ni hatari kama hata wawakilishi wetu tuliowachagua wamepoteza unyenyekevu kwetu! Nadhani Mzee Ulimwengu anaweza kuwa na kitu cha kuwakumbusha.
 
Back
Top Bottom