Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge

Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge

Kura ya kIITIFAKI INAWEZA KUTUMIKA AGAINST S.S (6). YA BI.KIROBOTO ILIKUWA HIVYOHIVYO NDANI YA CHAMA!Migiro kawekwa hapo kimkakati na watahakikisha inatumika njia yoyote kumweka kuwa mwenyekiti.
Nataka kufahamu, je hakuna utaratibu huru wenye muongozo katika sheria ya mabadiliko ya katiba kuhusu namna ya kumpata Spika bila kufuata taratibu za kichama?kwamba mtu asihitaji ruhusa ya chama chake kugombea bali yeye mwenyewe akijisikia kugombea ndo agombee!!!!!

Na hawa wabunge wengine wasio na vyama vya siasa watagombea kwa namna gani sasa?
 
Kila nafasi wanataka wao,na ni watu wazima,madaraka wameanza kupata mimi nikiwa sijuia hata a,e,i,o,u.
Akina Migiro,Sitta,Chenge,Lowassa ,Kificho,Makinda na wengineo karibu wote mna miaka zaidi ya 60,kwanini hamtaki kuwaachia uongozi vijana,kwani hii Tanzania ni nyie tu,kwani bila nyie Tanzania itakufa?nyadhifa kibao mnazo mnakuja kukaba hata penalt.Hebu jiulizeni huko Ulaya na Marekani hakuna kiongozi ambaye ni mwanasiasa ambaye kuanzia miaka ya 70 mpaka sasa 2014 baado yupo kwenye siasa au anagombea uongozi,hela mnazo na heshima mnayo lakini baado tu kila sehemu mnataka kuwepo,waachieni na wengine,nao wanajua kuongoza,kama nyie mlianza vijana hadi mumekuwa vibabu basi kuna vijana pia wanaweza kama nyie mlivyoweza
 
Andrew Chenge

Muhariri Michael Bahati

KAMA Tanzania ingekuwa ni nchi inayofuata maadili ya ukweli ya uongozi, Mtemi Andrew Chenge, ama angekuwa nje ya Bunge la Tanzania au, nikitazama mbali zaidi, pengine angekuwa amefungwa jela. Ndiyo sababu nimepatwa na mshituko wa mwaka baada ya kusikia kwamba Mbunge huyu wa Bariadi Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), anatajwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Katiba lililoanza wiki hii. Hakuna shaka kwamba Andrew Chenge ni msomi wa kiwango kizuri tu katika taaluma ya sheria. Nilikuwa nafuatilia Bunge la Tanzania wakati yeye akiwa

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa miaka 10 ya rais Benjamin Mkapa, na bungeni alikuwa mahiri kwa ufafanuzi wa miswada mbalimbali. Wakati nafasi yake ilipochukuliwa na Johnson Mwanyika, niliona wazi Serikali ilikuwa imepata pengo bungeni. Mwanyika mara nyingi alionyesha uso na haiba ya kiongozi asiyejiamini na kitaaluma alionyesha yuko nyuma ya Chenge. Hata Jaji Frederick Werema ambaye anashika nafasi ya AG kwa sasa, naye amekosa ushawishi

kama aliokuwa nao Chenge bungeni. Kimsingi, sina tatizo kabisa na usomi wa mbunge huyu. Tatizo langu kubwa na Chenge ni kwenye uadilifu. Naamini kwamba Katiba ni kitu kilicho kitakatifu na kama kweli Watanzania wanaamini katika utukufu wa Katiba, Chenge hawezi hata kufikiriwa kuwa Spika atayeongoza mchakato huo. Kumpa Chenge uspika wa Bunge hilo ni sawa na kuharibu mchakato mzima wa kutayarisha Katiba mpya. Kwa wasiofahamu vizuri

kuhusu mwanasiasa huyu, Chenge ndiye aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa utawala wa Mkapa. Yeye ndiye aliyeishauri serikali kuingia katika mikataba ya madini ambayo tunailalamikia leo, ununuzi wa rada mbovu na ununuzi wa ndege ya rais ambayo ilipigiwa kelele nchi nzima. Wakati wake, kulikuwa na fununu nyingi zikimtaja kunufaika na kila mikataba mibovu na isiyo na maslahi ambayo serikali yetu iliingia kwenye eneo la rasilimali zetu.

Ukweli uliibuka wazi wakati serikali ya Uingereza ilipojitosa kuchunguza kuhusu sakata la rada. Serikali ya Tanzania, kwa ushauri wa Chenge na ilinunua rada hiyo ya mtumba kwa bei inayokaribia mara nne ya bei yake ya soko. Kwa mujibu wa serikali ya Uingereza, Chenge alikuwa na kesi ya kujibu kwenye mauzo ya rada hiyo kutokana na kukosekana kwa maelezo ya kina ya ununuzi huo. Huo ndio wakati ambao Chenge alipachikwa jina la ‘Mzee wa

Vijisenti’ baada ya kubainika kuwa na zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania katika mojawapo ya akaunti zake za nje ya nchi zilizo katika Visiwa vya Jersey. Hebu tujiulize swali moja; katika hali ya kawaida, inawezekanaje kwa mtumishi wa serikali ya Tanzania kuwa na akaunti yenye thamani ya shilingi bilioni moja na bado akawa jasiri wa kuita kiwango hicho cha fedha vijisenti? Kwa sababu za wazi kabisa, Chenge hajachukuliwa hatua yoyote na serikali ya

Tanzania hadi sasa. Anakula kuku kwa mrija na imefikia wakati sasa watu wanamuona kuwa anafaa kuwa Spika wa Bunge la Katiba?! Itafikia wakati, wengine watasema anafaa hata kuwa Rais wa Tanzania?! Nimesikia majina mengine yakitajwa kuwania wadhifa huo wa Spika na sina matatizo nao isipokuwa jina la huyu Chenge. Kama Chenge atachukua fomu na hatimaye kuwania nafasi hiyo na kisha kushinda, huo utakuwa mwisho wangu wa kufuatilia kutazama Bunge

hilo. Nitatazamaje Bunge hilo na kulifuatilia ilhali anayeliongoza ana tuhuma ambazo hajazikanusha hadi leo? Nani kawahi kumsikia Chenge akisema ni wapi alipozipata fedha zile? Nimekuwa nikisoma kitabu cha Power, Politics and Death cha aliyekuwa Msemaji wa Serikali ya Nigeria, Olusegun Adeniyi, kinachozungumzia maisha ndani ya serikali ya marehemu Rais Umaru Mussa Yar’Adua. Miongoni mwa watu wanaotajwa sana katika kitabu hicho ni waziri wa sheria na mwanasheria mkuu wa Serikali ya Shirikisho la Nigeria, Michael Kaase Aondoakaa. Huyu bwana alikuwa

mwanasheria mahiri sana lakini tatizo lake alikuwa kibaraka wa mafisadi. Huyu ndiye aliyefanikisha kuachiwa huru kwa Gavana Fisadi wa Jimbo la Delta, James Ibori. Si huyo pekee lakini enzi yake bwana huyu Aondoakaa, Nigeria iliingia katika mikataba tata na kufanya maamuzi tata kuhusu ufisadi na mafisadi. Ni huyuhuyu ndiye aliyefanya kazi ya Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya Nigeria, Nuhu Ribadu, iote nyasi na akaishi maisha magumu kwa sababu ya kutaka kupambana na rushwa. Kwangu, sioni tofauti kubwa kati ya Chenge na Aondoakaa. Majirani zetu

hawatatuelewa endapo watamsikia Chenge akiwa ndiye Spika wa Bunge la Katiba. Serikali ya Uingereza itatushangaa endapo tutamchagua Chenge kwenye shughuli hii. Kazi ya kutengeneza Rasimu ya Katiba ilifanywa na watu ambao wana sifa ya usafi kwenye jamii ya Watanzania. Ndiyo maana Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Joseph Warioba, akiwa anasikindikizwa na watu kama Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Palamagamba Kabudi, Dk. Salim Ahmed Salim na

wengineo. Ombi langu kwa wajumbe wa Bunge la Katiba ni kwamba wasiharibu kazi hii ya kukumbukwa ya tume hii kwa kumpa Chenge fursa ya kutia mguu wake. Kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyopata kusema katika siku za nyuma; “Katiba ni Kitu Kitakatifu na Hakitakiwi Kuchezewachezewa.” - See more at:

Raia Mwema - Spika Chenge, tumekwisha
 
Methali: KILA PENYE ZANZIBAR PANA TANGANYIKA - Aidha kiwaziwazi au kiwiziwizi.
 
Hiyo nafasi wampe mtu ambaye hana chama, hii habari ya Chenge, Sita, Chikawe sidhani kama watatutendea haki katika kuliongoza bunge, kwani busara zao zitakuwa za kichama zaidi!

[Q

UOTE=Kakke;8791228]
Andrew Chenge

Muhariri Michael Bahati

KAMA Tanzania ingekuwa ni nchi inayofuata maadili ya ukweli ya uongozi, Mtemi Andrew Chenge, ama angekuwa nje ya Bunge la Tanzania au, nikitazama mbali zaidi, pengine angekuwa amefungwa jela. Ndiyo sababu nimepatwa na mshituko wa mwaka baada ya kusikia kwamba Mbunge huyu wa Bariadi Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), anatajwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Katiba lililoanza wiki hii. Hakuna shaka kwamba Andrew Chenge ni msomi wa kiwango kizuri tu katika taaluma ya sheria. Nilikuwa nafuatilia Bunge la Tanzania wakati yeye akiwa

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa miaka 10 ya rais Benjamin Mkapa, na bungeni alikuwa mahiri kwa ufafanuzi wa miswada mbalimbali. Wakati nafasi yake ilipochukuliwa na Johnson Mwanyika, niliona wazi Serikali ilikuwa imepata pengo bungeni. Mwanyika mara nyingi alionyesha uso na haiba ya kiongozi asiyejiamini na kitaaluma alionyesha yuko nyuma ya Chenge. Hata Jaji Frederick Werema ambaye anashika nafasi ya AG kwa sasa, naye amekosa ushawishi

kama aliokuwa nao Chenge bungeni. Kimsingi, sina tatizo kabisa na usomi wa mbunge huyu. Tatizo langu kubwa na Chenge ni kwenye uadilifu. Naamini kwamba Katiba ni kitu kilicho kitakatifu na kama kweli Watanzania wanaamini katika utukufu wa Katiba, Chenge hawezi hata kufikiriwa kuwa Spika atayeongoza mchakato huo. Kumpa Chenge uspika wa Bunge hilo ni sawa na kuharibu mchakato mzima wa kutayarisha Katiba mpya. Kwa wasiofahamu vizuri

kuhusu mwanasiasa huyu, Chenge ndiye aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa utawala wa Mkapa. Yeye ndiye aliyeishauri serikali kuingia katika mikataba ya madini ambayo tunailalamikia leo, ununuzi wa rada mbovu na ununuzi wa ndege ya rais ambayo ilipigiwa kelele nchi nzima. Wakati wake, kulikuwa na fununu nyingi zikimtaja kunufaika na kila mikataba mibovu na isiyo na maslahi ambayo serikali yetu iliingia kwenye eneo la rasilimali zetu.

Ukweli uliibuka wazi wakati serikali ya Uingereza ilipojitosa kuchunguza kuhusu sakata la rada. Serikali ya Tanzania, kwa ushauri wa Chenge na ilinunua rada hiyo ya mtumba kwa bei inayokaribia mara nne ya bei yake ya soko. Kwa mujibu wa serikali ya Uingereza, Chenge alikuwa na kesi ya kujibu kwenye mauzo ya rada hiyo kutokana na kukosekana kwa maelezo ya kina ya ununuzi huo. Huo ndio wakati ambao Chenge alipachikwa jina la ‘Mzee wa

Vijisenti' baada ya kubainika kuwa na zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania katika mojawapo ya akaunti zake za nje ya nchi zilizo katika Visiwa vya Jersey. Hebu tujiulize swali moja; katika hali ya kawaida, inawezekanaje kwa mtumishi wa serikali ya Tanzania kuwa na akaunti yenye thamani ya shilingi bilioni moja na bado akawa jasiri wa kuita kiwango hicho cha fedha vijisenti? Kwa sababu za wazi kabisa, Chenge hajachukuliwa hatua yoyote na serikali ya

Tanzania hadi sasa. Anakula kuku kwa mrija na imefikia wakati sasa watu wanamuona kuwa anafaa kuwa Spika wa Bunge la Katiba?! Itafikia wakati, wengine watasema anafaa hata kuwa Rais wa Tanzania?! Nimesikia majina mengine yakitajwa kuwania wadhifa huo wa Spika na sina matatizo nao isipokuwa jina la huyu Chenge. Kama Chenge atachukua fomu na hatimaye kuwania nafasi hiyo na kisha kushinda, huo utakuwa mwisho wangu wa kufuatilia kutazama Bunge

hilo. Nitatazamaje Bunge hilo na kulifuatilia ilhali anayeliongoza ana tuhuma ambazo hajazikanusha hadi leo? Nani kawahi kumsikia Chenge akisema ni wapi alipozipata fedha zile? Nimekuwa nikisoma kitabu cha Power, Politics and Death cha aliyekuwa Msemaji wa Serikali ya Nigeria, Olusegun Adeniyi, kinachozungumzia maisha ndani ya serikali ya marehemu Rais Umaru Mussa Yar'Adua. Miongoni mwa watu wanaotajwa sana katika kitabu hicho ni waziri wa sheria na mwanasheria mkuu wa Serikali ya Shirikisho la Nigeria, Michael Kaase Aondoakaa. Huyu bwana alikuwa

mwanasheria mahiri sana lakini tatizo lake alikuwa kibaraka wa mafisadi. Huyu ndiye aliyefanikisha kuachiwa huru kwa Gavana Fisadi wa Jimbo la Delta, James Ibori. Si huyo pekee lakini enzi yake bwana huyu Aondoakaa, Nigeria iliingia katika mikataba tata na kufanya maamuzi tata kuhusu ufisadi na mafisadi. Ni huyuhuyu ndiye aliyefanya kazi ya Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya Nigeria, Nuhu Ribadu, iote nyasi na akaishi maisha magumu kwa sababu ya kutaka kupambana na rushwa. Kwangu, sioni tofauti kubwa kati ya Chenge na Aondoakaa. Majirani zetu

hawatatuelewa endapo watamsikia Chenge akiwa ndiye Spika wa Bunge la Katiba. Serikali ya Uingereza itatushangaa endapo tutamchagua Chenge kwenye shughuli hii. Kazi ya kutengeneza Rasimu ya Katiba ilifanywa na watu ambao wana sifa ya usafi kwenye jamii ya Watanzania. Ndiyo maana Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Joseph Warioba, akiwa anasikindikizwa na watu kama Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Palamagamba Kabudi, Dk. Salim Ahmed Salim na

wengineo. Ombi langu kwa wajumbe wa Bunge la Katiba ni kwamba wasiharibu kazi hii ya kukumbukwa ya tume hii kwa kumpa Chenge fursa ya kutia mguu wake. Kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyopata kusema katika siku za nyuma; "Katiba ni Kitu Kitakatifu na Hakitakiwi Kuchezewachezewa." - See more at:

Raia Mwema - Spika Chenge, tumekwisha[/QUOTE]
 
ni kweli mkiimpa Chenge uenyekiti tumekwisha na sidhani km itapatikana katiba yenye kukithi haki ya wazalendo.
 
Hiyo ndio Tanzania Bwana. Mtu bila aibu anathubutu eti kugombea kuwa spika wa bunge letu la katiba, mtu ambaye si safi hata kidogo. Na chama chama chake kilimuweka kwenye kamati ya maadili. Kwa maadili gani aliyo nayo huyo Chenge?

Tiba
 
wote hao waliobakia sio watu wazuri, Sitta yule tunayemfahamu kwa misimamo siye tutakaye mshuhudia tena, alionyesha wazi kushabikia serikali 3, na huyo mama ni ndiye tangu mwazo alikuwa anasuka mikakati ya kuhujumu mchakato wa katiba
Hauko Sahihi ,Sita ni waziri wa kwanza kupinga serikali tatu,tokea ile rasimu 1,yeye ni mtu wa kwanza kupinga hadharani....ila hao wote majanga,nina wasiwasi atapewa mama Migiro
#TeamSerikali3 #
 
Hiyo ndio Tanzania Bwana. Mtu bila aibu anathubutu eti kugombea kuwa spika wa bunge letu la katiba, mtu ambaye si safi hata kidogo. Na chama chama chake kilimuweka kwenye kamati ya maadili. Kwa maadili gani aliyo nayo huyo Chenge?

Tiba

Mbona chama chao kinakataza watu wenye maadili kushika nafasi za uongozi?Ndiyo maana kwao wala rushwa,mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma kwenye chama chao ndiyo wenye nyota na huwezi kuwagusa.Kumbuka kuvua GAMBA kama liliweza kutoka.Usikasirike ndiyo Tanzania yetu.
 
Chenge ni worse,lakini mtu yoyote aliekuwa kwenye system muda mrefu hafai ikiwa ni pamoja na huyo Siita.
 
Huu ni mtihani kwa vyama vya upinzani ,kwani inatakiwa wamuumbue kuanzia sasa na kama haondolewi basi visishiriki kwenye bunge la katiba na wawashawishi na wengine wasusie bunge hilo la katiba kwani heshima ni kitu cha bure ,huyu Chenge si ndie huyuhuyu alieuwa kwa gari ?
 
Kwa magamba lolote linawezekana.
Hapa si pahala pa mchezo nikimaanisha huko kwenye bunge, hakuna magamba wala magome ,bunge hili si la kucheka na CCM kwani halihusiani na chama chaowala chama kingine ,hivyo na wao wanatakiwa wawe na heshima la si hivyo patachimbika.
 
pia mjue huyu ni mwanamtandao wa richmonduli,kuna vigazeti njaa vinambeba sana huyu fisadi,siku ile ya uchaguzi wa muda waliweka picha yake front page na kuandika Chenge moja kwa moja uenyekiti,hizi njaa ni matatizo matupu,
 
ukiona hivyo nchi imeshakufa siku nyingi sana imebaki maziko tu, huyu huyu change naye anatajwa kwa swala nyeti na seriouos kama hili??? kweli CCM mmemfanya nyinyi mtanganyika????
 
Back
Top Bottom