Spika Dkt. Tulia Ackson: Mbeya Watanikumbuka Kwa Ujenzi wa Barabara Njia 4

Spika Dkt. Tulia Ackson: Mbeya Watanikumbuka Kwa Ujenzi wa Barabara Njia 4

Spika wa Bunge mh.Dk.Tulia Ackson Mwansasu Akihojiwa na Clouds kwamba anaacha alama gani Mbeya amejibu kwamba ikitokea hajaendelea kuwa mbunge basi Wana Mbeya watamkumbuka Kwa ujenzi wa Barabara ya Njia 4 Kwa miaka yake hii mi 5 ambayo amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini.

Japo jambo hili ndio linaonekana Kwa haraka lakini Mimi nitamkumbuka Kwa mambo Makuu mengine ma 3 ukiacha Hilo la Barabara ya Nsalaga-Ifisi njia 4. Mambo hayo ni ;
1)-Ujanzi wa Jengo la wodi ya kina Mama pale Meta la gorofa 6 ambalo limeipa hadhi Hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya

2)-Ameacha ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji wa kutoka chanzo Cha mto kiwira Wilaya ya Rungwe Hadi Jijini Mbeya na Mbalizi Kwa Zaidi ya Bilioni 160.

3)-Ukamilishaji wa Uwanja wa ndege wa Songwe(Anapigania uitwe Mbeya),ikumbukwe Toka Mwandosya ameasisi ujenzi wake awamu ya Mkapa ,uwanja Imekamilika mwaka huu 2023 baada ya Kubomoa na kuijenga Upya runwaya zake,kufunga taa na jengo la Abiria.

4)-Ujenzi wa Barabara ya Igawa-Uyole-Songwe-Tunduma na Uyole-Mbalizi Bypass Kwa njia 4 Kwa Utaratibu wa EPC+F

5)-Mradi wa Tactic una components za Barabara za mtaani km 20,Masoko 3,Stand 3(Soon unaanza).

Hata kama by 2025 Miradi itakuwa haijakamilika inaendelea ila ni vitu ambavyo vinaonekana unaweza waoneaja watu wakaelewa.

----
"Nikisema Mbeya mjini watanikumbuka kwa jambo gani ni kwamba ujenzi wa barabara ya njia nne umeshaanza maana yake ile barabara itakapokamilika au hata kama haikukamilika mimi nikiwa mbunge imeshaanza hivyo siku zote watajua kwamba ilianza kujengwa wakati Mbunge akiwa fulani.

Lakini pia tunazipigania barabara za mitaa, lami zimeshaanza hapa na pale lakini ni dhahiri nchi ni kubwa hii na fedha zote haziwezi kwenda kufanya kazi Mbeya pekee kwahiyo itatuchukua muda ila tumeshaanza kazi na Wananchi wanaona"

View: https://twitter.com/CloudsMediaLive/status/1701840872604643605?t=PfAYhz-xe9rsq-mNS-LWxA&s=19

My Take
Sugu wa Chadema amekuwa Mbunge miaka 15 hana hata kitu Kimoja Cha maana anaweza onesha Wananchi Ili kuja kumkumbuka.

Hizo projects siyo yeye kazisukuma. Kwanza nyingi ziko nje ya Jimbo lake. Yeye eneo lake linaanzia Uyole na na kuishia Iwambi kwa mijibu wa Tanzam road. Kuelekea Chunya linaishia unapoanza msitu wa Kawetere na kwa kuelekea Rungwe linaishia Igawilo.

Mradi wa Barabara ya Km 160 za Igawa- Tunduma ni mradi mkubwa wa Serikali wala siyo push ya Tulia.

AnachowezTulia Ackson ni uchafuzi tu Jiji la Mbeya kwa kujaza Bajaj nyingi kuliko mahitaji ya Jiji.
 
Chama kinaweza kuwa mizinguo, lakini hamuwezi kupata muwakilishi bora zaidi ya anayekuwa spika. Mwingine yoyote ni kushuka chini.
Kuwa na Spika kutoka kwenye Jimbo hakulisaidii jimbo chochote. Angalia Urambo, Njombe na Kongwa kama kuna maendeleo ya kuzidi majimbo/ wilaya zingine.

Ni akili mburura ndiyo inashangilia kuona Spika anatoka wilaya/ jimbo lake. Mbunge anapaswa kuwa back bench kupush agenda
 
Haifuti hiyo legacy,ni zamu ya Sugu kuonesha amefanya nini Mbeya Kwa miaka 15.

Kwani wewe unachagua Mbunge Kwa Ajili gani?

Mwisho kati ya wewe kiasi,boga Sugu na Msomi Dr.Tulia nani hajitambui?
Mbeya hawawezi kumchagua tena Sugu. Hilo sahau kabisa. Mbeya siyo majimbo ya wajinga kubakia wamekariri mbunge. Unapewa miaka 5 na ukiwa na bahati 5 mingine.

Kama CHADEMA wanataka wapoteze jimbo basi wamuweke Sugu, tutarudi hapa 2025 kuja kuisoma hii post
 
Kuwa na Spika kutoka kwenye Jimbo hakukisaidii jimbo chochote. Angalia Urambo, Njombe na Kongwa kama kuna maendeleo ya kuzidi majimbo/ wilaya zingine.

Ni akili mburura ndiyo inashangilia kuona Spika anatoka wilaya/ jimbo lake. Mbunge anapaswa kuwa back bench kupush agenda
Hawa ndo watanzania sasa
 
Hizo projects siyo yeye kazisukuma. Kwanza nyingi ziko nje ya Jimbo lake. Yeye eneo lake linaanzia Uyole na na kuishia Iwambi kwa mijibu wa Tanzam road. Kuelekea Chunya linaishia unapoanza msitu wa Kawetere na kwa kuelekea Rungwe linaishia Igawilo.

Mradi wa Barabara ya Km 160 za Igawa- Tunduma ni mradi mkubwa wa Serikali wala siyo push ya Tulia.

AnachowezTulia Ackson ni uchafuzi tu Jiji la Mbeya kwa kujaza Bajaj nyingi kuliko mahitaji ya Jiji.
Kabla ya mapovu ilitakiwa uoneshe alichofanya Sugu Kwa miaka 15 alivyokuwa mbunge wa Mbeya.

Mwisho ukisema sio yeye hajaanza Leo Wala Jana ku push hiyo miradi na Serikali ingeweza kuisubilisha ila Kwa kelele na heshima yake kama Spika Serikali imelazimika kuanza Ujenzi wa hiyo miradi.

Kwa taarifa Yako tuu Kambi ya mradi wa Maji Iko Forest Mpya Jirani na Ofisi ya TFS Kanda ,Sasa hapo sijui ni Jimbo la nani.

Tulia ataonesha hiyo miradi,hao wengine wataonesha nini?
 
Mbeya hawawezi kumchagua tena Sugu. Hilo sahau kabisa. Mbeya siyo majimbo ya wajinga kubakia wamekariri mbunge. Unapewa miaka 5 na ukiwa na bahati 5 mingine.

Kama CHADEMA wanataka wapoteze jimbo basi wamuweke Sugu, tutarudi hapa 2025 kuja kuisoma hii post
Watamuweka nani hao Chadema? Mwambukusi au? Sugu atakubari?
 
Huyu mpuuzi kweli kweli, miradi yote hiyo ni ya serikali na ilipangwa kutekelezwa muda mrefu sana.
Huo mda mrefu ndio haikutekelezwa Bali imetekeleza Sasa hivi awamu ya Spika Kwa heshima yake na amekuwa anapigia kelele mara nyingi.

Kama ni kupangwa aisee imepangwa miradi Mingi sana ila hakuna kinachoendelea

Kwa hiyo mapovu hayana Cha kukusaidia,ni zamu ya Sugu na Chadema kuonesha Wakifanya nini Mbeya Kwa miaka 15?
 
Kuwa na Spika kutoka kwenye Jimbo hakukisaidii jimbo chochote. Angalia Urambo, Njombe na Kongwa kama kuna maendeleo ya kuzidi majimbo/ wilaya zingine.

Ni akili mburura ndiyo inashangilia kuona Spika anatoka wilaya/ jimbo lake. Mbunge anapaswa kuwa back bench kupush agenda
Kama kuwa na bosi wa wabunge kama mbunge wenu hakuna faida basi kuwa na mbunge yeyote hakuna faida. Pia angalia na akili za spika. Yule wa Urambo badala ya kufanya jambo la maana akaenda kujenga ofisi yake Urambo!!?
 
Kabla ya mapovu ilitakiwa uoneshe alichofanya Sugu Kwa miaka 15 alivyokuwa mbunge wa Mbeya.

Mwisho ukisema sio yeye hajaanza Leo Wala Jana ku push hiyo miradi na Serikali ingeweza kuisubilisha ila Kwa kelele na heshima yake kama Spika Serikali imelazimika kuanza Ujenzi wa hiyo miradi.

Kwa taarifa Yako tuu Kambi ya mradi wa Maji Iko Forest Mpya Jirani na Ofisi ya TFS Kanda ,Sasa hapo sijui ni Jimbo la nani.

Tulia ataonesha hiyo miradi,hao wengine wataonesha nini?
Sugu amekua mbunge kwa miaka 15 we jamaa ni muongo sana na mzushi wa kiwango cha juu
 
Haifuti hiyo legacy,ni zamu ya Sugu kuonesha amefanya nini Mbeya Kwa miaka 15.

Kwani wewe unachagua Mbunge Kwa Ajili gani?

Mwisho kati ya wewe kiasi,boga Sugu na Msomi Dr.Tulia nani hajitambui?
Hivi kumbe sugu alikuwa mbunge for 15 years!! Na bado hajaridhika na hakuna kitu alifanya!! Then utasikia miccm ni walafi wa madaraka, kumbe wote wale wale🙆🙆
 
Back
Top Bottom