Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi

Kuna watu wengi Sana humu nawaheshimu Pascal Mayalla mmoja wapo halafu Kuna Mtu anaitwa barafu na wengine wengi.

Ila Kaka yangu Pascal Mayalla Mimi kwenye hili saga najiuliza maswali mengi sana , likiwepo na hili la Mbunge kutoka gerezani usiku na asubuhi kwenda kuapishwa, tena sio bungeni Kwa nini? Kuna nini?

Halafu mbona spika katangaza kuwatambua bila amri ya Mahakama? Yani yeye katangaza asubuhi zuio la Mahakama limetoka mchana bado unawatupia mzigo CHADEMA?

Katiba inasema , kila mtu ana Uhuru WA kutoa maoni yake Ila asivunje Sheria.

Naheshimu mawazo yako, Ila sikubaliani nayo.
 
Mkuu Nguruvi3 nimependa uandishi wa hoja zako,umeelezea kwa lugha nyepesi na yenye kueleweka saana..

Kwenye hili sakata la COVID 19 kuna makosa pande zote 3,chama,wabunge na spika.

Lakini hoja kuu ya pascal ni chanzo cha tatizo...na hili thread yake kama nimemuelewa ka base kwenye kuishauri Chadema,labda baadae atakuja na thread ya kumshauri spika...hivyo kwa sasa tujadilini hoja yake kuu.
 
Hapa umemaliza kila kitu, heshima kwako Mkuu.
 
Mkuu kama unamsoma Pascal Mayalla hoja yake ni utetezi kwa COVID19 kwa namna yote
Ujenzi wake wa hoja unaruka ruka tu, na nitakupa mifano

1. Anatuhumu Chadema kukiuka katiba. Tunamuuliza atufafanulie ni wapi imekiukwa! hajaweza kutueleza hata aya moja lakini anasisitiza imekiukwa.

2. Anasema CC ya Chadema ni kangaroo court! tunamuuliza kosa walilofanya ni lipi, hana jibu

3. Anasema barua ya NEC ni halali. Tunamuuliza COVID19 walipewa nani, hana jibu

4. Anasema Chadema waende kuripoti Polisi. Tunamuuliza zile kesi za masanduku ya kura walizoripoti Polisi zimeishia wapi? Hana jibu anataka waende tu

5. Anasema Halima Mdee ni mwenyekiti wa Bawacha, CC si mamlaka yeke ya nidhamu. Tunamuuliza kwani amefukuzwa Uenyekiti au Uanachama? Hana jibu

6. Anasema Spika aliambiwa na COVID wanaenda mahakamani! Tukamuuliza angeambiwa na Chadema kwamba wamefukuzwa angekubali bila barua ya kitaasisi? Hana jibu anasema majungu ya Spika Tulia na COVID19 wakati wanasukana ni muhimu kuliko Barua ya mahakama

7. Tunamuuliza, hivi kesi ya wanachama na chama chao mawakili wa serikali wanaingiaje? Pasco haana jibu anasema kwasababu wameonewa!

8. Tukamuuliza Nusrat Hanje katolewa usiku bila amri ya mahakama, nani kutoka Chadema alitoa amri hiyo? Hana jibu. Nani alimpelekea fomu magereza? Pasco hana jibu

Mimi sina tatizo na hoja zake na napenda sana mijadala ya namna hii, nina tatizo na biasness

Hana anaposhika, anatafuta hoja ya siku! kwamba kumekucha hii hoja inaweza kubadili mwelekeo basi anaitumbukiza.

Ni nadra sana nasema haya lakini anapozungumza kama Mwanasheria na Mwandishi, hapana! ni mwenzetu tumsaidie.
 


Yaani kwa mwana sheria kutetea uvunjifu wa sheria kwasababu tu ya ukada ina shusha sana credibility yako
 
Ushauri kwa Chadema

Naomba chadema wajitoe katika kesi ya Halima mdee wasiweke wakili yeyote na waendelee kukijenga chama na join chadema policy
 
Kesi iliyopo mahakamani si ya kisiasa but waliofungua kesi wanaona wamenyimwa HAKI yao, mahakama hazisikilizi kesi za kisiasa
Tusiyumbishwe na maneno, wamenyimwa haki yao ya kisiasa. Huwezi kupeleka kesi mahakamani ikihitaji haki yako ya kuwa mbunge halali halafu usiseme hawagusi mambo ya siasa. Lazima wabalance pande zote, sheria za vyama zinasemaje na uhalali / ubatili uko wapi!
 
Ushauri wa mchawi ?
Si upeleke kwenu huku uliishakataliwa. Una roho ngumu kama yule mwandishi nguli anaedai alipata A ya sheria.
 
Nawewe utumie akili basi...

Chadema haijafukuza wabunge Bali imefukuza wanachama wake....

Chadema haikuwahi kuthibitisha kuwa na wabunge viti maalum Bungeni hivyo hao sio wabunge wa Chadema..

Imedili na hao kina Halima kama wanachama Wasaliti na wahujumu na wala sio wabunge.

Chadema ni Mpango wa Mungu....utaelewa siku Moja...
 
Mkuu pasco hoja zinajibiwa kwa hoja.
Mkuu Nguruvi3, naunga mkono hoja, hoja zijibiwe kwa hoja. Asante kwa kujibu hoja kwa hoja, japo na wewe kuna maeneo unajibu hoja kwa hoja na kuna maeneo unaleta viroja. Japo sisi wana jf, as if members, we are all equal, and we have an equal status as jf member, lakini kupitia michango yetu humu, tumetoka kufahamiana na kuheshimiana hivyo wewe ni miongoni mwa well respected members kwenye ratings zangu, usiiharibu heshima hii kwa kuchanganya hoja na viroja!.
Nimeshangaa umetangulizi suala la mahaba ya wasiokubaliana nawe kwa Chadema! huo ni ufinyu au uhaba wa hoja. Hakuna uchama hapa na wengine hatujui hivyo vyama, lakini tukae kimya kama mazuzu tukinajisiwa akili na akina Tulia
Matumizi ya neno najisi sio hoja ni kiroja. Kwa vile nimesema nimemuangalia kwa macho yangu na kumsikia Spika wa Bunge Dr. Tulia Akson, kwa masikio yangu, mengi uliyoyaandika kumhusu Dr. Tulia na uamuzi wake ni viroja, hivyo naasume hukumsikia, hivyo nimejitolea kukuletea Spika wa Bunge Mhe. Dr. Tulia Akson Mwansasu, muangalie kwa macho yako, na kumsikiliza kwa masikio yako, kisha unirudie kuwa kama ungesikiliza kabla, kuna hoja usinge zileta na kuna viroja visingekuwepo. Ila pia licha ya kuona na kusikia, bado nitaendelea kufafanua kwasababu kuna wenzetu wengi wana macho lakini hawaoni na wana masikio lakini hawasikii
Umeandika mambo mengi na kuficha hoja muhimu kwa bahati mbaya wewe ni mwanasheria tena mwanafunzi wa Tulia Akson PhD na kuna kila sababu ya kuwa na shaka na hilo darasa, sorry!.
No one is perfect, ruksa kuwa na mashaka na LL.B ya UDSM, ila kwa wanafunzi walitaka kusomea sheria, getting UDSM LL.B admission is not a joke!. LL.B za vyuo vingine vyote Tanzania, LL.B zao ni 3-year, UDSM ni 4-years. Dr. Tulia ametoka na Div 1 ya 7 points O-level na 3 points A-level, akapiga GPA ya 4.4 hivyo she was retained. Hivyo kumdoubt mtu kama huyu ni kiroja!. Mimi kuni doubt ni sawa kwasababu japo LL.B yangu ni Hons,lakini sijawahi ku practice, kwa wengi wasio jua fani ya sheria, wako carried out na court room legal drama za mawakili wakiamini mwanasheria machachari ni kwenye litigations, hawajui kuwa kuna wanasheria kibao hawana time kabisa na litigations, wao wamejikita tuu kwenye legal opinion.
Hii point ina maana na umuhimu gani? Hoja ni COVID19 wameteuliwaje na nani na kikao gani.
Hata kama wameteuliwa na 'kigogo' , je huo ndio utaratibu wa katiba unayosema inavunjwa?.
Time ya Uchaguzi NEC, inapokiandikia chama kuomba majina, na kikapewa majina hayo 18. Kwa NEC issue imeishia hapo. Hao 18 wamepatikanaje, sio issue ya NEC, walitaka majina, wameyapata wakawapa uteuzi na kumpa Spika. Kwa NEC ni majina halali, yamepelekwa kihalali Bungeni, wameapishwa ni Wabunge halali kabisa. Kama kuna issue yoyote ya forgery, then it's an internal matters za Chadema, it's up to Chadema to raise them and prove, NEC wangebatilisha batilisha uteuzi wao siku nyingi, ndio maana nimesema Chadema must learn to do things right.
Naunga mkono hoja. Pia Msikilize Dr. Tulia hili limejibiwa
Si kweli unachosema sana ni uongo!.
Duh...!
Wanachama wa CUF walipoteza Ubunge mara moja
Tundu Lissu kesi yake haijaisha na si mbunge kuna ''replacement'' tayari
It's timings. Msikilize Dr Tulia
Sheria za Bunge ni zipi? Za Ndugai au za Tulia Akson PhD!.
Sheria ni za nchi, sio za mtu na hiki ni kiroja!.
Lakini pia unajichanganya, tambua kwamba kubaki na ubunge ni amri ya mahakama
Kumbuka hii hoja halafu utaona tatizo hapa chini
Sijajichanganya popote ila utakuwa wewe
Uongo uongo uongo! mkubwa. Mnadhalilisha taaluma ya sheria wewe na mwalimu wako Tulia Akson PhD.
Hiki ni kiroja!.
Huwezi kwenda Bungeni na kusema umechaguliwa na NEC na Bunge likakuruhusu kuingia kwasababu umelitaarifu kwa barua . Huo si utaratibu lazima uwe na nyaraka za NEC na vitambulisho vingine.
You are right, Barua ya NEC ya uteuzi wa wabunge hao ni legit credentials bonafide genuine certificates!
Huwezi kumwandikia barua Spika eti unakwenda mahakamani na Spika huyo akakubali, huu niu upuuzi mkubwa. Spika anafanyia kazi taarifa za kiofisi si vijibarua visivyo na ushahidi
Hiki ni kiroja, Msikilize Dr. Tulia.
Spika Tulia Akson PhD alipaswa kuomba apewe barua ya mahakama kwamba lipo shauri, siyo barua za ''mapenzi' tu kutoka COVID.
Kiroja, Msikilize Dr Tulia.
Hili halihitaji kujua sheria linahitaji weledi tu na nakuhakikishia watu wanaojua wanamuona Tulia Akson PhD mtu wa ajabu sana! hakuna kitu pale , empty !
Kiroja!.
Nimekupa scenario pale juu, pia utambue suala la Tundu Lissu lipo mahakamani kavuliwa ubunge. Hivi huoni double standard na kwa PhD holder hili halikupawa kufanywa kizembe namna ile. Professor ? real .
Timings, Msikilize Dr Tulia kisha compares and contrasts the two scenarios.
Rejea hapo juu! nilipokueleza kuwa T.Akson PhD anafanyia kazi taarifa rasmi na ndicho walichosema wakati Chadema walipodai kupeleka barua.
Refer the video
Job Ndugai alisema hawezi kufanyia taarifa za kusikia anataka taarifa ya chama.
Akaonyeshwa dispatch book na kunywea hadi alipovurunda siku hizi anazungumza vichochoroni
Refer the video
Mwambie Mwalimu wako Tulia Akson PhD kwamba anachokifanya ni majungu.
Kiroja
Taarifa ya kwenda mahakamani inathibitishwa na nyaraka za mahakama siyo hadithi.
Kwa kukusaidia, na wengine ambao bundle za kumtazama video.
The chronology of events
  1. Jumatano May 11 Usiku. Baraza Kuu Chadema Linawatimua Kina Halima Mdee na timu yake
  2. Alhamisi May 12 asubuhi: Halima Mdee na kundi lake wakafungua shauri Mahakamani Kuu DAR es Salaam na kumjulisha Spika with case number.
  3. Alhamisi saa 9:30 alasiri, Barua ya Chadema yafika Ofisi ya Bunge Dar es Salaam, waelezwa Barua zinapokelewa Dodoma
  4. Ijumaa Saa 3 asubuhi Kigaila afikisha barua kwa Spika Dodoma
  5. Ijumaa hiyo hiyo barua nyingine ya DHL yawasili Bungeni Dodoma.
P huwezi kwenda na kudai CCM wamekteua kuwa Mbunge na eti T. Akson PhD akakubali tu kwasababu anakujua ni mwanafunzi wake na unaandika makala magazeti! hell no! that is stupid
Hiki ni Kiroja!.
Kazi za umma zinafanywa kwa taratibu na nyaraka, alipaswa kuwaambi wampe barua ya mahakama
Refer the video
Kiroja.
Pasco please
Chadema walijua mchezo wa Serikali, Bunge na Mahakama. Kutafuta nani amefanya forgery ingechukua miaka 10. Hawa si ndio wanamsubiri dereva wa Tundu Lissu?
You have a point to do with trust
Polisi wana intelejensia ya kubaini uhalifu tuhuma za Chadema zilitosha zinatoka katika taasisi. Hilo linawezekana huko kwenye Polisi wa kweli, hapa kwetu ni kichekesho tu
Kuna vitu polisi wanaweza, ila you have to report, sio kusema tuu kwenye press conference
Kwa taarifa yako kesi ya COVID19 itaisha 2025 December.
Asante kwa taarifa.
Hili neno.
Hoja usiyojibu, mawakili wa serikali wanamwakilisha nani?
Kesi ni ya wanachama na chama chao, hao mawakili ni kwa ajili ya nani
Ukifungua shauri lolote kuihusu Taasisi yoyote ya serikali,
Mshtakiwa wa kwanza ni Taasisi husika
Mshtakiwa wa pili ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Ni hitimishe kwa kukuambia Pascal hoja zinajibiwa kwa hoja, unachoeleza kwa maelezo mengi ni kutaka kupoteza wasomaji. Tulia Akson PhD na Professor hakufuata au hajui taratibu za ofis
Wewe wasema!.
Inasikitisha Spika wa Bunge anafanyia kazi taarifa za majungu na si za kiofosi.
Kiroja ila refer the video
Spika alikuwa na barua ya CDM ya kiofisi si vikaratasi vya COVID. Barua ya mahakama ni ya kiofisi
The video
Suala zima limemuonyesha Tulia, Tuna tatizo nchini, huyu anaongoza mhimili wa kutunga sheria! eee mola! ee mungu inusuru nchi hii.
Sala yako mungu atainusuru, usichojua ni Dr. Tulia Akson ndiye chaguo la Mungu kuwa Spika wetu kwa Bunge Letu. Uthibitisho wa hili ni mimi mwenyewe
P
 
Hawa C-19 hata wakiendelea na ubunge acha iwe hivyo kwa kuwa mamlaka inawakingia kifua. Lakini kwani 2025 ni mbali?
 
Mkuu Pascal Mayalla ingawa hukujibu hoja umetumia video ya Mwalimu wako Tulia Akson, kwasehemu kubwa sana unanikwaza. Ninakwazika pale unapotaka niangalie Tulia kasema nini

Tulia ni Professor , ni Mbunge, ni Spika. Inaniwia tabu sana kumtafutia position kwa nafasi zake hizo
Kuwa na point GPA n.k. ni tofauti na shughuli nyingine kama za utawala

Tanzania tunafanya makosa kudhani kuwa 'academic excellence' ina mashiko katika management. Tulia anaweza kuwa mwalimu mzuri, kwa siasa na management hana tofauti na diwani yoyote wa CCM.
 
Mkuu pascal alishakuwa furushi tupu.
Haoni mapungufu ya uteuzi wa hawa covid 19?
 
Mayala amekuwa kama wale akina mama wambeya wa uswahilini. Maneno mengi yasiyo na chochote, wala ushahidi.
 
Mmbeya huyu, hata siku moja hataleta ushahidi wowote, kwa sababu hana.
 
We andika ujinga wooote lakini tushakujua ulikuwa mmoja wa wasaidizi wa yule chizi Musiba
 
Ukweli ni huu
CHADEMA ni Mbowe tu wengine holahola
Mbowe anajua na alifacilitate Kina Mdee kuwepo bungeni.
Mnyika alisaini na kutuma majina na nyaraka zingine NEC
CCya CHADEMA ilikosea kwenye process na ilivuka mipaka yake kikatiba ya CHADEMA
Katiba ya CHADEMA inakiuka katiba ya nchi. Kunyima mwana Chama kwenda mahakamani.
Mbowe si msafi CHADEMA na anaitumia Kwa maslahi binafsi.
MaCHADEMA upofu wa ushabiki umeua akili zao hata kutoona ukweli
CHADEMA kimepoteza mwelekeo na hakina tena diraa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…