Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Mkuu Pascal Mayalla Nina uhakika utawajibu kwa hoja na kuwashinda, kila la kheri kwako na kwa vile upo hapa jukwaani tutaomba mrejesho kutoka kwako MUNGU akusimamie.

LISSU alisema akimaliza upande wetu atakuja kwa wanahabari hakuna aliye salama.
 
Kwa jinsi ninavyomjua Pascal Mayalla hawatamuweza hyu jamaa anajielewa huwa haandiki jambo asilo na uhakika nalo. Go Pascal Go Mayalla.
 
Maumivu ya kichwa uanza pole pole wanapotaka tutafika dalili ya mvua mawingu Tanzania yetu imetanda wingu zito...
 
hivi yule ndugai alisoma chuo gani na ana kiwango gani cha elimu? hatuwezi kuwa na speaker mpuuzi wa kiwango hiki halafu tuendlee. sasa pascal kaandika kitu gani kibaya pale
 
Hilo ni Rubber Stamp Parliament and the extended arm of the Executive, mbona hilo liko wazi kabisa?
 
Naona sehemu kubwa wanayoilalamikia ni " huduma za kibinadamu"

Ukweli mkubwa alioutoa Mayalla unaachwa.
 
Pascal Mayala huwa aeleweki yuko upande gani .,sasa atatetewa na upande gani..unafiki ni kama upepo unavuma kusikoeleweka.

where to switch and abide.. you too have funny.
Mwandishi wa habari hatakiwi kuwa na upande wowote bali asimamie ukweli.
 
Ushauri wangu kwako ni huu:

Kama simu unayotumia ina uwezo wa kutumika mitandaoni na kama simu yako haina password, basi nakushauri uweke password haraka iwezekanvyo.

Leo Bungeni, kesho unaweza kuitwa kule kwingine ambako huwa hawakosi makosa.

Soma alama za nyakati angali mapema.
 
Ohooo naona mambo ni motooo

kule kwenye uzi wake naona kuna mmoja kamuambia aandaye vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wake ikiwezekana na sehemu walipozikwa
 
Back
Top Bottom