Spika Dkt. Tulia Ackson: Mbeya Watanikumbuka Kwa Ujenzi wa Barabara Njia 4

Hizo projects siyo yeye kazisukuma. Kwanza nyingi ziko nje ya Jimbo lake. Yeye eneo lake linaanzia Uyole na na kuishia Iwambi kwa mijibu wa Tanzam road. Kuelekea Chunya linaishia unapoanza msitu wa Kawetere na kwa kuelekea Rungwe linaishia Igawilo.

Mradi wa Barabara ya Km 160 za Igawa- Tunduma ni mradi mkubwa wa Serikali wala siyo push ya Tulia.

AnachowezTulia Ackson ni uchafuzi tu Jiji la Mbeya kwa kujaza Bajaj nyingi kuliko mahitaji ya Jiji.
 
Chama kinaweza kuwa mizinguo, lakini hamuwezi kupata muwakilishi bora zaidi ya anayekuwa spika. Mwingine yoyote ni kushuka chini.
Kuwa na Spika kutoka kwenye Jimbo hakulisaidii jimbo chochote. Angalia Urambo, Njombe na Kongwa kama kuna maendeleo ya kuzidi majimbo/ wilaya zingine.

Ni akili mburura ndiyo inashangilia kuona Spika anatoka wilaya/ jimbo lake. Mbunge anapaswa kuwa back bench kupush agenda
 
Haifuti hiyo legacy,ni zamu ya Sugu kuonesha amefanya nini Mbeya Kwa miaka 15.

Kwani wewe unachagua Mbunge Kwa Ajili gani?

Mwisho kati ya wewe kiasi,boga Sugu na Msomi Dr.Tulia nani hajitambui?
Mbeya hawawezi kumchagua tena Sugu. Hilo sahau kabisa. Mbeya siyo majimbo ya wajinga kubakia wamekariri mbunge. Unapewa miaka 5 na ukiwa na bahati 5 mingine.

Kama CHADEMA wanataka wapoteze jimbo basi wamuweke Sugu, tutarudi hapa 2025 kuja kuisoma hii post
 
Hawa ndo watanzania sasa
 
Kabla ya mapovu ilitakiwa uoneshe alichofanya Sugu Kwa miaka 15 alivyokuwa mbunge wa Mbeya.

Mwisho ukisema sio yeye hajaanza Leo Wala Jana ku push hiyo miradi na Serikali ingeweza kuisubilisha ila Kwa kelele na heshima yake kama Spika Serikali imelazimika kuanza Ujenzi wa hiyo miradi.

Kwa taarifa Yako tuu Kambi ya mradi wa Maji Iko Forest Mpya Jirani na Ofisi ya TFS Kanda ,Sasa hapo sijui ni Jimbo la nani.

Tulia ataonesha hiyo miradi,hao wengine wataonesha nini?
 
Watamuweka nani hao Chadema? Mwambukusi au? Sugu atakubari?
 
Huyu mpuuzi kweli kweli, miradi yote hiyo ni ya serikali na ilipangwa kutekelezwa muda mrefu sana.
Huo mda mrefu ndio haikutekelezwa Bali imetekeleza Sasa hivi awamu ya Spika Kwa heshima yake na amekuwa anapigia kelele mara nyingi.

Kama ni kupangwa aisee imepangwa miradi Mingi sana ila hakuna kinachoendelea

Kwa hiyo mapovu hayana Cha kukusaidia,ni zamu ya Sugu na Chadema kuonesha Wakifanya nini Mbeya Kwa miaka 15?
 
Kama kuwa na bosi wa wabunge kama mbunge wenu hakuna faida basi kuwa na mbunge yeyote hakuna faida. Pia angalia na akili za spika. Yule wa Urambo badala ya kufanya jambo la maana akaenda kujenga ofisi yake Urambo!!?
 
Sugu amekua mbunge kwa miaka 15 we jamaa ni muongo sana na mzushi wa kiwango cha juu
 
Sawa miaka 10 amefanya nini? Si utaje?
We ulisema miaka 15 siwez endelea ku-argue na watu ambao ni wazushi na waongo
Ndo maana walitaka kukupiga ban permanent sikuelewa ila leo ndo nimeelewa kwanin watu wengi walikua hawako upande wako
 
Haifuti hiyo legacy,ni zamu ya Sugu kuonesha amefanya nini Mbeya Kwa miaka 15.

Kwani wewe unachagua Mbunge Kwa Ajili gani?

Mwisho kati ya wewe kiasi,boga Sugu na Msomi Dr.Tulia nani hajitambui?
Hivi kumbe sugu alikuwa mbunge for 15 years!! Na bado hajaridhika na hakuna kitu alifanya!! Then utasikia miccm ni walafi wa madaraka, kumbe wote wale wale🙆🙆
 
Hivi kumbe sugu alikuwa mbunge for 15 years!! Na bado hajaridhika na hakuna kitu alifanya!! Then utasikia miccm ni walafi wa madaraka, kumbe wote wale wale🙆🙆
Tueleze for 10 years anataka tena Kwa lipi alilofanya?
 
We ulisema miaka 15 siwez endelea ku-argue na watu ambao ni wazushi na waongo
Ndo maana walitaka kukupiga ban permanent sikuelewa ila leo ndo nimeelewa kwanin watu wengi walikua hawako upande wako
Huna hoja na huna Cha kuonesha kiufupi Sugu alikuwa Mzigo Kwa Wana Mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…