from chanzo cha uwakika ndani ya vyombo vya usalama wa nchi tusubiri tutaona mwisho wa picha hii ya katiba
Andrew Chenge, mbunge wa Bariadi Magharibi na mwanasheria mkuu wa zamani, amejitoa katika kinyanganyiro cha uenyekiti wa Bunge la Katiba.
Taarifa kutoka ndani ya kinachoitwa, Kambi ya Edward Lowassa zinasema, Chenge ameamua kujitoa katika kinyanganyiro hicho kwa ushauri wa kigogo mmoja mwandamizi katika idara ya usalama wa taifa.
Habari zinasema, sababu ya Chenge kujitoa katika kinyanganyiro hicho ni kumlinda Lowassa asichafuke.
Tunataka mgombea wetu Edward (Lowassa) asichafuke. Kumruhusu Chenge kuwa mgombea wa kiti cha uspika (uenyekiti), ni kuhalalisha kuchafuliwa Lowassa, ameeleza mmoja wa makada wa CCM ambaye yuko karibu na Lowassa.
Amesema, Tumepima na kugundua kwamba Chenge akiwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba, wabaya wa Lowassa baada ya kujadili katiba watamshambulia Chenge na Lowassa. Jambo hili litatugharimu na hivyo tumeona tumuachie mzee Sitta msalaba wake.