Spika amvaa Mwigulu bungeni kushindwa kujibu swali la Mpina

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Akson ameitaka wizara ya Fedha na Mipango kujibu upya swali namba 129 lililoulizwa na Mbunge Kisesa Luhaga Mpina, ambaye aliitaka serikali kutoa maelezo ya kwanini kesi 1,097 za kodi zenye thamani ya shilingi trilioni 360 na dola za Marekani milioni 181.4 hazijaamuliwa hadi sasa.

Hatua hiyo ya Spika imekuja baada ya majibu ya Naibu waziri wa Fedha na Mipango Hamadi Hassan Chande kwenda kinyume na swali la msingi la Mbunge Mpina.

Hata waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba alipojaribu kutoa ufafanuzi, maelezo yake hayakufanana na swali la msingi la Mbunge huyo wa Kisesa.

Baada ya Spika kuwahoji viongozi hao wa wizara ya Fedha na Mipango na kukosa majibu yanayoridhisha, ndipo akaamuru swali hilo likajibiwe tena kama ambavyo limeulizwa na Mbunge Luhaga Mpina.

CHANZO: TBC

 
Hana lolote la maana mnafiki tu, akipewa uwaziri hutosikia Tena akikosoa
Labda ungeweka wazi unafiki wake ni upi maana Spika ndio amemshambulia Mwigulu kushindwa kujibu swali la Mbunge na Mbunge yeye alikuwa anatekeleza wajibu wake kikatiba na watanzania wote tumeona Sasa mnafiki ni wewe au Mpina?
 
Swali zuri kabisa,wake na majibu..

Pili waje na majibu zile Til.1.3 za CAG zilienda wapi?
 
Mbona swali rahisi sana hilo?
Ni kuwa kuna madai makubwa kiasi hicho kwa sababu ya ule utopolo wa Magufuli eti anawadai Accacia kodi ya trilioni mwaka 360 za makinikia
 
Hana lolote la maana mnafiki tu, akipewa uwaziri hutosikia Tena akikosoa
Waziri hakosoi serikali, Bali anawajibika kwa yale yanayotokea kwa serikali.

Mbunge yeye ndio kazi yake kuisimamia serikali na kuiwajibisha. Hata Bashe alikuwa akikosoa serikali Ila alipopata uwaziri hakuweza kuendelea kwa sababu nilizokupatia.

Hata huko kwenu chadema, Mjumbe kamati kuu hawezi kukosoa chama. Ila mwanachama wa kawaida anaweza kukosoa
 
Sawa msukule wa dikteta Jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…