Spika Dkt. Tulia aahirisha Bunge kutokana na hililafu kwenye vipaza sauti

Spika Dkt. Tulia aahirisha Bunge kutokana na hililafu kwenye vipaza sauti

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia yanayojiri kwenye Mkutano wa 13, Kikao cha 1, leo Oktoba 31, 2023.


Mbunge mpya wa Mbarali, Bahati Ndingo ameapa leo baada ya kushinda nafasi hiyo kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba 19, 2023.

Uchaguzi mdogo wa ubunge Mbarali umefanyika baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Francis Mtega (CCM), kilichotokea Julai mosi, 2023 kwa ajali ya kugongwa na trekta dogo (power tiller), kisha kuzikwa Ludewa mkoani Njombe

Ndingo ameapishwa leo Jumanne Oktoba 31, 2023 katika kikao cha kwanza cha Bunge katika Mkutano wa 13.

Kabla ya uchaguzi huo, Ndingo alikuwa ni mbunge wa viti maalumu na alilazimika kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wake.

Aidha, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, ameahirisha kikao cha Bunge kwa muda wa Nusu Saa baada ya kutokea kwa hitilafu kwenye vipaza sauti vyake.
 
Bora ni fuatilie maigizo kuliko kuangalia upuuzi ambao hauna faida zaidi ya hasara kwa nchi
 
Back
Top Bottom