Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi

Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi

Wanabodi,

Leo tena nimepata fursa kuwaletea zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" na issue iliyo mezani ni Sakata la wabunge 19 wa Chadema, Chadema imewatimua ikijua it's done with them, Spika wa Bunge amewakingia kifua, hivyo wanaendelea na ubunge wao kusubiria aumuzi wa mahakama.

Humu JF, tuko wanachama wa aina nyingi, ila pia sisi wanachama wa JF, kuna baadhi yao ambao wana command much respect humu jukwaani, hivyo bandiko hili ni kuwajibu baadhi yao.

Siku zote Chadema imekuwa ikiendesha baadhi ya mambo yake kienyeji enyeji bila kufuata Katiba sheria taratibu na kanuni na haswa timua timua zake, japo Chadema ina katiba, na hiyo katiba imeweka miongozo yote ya kushughulikia nidhamu, kwa lengo la kutenda haki, lakini hakuna hata timua timua moja ambayo Chadema wamefuata katiba yake. Timua timua zote ni kinyume cha katiba yake, and always they have been doing that and go away.

This time around, kwenye hili la kina
Halima Mdee, Chadema imekwaa kisiki, tena kisiki cha mpingo, ukijikwaa kwenye kisiki cha mpingo, lazima utaumia wewe, hivyo hili ni Bandiko la kuwahimiza rafiki zangu wana Chadema, Kwa Chadema as chama as well as individually, they should always seek the truth & the truth will set them free. Uamuzi wa Spika wa Bunge, Dr. Tulia Akson kuwakingia kifua, wabunge waliowatimua kikangaroo ni uamuzi sahihi, yaani uamuzi very right, done at the right time and done right.

Ushauri wangu kwa Chadema ni from now, Chadema must learn, the hard way, not only how to do the right things, but also do them right!.

Mkuu Fundi Mchundo , vitu vingine sio vya kuuliza ni kutaka tuu kumuonea Spika.
Uchaguzi unasimamiwa na NEC, Wabunge wote wanapewa barua ya utambulisho ya NEC ndio wanatinga Bungeni. Sii kazi ya Bunge au Spika kuhoji wamepatikanaje, as long as Barua ya utambulisho ya NEC imemfikia then ni authentic letter, Bunge halina sababu yoyote kuhoji utambulisho wa NEC.

Humu JF wengi wana mahaba na Chadema hivyo they are just too blind to see jinsi inavyofanya mambo ya hovyo. Hili jambo ni Chadema wenyewe wameli mishandled toka mwanzo.

Naomba niunganishe na hoja ya Mkuu Nguruvi3 nizijibu kwa pamoja kuwaonyesha makosa ya Chadema ya kijinga kabisa.

Kwa faida ya wengine naomba nianzie mbali.
  1. Hili jambo limeanzishwa na Chadema kususia kutambua matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ikasema hailitambui Bunge na haitambui Rais
  2. NEC ikatoa nafasi 18 za viti maalum, Chadema wakasema hawateua na hawana time.
  3. Mdee of course, accompanied by Bulaya, wakam consult a very high ranking Kigogo wa Chadema on the benefits of hizo nafasi 19, Kigogo huyo not only gave them a go ahead, but also facilitated them!.
  4. Introduction credentials from Chadema (a bone of contention) introduced the 19 to NEC.
  5. NEC wakawapa barua za utambulisho, authentic bonafide genuine certificates wakaziwasilisha Bungeni, hivyo Kibunge, hawa ni Wabunge halali kabisa!.
  6. Spika/Bunge has nothing to do with the process iliyotumika kumpata mbunge yoyote, as long as ameteuliwa na NEC.
  7. Kukitokea mgogoro wowote wa Uchaguzi, kwa mtu yoyote kupinga ushindi wa mgombea mahakamani, huyo Mbunge ataendelea kuwa mbunge mpaka mahakama itakapotoa hukumu.
  8. Na kukitokea mgogoro wa kichama, mbunge yoyote kufutwa uanachama na chama chake, anapaswa kupoteza ubunge wake automatically ila akiliarifu Bunge kuwa amepinga mahakamani kuvuliwa kwake uanachama, Bunge litamkingia kifua kusubiria aumuzi wa mahakama.
  9. Hivi ndivyo ilivyofanyika kwa Hamad Rashid Mohammed, David Kafulila na Zitto Kabwe. Na baada ya uamuzi wa mahakama, walivuliwa ubunge, Zitto alijivua na kuaga rasmi Bunge.
  10. Hivyo jana asubuhi kupitia Bunge live, Spika alizungumza huku nikimuona kwa macho yangu na kumsikia kwa masikio yangu, alitangulia kupokea taarifa ya kina Mdee kufungua kesi mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama, kwa kutaja siku, saa na dakika, kabla ya kupokea taarifa rasmi ya Chadema kuwafuta uanachama. Hivyo Spika Tulia yuko right na Bunge liko right kuwakingia kifua.
  11. Haya sasa ninayoendelea nayo ni yangu. Watu wengi humu wana mahaba niue na Chadema, na siku zote mapenzi yakizidi huleta upofu hivyo hamuoni makosa ya Chadema.
  12. Baada tuu ya Wabunge hao kuapishwa na Chadema kuwakana, sisi washauri wa bure tukawashauri Chadema wafanye a due process wameingiaje Bungeni, barua ya utambulisho toka Chadema imeandikwa na kusainiwa na nani.
  13. Hii due process ingebainisha kuna forgery, forgery ni jinai, walipaswa kuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike na hiyo barua yao ya utambulisho, iwe authenticated na ingebainika ni forgery, wala sio Bunge bali ni NEC ndio wangetengua zile barua zao za uteuzi na wangevuliwa ubunge.
  14. Chadema ina katiba yake katiba hiyo imeweka sheria taratibu na kanuni za nidhamu. CC ni mamlaka ya nidhamu ya wabunge, kwanini waliliendesha shauri la wabunge hao Kikangroo bila kufuata taratibu na kanuni zao. Kwanini CC ya Chadema wawatimue wabunge hao bila kufanyika kwanza kwa a due process?!
  15. CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee, mwisho wa mamlaka ya CC ya Chadema kwa Mwenyekiti wa Bawacha ni kumsimamisha tuu, lakini mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu, sasa hiyo CC ya Chadema, ilipata wapi mamlaka ya kumtiimua Halima Mdee?.
  16. Kikao cha Baraza Kuu kilipoitishwa kwanini hawakupeleka shauri la Mdee kwenye mamlaka yake sahihi ya nidhamu?.
  17. Baraza Kuu linapokaa kama mamlaka ya rufaa kwa wale wabunge 18, ukimuondoa Halima Mdee, kabla ya kupiga kura kuridhia maamuzi ya CC, walipaswa kujiridhisha kuwa taratibu zilifuatwa.
  18. Kile kikao cha CC ya Chadema mimi nimekiita CC ya Chadema imekaa kama a Kangaroo Court, na ule uamuzi wa CC ya Chadema, mimi niliuita ni uamuzi wa Kikangroo, kitendo cha Baraza Kuu kuyabariki maamuzi batili ya Kikangroo bila kufanyika kwanza kwa a due process, kumepelekea Baraza Kuu Chadema kufanya Ukangaroo as well.
  19. A way forward ni Mahakama ambayo ni a proper court itayapindua maamuzi ya Kikangroo ya CC ya Chadema yaliyobarikiwa na Baraza Kuu na kuamuru a due process ifanyike.
  20. Wito wangu kwa wapenzi wa Chadema, seek the truth and the truth will set you free. Iambieni Chadema ukweli, ndio mtaijenga Chadema kuwa ni chama mbadala kuireplace CCM. Kwa haya madudu na maroroso kama haya, Ikulu yetu wangeweza?.
Paskali
Pascal Mayalla

Tulikuambia Mwalimu na Dkt wako hakuna kitu! unahitaji ushahidi mwingine?

JokaKuu
Mkuu Nguruvi3, usiniambie na wewe ambaye ni one of ma top GT wa humu jf, usiniambie na wewe umeingia chaka na ile hukumu ya juzi ni hukumu ya ku stuck out hilo shauri kutokana na procedural improperity lakini sio shauri lenyewe!.

Shauri lenyewe la msingi ni ombi la certiorari na mandamus dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama utakaowapotezea sifa za kuwa wabunge. Ombi hili hufanywa kwa judicial review ambayo huombwa kwa kujaza a chamber summons suppoted by affidavits. Hivyo sio kesi imehukumiwa kina Mdee wameshindwa Chadema wameshinda!. No!
kilichofanyika na uamuzi huo ni kwamba
  1. Kina Mdee na kundi lake wamefungua shauri mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema na CC ya Chadema, kutakako pelekea wao kupoteza ubunge wao.
  2. Shauri hilo ni ombi la certiorari na mandamus kupitia a judicial review
  3. Mahakama Kuu imeweka procedure ya jinsi ya ku file a lawsuit of judicial review is by filling a chamber summons suppoted by affidavits.
  4. Kina Mdee wametimiza takwa hili.
  5. Chadema ikatoa mapingamizi 7 kupinga kupokelewa kwa shauri hilo.
  6. Mahakama Kuu imekubaliana na baadhi ya hoja Chadema kuwa kuna makosa ya procedural improperity lakini sio shauri lenyewe.
  7. Hivyo mahakama ime struck out, yaani imegoma kupokea ombi la kina Halima Mdee na sio kuwa ombi limekataliwa.
  8. Kinachofuatia no kina Mdee, ku rekebisha ombi lao na kuliomba upya.
  9. Hivyo Mwalimu wangu wa Sheria, Dr. Tulia Akson Mwansasu yuko very right kwenye hili, kama nilivyo eleza hapa
  10. Hapa Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi
Therefore, hii ngoma bado ni mbichi, it's not over until it's over!. Ila pia nimebaini kunahitajika wataalamu wa sheria, kuwa wanawafafanulia wananchi hukumu mbalimbali kwa lugha rahisi ya wananchi.
P.
 
Ulikubaliana na nani?
Mkuu nguvu, jambo lolote likitokea na likifanyika na kukamilika, katika kulielezea jambo hilo, tunaanza na hoja kuwa tumekubaliana, hata kama mlibishana sana kuhusu jambo hilo na hamkukubaliana kabisa, lakini katika kulieza ni kueleza bado tunaeleza kuwa tumekubaliana kutokukubaliana.
P
 
Mkuu Nguruvi3, usiniambie na wewe ambaye ni one of ma top GT wa humu jf, usiniambie na wewe umeingia chaka na ile hukumu ya juzi ni hukumu ya ku stuck out hilo shauri kutokana na procedural improperity lakini sio shauri lenyewe!.

Shauri lenyewe la msingi ni ombi la certiorari na mandamus dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama utakaowapotezea sifa za kuwa wabunge. Ombi hili hufanywa kwa judicial review ambayo huombwa kwa kujaza a chamber summons suppoted by affidavits. Hivyo sio kesi imehukumiwa kina Mdee wameshindwa Chadema wameshinda!. No!
kilichofanyika na uamuzi huo ni kwamba
  1. Kina Mdee na kundi lake wamefungua shauri mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema na CC ya Chadema, kutakako pelekea wao kupoteza ubunge wao.
  2. Shauri hilo ni ombi la certiorari na mandamus kupitia a judicial review
  3. Mahakama Kuu imeweka procedure ya jinsi ya ku file a lawsuit of judicial review is by filling a chamber summons suppoted by affidavits.
  4. Kina Mdee wametimiza takwa hili.
  5. Chadema ikatoa mapingamizi 7 kupinga kupokelewa kwa shauri hilo.
  6. Mahakama Kuu imekubaliana na baadhi ya hoja Chadema kuwa kuna makosa ya procedural improperity lakini sio shauri lenyewe.
  7. Hivyo mahakama ime struck out, yaani imegoma kupokea ombi la kina Halima Mdee na sio kuwa ombi limekataliwa.
  8. Kinachofuatia no kina Mdee, ku rekebisha ombi lao na kuliomba upya.
  9. Hivyo Mwalimu wangu wa Sheria, Dr. Tulia Akson Mwansasu yuko very right kwenye hili, kama nilivyo eleza hapa
  10. Hapa Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi
Therefore, hii ngoma bado ni mbichi, it's not over until it's over!. Ila pia nimebaini kunahitajika wataalamu wa sheria, kuwa wanawafafanulia wananchi hukumu mbalimbali kwa lugha rahisi ya wananchi.
P.
Mkuu Pascal Mayalla

Kwani Spika Dkt Prof Tulia anasubiri nini? mwenendo wa kesi au maamuzi ya Mahakama?
Maamuzi yametoka bila kujali technicalities na yeye alisema anasubiri maamuzi!
Si kazi ya Spika kfuatilia procedure za Mahakama

Mwl wako anabofoa si kwa kesi hii hata anavyoendesha kazi mjengoni ni aibu tupu. Bunge sasa ni UVCCM

Magufuli alituumiza sana, watu kama akina Tulia ni zao la utawala hovyo! tunaishi na maumivu

JokaKuu
 
Mkuu Pascal Mayalla

Kwani Spika Dkt Prof Tulia anasubiri nini? mwenendo wa kesi au maamuzi ya Mahakama?
Maamuzi yametoka bila kujali technicalities na yeye alisema anasubiri maamuzi!
Si kazi ya Spika kfuatilia procedure za Mahakama

Mwl wako anabofoa si kwa kesi hii hata anavyoendesha kazi mejngoni ni aibu tupu. Bunge sasa ni UVCCM

Magufuli alituumiza sana, watu kama akina Tulia ni zao la utawala hovyo! tunaishi na maumivu

JokaKuu

..Spika inabidi aeleze nini kinaendelea baada ya maamuzi yalitolewa na mahakama kuu.

..kwanini hachukui hatua wakati uamuzi unaosimama mpaka sasa hivi ni ule wa Cdm kuwafuta uanachama kina Halima?

..Je, kina Halima wamefungua maombi mapya mahakamani? Je, Spika ana taarifa hizo?

..Je, Spika amepewa maelekezo yoyote na mahakama kumzuia asiwaondoe kina Halima bungeni?
 
Kwamba Spika anatafuta habari zinazowahusu COVID19 zikiwa njema tu hatafuti habari zinazowahusu zikiwa mbaya

Tangu jana alipaswa awe amewasimamisha hadi mahakama itakapotoa uamuzi mwingine kama utakuwepo

Kinachofanyika hapa ni kuchafua tu sheria za nchi na anayefanya haya ni Spika Dr Prof Tulia (sad)

Kwa upande mwingine jambo hili linaonyesha '' DHAMIRA NA NIA'' na Mh F.A.MBOWE aione dhamira na nia njema!!
 
..Spika inabidi aeleze nini kinaendelea baada ya maamuzi yalitolewa na mahakama kuu.

..kwanini hachukui hatua wakati uamuzi unaosimama mpaka sasa hivi ni ule wa Cdm kuwafuta uanachama kina Halima?

..Je, kina Halima wamefungua maombi mapya mahakamani? Je, Spika ana taarifa hizo?

..Je, Spika amepewa maelekezo yoyote na mahakama kumzuia asiwaondoe kina Halima bungeni?
Ni ajabu kwamba Pascal haioni mantiki hii - au anavutiwa kuiepa.

Mabandiko yake marefu yangekuwa na maana kama angekiri mishkeli hii ya msingi ya Spika na kujaribu kuielezea hata kwa kuspin akijisikia.
 
Ni ajabu kwamba Pascal haioni mantiki hii - au anavutiwa kuiepa.

Mabandiko yake marefu yangekuwa na maana kama angekiri mishkeli hii ya masingi ya Spika na kujaribu kuielezea hata kwa kuspin akijisikia.

..niliwahi kumwambia Pascal kuwa wakati mwingine anapotosha.
 
..niliwahi kumwambia Pascal kuwa wakati mwingine anapotosha.
Mkuu, uzuri Pascal amesha-declare kuwa yeye ni kada wa CCM. Waelewa tunaelewa jinsi CCM inavyoathiri nafsi za waumini wake. Basi atupotoshe kwa akili; asionyeshe kudharau uelewa wetu.

Anajua tunajua vizuri sana kuwa anachofanya Spika tangu mwanzo (enzi za Ndugai) ni uhuni. Akiri huu mushkeli na kuuelezea kwa mantiki nzuri za kiCCM tukubali kutokubaliana. No need to insult our intelligence.
 
Kwa hii hukumu ya Leo, nimepigwa bonge la surprise!

Wanabodi,
Baadhi ya mabandiko yangu sio mabandiko ya average mind ni mabandiko ya deep thinkers, moja ya mabandiko hayo ni Bandiko hili Ushauri wa Bure: Ukijikwaa ukaanguka, usiangalie tu pale ulipoangukia, bali angalia pale ulipojikwaa

Maadam Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya kina Mdee, hiki nilicho andika kwenye bandiko hili, sasa ndio kinakwenda kutokea!. It will be very devastating and disturbing!.

Wale ambao sio average mind, wana uwezo to connect the dots, baada ya Chadema kumtimua Zitto kwa dhulma, there are bad things that happed to Chadema na wahusika wa kadhia ya Zitto, but no one connected the dots and linked the consequences, hivyo sasa baada ya Chadema kuwatimua hawa Wabunge 19, naombeni sasa watch closely what will happen to Chadema and the main players and connect the dots.

God forbids!.
P.
Tumia akili na Maarifa yako vizuri unaweza kuonekana Mpuuzi na wakati wa kurekebisha umekupita kama huna Kazi za kufanya omba upewe ajira Ndugu yangu hizi aibu Ndogo Ndogo zikupite
 
Mkuu Pascal Mayalla

Kwani Spika Dkt Prof Tulia anasubiri nini? mwenendo wa kesi au maamuzi ya Mahakama?
Maamuzi yametoka bila kujali technicalities na yeye alisema anasubiri maamuzi!
Si kazi ya Spika kfuatilia procedure za Mahakama

Mwl wako anabofoa si kwa kesi hii hata anavyoendesha kazi mejngoni ni aibu tupu. Bunge sasa ni UVCCM

Magufuli alituumiza sana, watu kama akina Tulia ni zao la utawala hovyo! tunaishi na maumivu

JokaKuu
I'd like to differ, to me she is much much better than her predecessor.

Soma hii Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!
P
 
Hapana! unalinganisha uvundo

Tulia si ndiye alisema Rais ni mkuu wa mihimili yote! kwani separation of power inafundishwa mwaka wa ngapi?

Msikilize maamuzi yake yote ni politics tu no legal mind at all.

Si huyu Tulia ndiye alitoa maamuzi kabla ya mahakama !

Tulia akasema Mahakama ikitoa uamuzi ataufuata! Uamuzi si umeshatoka sasa procedure za mahakama zinamhusu vipi! Hana credibility wala integrity, muongo, mnafiki tu

Huyu ni zao la utawala mbovu wa JPM! Hakuna kitu pale ! Madhara ya JPM ni haya , tunaishi nayo

JokaKuu
 
Hapana! unalinganisha uvundo
Mkuu Nguruvi3 , hii sio lugha ya ki GT!.
Tulia si ndiye alisema Rais ni mkuu wa mihimili yote! kwani separation of power inafundishwa mwaka wa ngapi?
Somo la Topic ya kwanza la LW200, mwaka wa kwanza.
Kinachofundishwa kuhusu the separation of power is a myth, the truth ni alicho kisema, it's true kuna Mhimili uliojichimbia chini zaidi!.
Msikilize maamuzi yake yote ni politics tu no legal mind at all.
Not true!.
Si huyu Tulia ndiye alitoa maamuzi kabla ya mahakama !.
She did the right thing!.
Tulia akasema Mahakama ikitoa uamuzi ataufuata! Uamuzi si umeshatoka sasa procedure za mahakama zinamhusu vipi! Hana credibility wala integrity, muongo, mnafiki tu.
Lazima tujifunze kutofautisha uamuzi na struck out.
Hapa naeomba nikuelimishe wewe na wengine
  1. Shauri ni la kuomba mambo mawili, 1. Certiorari kulizuia Chadema kuwatimua na Mandamus kuilazimisha Chadema kuwarejeshea uanachama wao.
  2. Ombi hilo huombwa kupitia shauri la Judicial Review na husikilizwa na majaji watatu.
  3. Kabla ombi hilo kuruhusiwa kifunguliwe, muombaji muombaji anatakiwa kumuomba kibali cha mahakama kufungua shauri hilo Kwa kujaza chamber summons suppoted by affidavits. Hizi ni procedures. Ombi hilo husikilizwa na Jaji mmoja.
  4. Hivyo kilichofanyika ni ombi la kufungua shauri ndio limekuwa struck out, for being defective na sio dismissed.
  5. Hivyo watarekebisha makosa, waombe tena kibali cha kufungua shauri.
  6. Wakikubaliwa kufungua shauri, ndio watasikilizwa, uamuzi wa shauri ndio unamatter.
  7. Kupitia hii kesi nimebaini fursa, watu wanahitaji sana elimu ya sheria.
Huyu ni zao la utawala mbovu wa JPM! Hakuna kitu pale ! Madhara ya JPM ni haya , tunaishi nayo

JokaKuu
JPM was not a saint and so does Samia, JK, Mkapa, Mwinyi and Nyerere, huna sababu ya kumtaja JPM kwa ubaya kuhusu utawala mbovu pia ana mema yake!.

Hivi hatuwezi kujadiliana bila any consecration of the dead?. Waacheni wafu wapumzike kwa amani!.
P
 
Mkuu Nguruvi3 , hii sio lugha ya ki GT!.
Napata tabu sana kutafuta maneno ya kuwapendeza watu, I'm a straight shooter
Ndugai na Tulia wanatofauti za jinsia tu lakini wana 'like mind'
Huwezi kuwaweka katika mizani na akina Sapi, Msekwa, Sitta !
Somo la Topic ya kwanza la LW200, mwaka wa kwanza.
Kinachofundishwa kuhusu the separation of power is a myth, the truth ni alicho kisema, it's true kuna Mhimili uliojichimbia chini zaidi!
Leo US , SCOTUS imefuta Roe V Wade ruling iliyodumu 50 yeaars. Biden kama wengine wote wanalalamika
Biden kahutubia taifa na kusema hana option nyingine kama executive power!

Mjini London, Boris Johnson aliitwa na Polisi na kuhojiwa kama raia mwingine
Spika wa House of common akawazuia conservatives waliotaka kuleta mizengwe ya kuficha uozo wa Boris

Kama uliwahi kusikiliza mabunge ya huko nyuma utabaini kulikuwa na element za separation of power, siku hizi Bunge linasubiri maagizo sawa na UVCCM. Mijadala ya mjengoni imebaki kuwa debate za high school
The buck stops with her
.

Not true!.

She did the right thing!.
Kutoa maagizo kabla ya mahakama ilikuwa ku pre empty judgement. Kwa mwanasheria kulikuwa naoption nyingine bora ambazo zingetoa majibu yale yale aliyotarajia.
Lazima tujifunze kutofautisha uamuzi na struck out.
Hapa naeomba nikuelimishe wewe na wengine
  1. Shauri ni la kuomba mambo mawili, 1. Certiorari kulizuia Chadema kuwatimua na Mandamus kuilazimisha Chadema kuwarejeshea uanachama wao.
  2. Ombi hilo huombwa kupitia shauri la Judicial Review na husikilizwa na majaji watatu.
  3. Kabla ombi hilo kuruhusiwa kifunguliwe, muombaji muombaji anatakiwa kumuomba kibali cha mahakama kufungua shauri hilo Kwa kujaza chamber summons suppoted by affidavits. Hizi ni procedures. Ombi hilo husikilizwa na Jaji mmoja.
  4. Hivyo kilichofanyika ni ombi la kufungua shauri ndio limekuwa struck out, for being defective na sio dismissed.
  5. Hivyo watarekebisha makosa, waombe tena kibali cha kufungua shauri.
  6. Wakikubaliwa kufungua shauri, ndio watasikilizwa, uamuzi wa shauri ndio unamatter.
  7. Kupitia hii kesi nimebaini fursa, watu wanahitaji sana elimu ya sheria.
Mkuu kazi ya mahakama si kuelekeza mteja afanye nini.

Kitu kimoja ninachojua, kilichofanyika ni mchezo kama ule wa hukumu ya Wakurugenzi. Mahakama za chini zilitoa hukumu kwa kusema haikuwa sahihi kwa Wakurugenzi kusimamia chaguzi. Wana harakati na Wapinzani walifurahi sana bila kujua ni trick ya kuisafisha mahakama. Kesi ilipokwenda mahakama kuu uamuzi ukabadilishwa kwamba '' Wakurugenzi wanakula kiapo na hivyo kutenda haki'' ni hukumu ya hovyo sana iliyodhalilisha mahakama lakini kama tulivyowahi kujadiliana mimi na wewe '' mzee wa GPA 4.0 probation period ilimuathiri' tuachie hapo

Hii kesi nayo inachezewa hivyo ili COVID19 ionekana mahakama inasimamia haki, guess what dana dana zitapigwa hadi 2025 au la inaweza kutoka hukumu tukashika vichwa

Mkuu pasco , ukikosea procedure ina maana hakuna shauri hadi utakaporekebisha na kuwasilisha tena
Hadi hapo hakuna kesi iliyopo mahakamani na hoja aliyotumia Mwalimu wako Dr Pof Tulia nayo inapoteza mashiko
Hii haitaji kubobea katika sheria ni mambo ya wazi tu.

Jumatatu utamsikia Spika Dkt Tulia akizungumza kwasababu tayari keshaandaa mazingira ya COVID kurekebisha
Tulia anadhalilisha sana taaluma yake, Wanafunzi wake., Bunge n.k.

Suala la COVID19 lipo wazi ni michezo michafu tu na bahati nzuri michezo hiyo inachezwa Tanzania
Ingalikuwa nchi nyingine ufujaji wa kodi kwa malipo ya CIVID ingalikuwa scandal

JPM was not a saint and so does Samia, JK, Mkapa, Mwinyi and Nyerere, huna sababu ya kumtaja JPM kwa ubaya kuhusu utawala mbovu pia ana mema yake!.

Hivi hatuwezi kujadiliana bila any consecration of the dead?. Waacheni wafu wapumzike kwa amani!.
P
Heee! Miaka 23 tunamtaja Nyerere kila siku kwa mazuri na mabaya yake
Tumemsema Mkapa kwa mazuri na Mabaya yake
JPM hana tofauti na Marehemu wengine wote duniani

Hii habari ya kutaka kuficha mabaya yake wengine hatuikubali, ikiwa ni hivyo tusizungumzie Marehemu yoyote

Otherwise JPM alituachia ubovu mkubwa sana hasa alipochafua uchafuzi wa 2020 na kuweka watu wake pale mjengoni na Mwalimu wetu ni zao lake, tunaishi na ubovu wa mabaya ya JPM kila uchao! hakuna namna tutasema tu !

JokaKuu
 
Mkuu Nguruvi3 , hii sio lugha ya ki GT!.
Lazima tujifunze kutofautisha uamuzi na struck out.
Hapa naeomba nikuelimishe wewe na wengine
  1. Shauri ni la kuomba mambo mawili, 1. Certiorari kulizuia Chadema kuwatimua na Mandamus kuilazimisha Chadema kuwarejeshea uanachama wao.
  2. Ombi hilo huombwa kupitia shauri la Judicial Review na husikilizwa na majaji watatu.
  3. Kabla ombi hilo kuruhusiwa kifunguliwe, muombaji muombaji anatakiwa kumuomba kibali cha mahakama kufungua shauri hilo Kwa kujaza chamber summons suppoted by affidavits. Hizi ni procedures. Ombi hilo husikilizwa na Jaji mmoja.
  4. Hivyo kilichofanyika ni ombi la kufungua shauri ndio limekuwa struck out, for being defective na sio dismissed.
  5. Hivyo watarekebisha makosa, waombe tena kibali cha kufungua shauri.
  6. Wakikubaliwa kufungua shauri, ndio watasikilizwa, uamuzi wa shauri ndio unamatter.
  7. Kupitia hii kesi nimebaini fursa, watu wanahitaji sana elimu ya sheria.
P
Mkuu Pascal Mayalla , JokaKuu amesema mara nyingi kuwa unapotosha

Umemsikia wakili wa COVID19 baada ya kufanya marekerekbisho?
1. Wamepeleka maombi upya na kuyalipia na kesi imepewe namba mpya
2. Wameomba mahakama ''ilinde Ubunge wao'' kwa kujua hawana sifa baada ya kesi kutpwa, si shauri

Maana yake ni moja, kwamba, COVID19 walipoteza kesi yenye shauri! hawakupoteza shauri

Kwa kupoteza kesi hawakuwa na status ndiyo maana Mwalimu wako Dkt Prof alijificha

Tunajua kinachofanyika si sheria ni politics na uhuni huni tu usiokuwa na maana yoyote
 
Ukifuatilia mijadala hapo juu utabaini kizazi kijacho kinahitaji mabadiliko makubwa katika kujenga watu wenye mawazo yenye Busara na kujenga.
Mfano Kuna hoja ya wanasiasa waliovuliwa ubunge pamoja na kukata rufaa mahakamani.Swali je,Ilikuwa ni sahihi kama jibu ni hapana je,kunahaja ya kuendeleza uvunjaji huo wa haki?
Chama kinacho Nadi kuwatendea haki wananchi kinashindwaje kutenda haki Kwa watu wao wachache Kwa kufuata haki badala ya chuki na uhasama?

Katiba ya nchi inayo onesha njia ya kupata haki ndiyo matamanio ya wengi inakuwaje sasa Katiba ya chama kinachoshinikiza tuwe na katiba Bora ya nchi inakuwa mfano wa kushindwa kuheshimu mambo ya kikatiba kuanzia Ngazi ya chama?

Naamini Kuna watu wanadai katiba mpya alafu hawajui kama wakiipata watakuwa na wajibu gani katika Katiba.

Wanaweza kufikiria kwamba tukipata Katiba mpya basi watakuwa wamepata nafasi ya kuiongoza nchi kumbe Kuna mchakato zaidi unahitajika ilikufikia malengo hayo na ndani ya katiba nzuri Pia watakuwa na changamoto kama zinazotokea kwenye chama kinachotaka kufukuzafukuza wanachama ambao nao wanalindwa na katiba.
 
Napata tabu sana kutafuta maneno ya kuwapendeza watu, I'm a straight shooter
Ndugai na Tulia wanatofauti za jinsia tu lakini wana 'like mind'
Huwezi kuwaweka katika mizani na akina Sapi, Msekwa, Sitta !
Mkuu Nguruvi3 , hili la Tulia kuwa Spika, kwanza nilisikia sauti nikalileta humu, Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... sababu za mimi kuisikia hii sauti ni hii
Leo nilikuwa naangalia jinsi Bunge la Marekani, the Congress linavyomshughulikia rais wa Marekani, Donald Trump, ambapo azimio la kumshitaki kwenye Bazara la Senate limepitishwa, japo kule Senate itakuwa ni ngumu kwa azimio hilo kupata ile theluthi 2 ya kumuondoa ila kumshitaki tuu rais ni hatua kubwa.

Kuna mchangiaji mmoja akasema hata Tanzania ikithibitishwa rais Magufuli amevunja katiba kwa kuzuia mikutano ya siasa kinyume cha katiba, anaweza kushtakiwa!.

Ndipo nikauliza ni Bunge lipi hilo la kumshitaki Rais Magufuli?, nikauliza kama ni Bunge hili hili la Mhe. Ndungai au ni Bunge lijalo?, na ndio mara ghafla nikasikia sauti from within, ikiniambia kuwa "Spika ajaye ni Mhe. Dr. Tulia Akson. Sauti hiyo ikaniambia japo Mhe. Ndungai, atakuwa anatamani sana kuendelea kuwa Spika, lakini Ndugai hatakuwa kwa sababu fulani,
hivyo Spika JYN alipojiuzulu, nilisema huu ni mpango wa Mungu, kutupatia Spika bora kwasababu JYN alikuwa ni Bora Spika Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa? hivyo alipochaguliwa Dr. Tulia nilisema Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana! hivyo hiki anachofanya sasa Dr. Tulia ni blending sheria na haki. Mahakama ndio chombo cha utoaji haki nchini Tanzania lakini mara kibao, mahakama hazitendi haki kwasababu ya kufuata sheria. Kisheria ili mtu awe mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa, the moment mtu amevuliwa uanachama, from that very moment anakuwa amepoteza sifa za kuwa mbunge, lakini kwa vile Spika Dr. Tulia, anajua kina Mdee hawajatendewa haki, anatumia the role checks and balance kwa the parliament kui check mahakama na kugrant silent stay orders za kuendelea na ubunge wao hadi shauri lao lisikilizwe.
Leo US , SCOTUS imefuta Roe V Wade ruling iliyodumu 50 yeaars. Biden kama wengine wote wanalalamika
Biden kahutubia taifa na kusema hana option nyingine kama executive power!

Mjini London, Boris Johnson aliitwa na Polisi na kuhojiwa kama raia mwingine
Spika wa House of common akawazuia conservatives waliotaka kuleta mizengwe ya kuficha uozo wa Boris
Kiukweli hapa kwetu mkuu wa mhimili wa The Executive anaogopwa hakuna mfano ndio maana ana kinga ya kutokushitakiwa, ila hana kinga ya kutohojiwa!. Ndio maana baada ya Tundu Lissu kushambuliwa na wale 'wasiojulikana' nikasema humu kama yule aliyetawa kuwa "tume trip simu yake" ni Lissu, na yakatamkwa maneno haya "vita vya uchumi ni ngumu kuliko vita vya kawaida, unajua msaliti huwa anafanywa nini vitani "huwezi kuwa msaliti ukaachwa hivi hivi kusurvive" nikashauri aliyetoa kauli hiyo, awe wa kwanza kuhojiwa!. Tena nikashauri kama wao wanaogopo kumhoji, sisi media tunaweza kumhoji mtu yoyote hata mwenye kinga ya kutokushitakiwa, hivyo waseme tuu wameshindwa, tuwasaidie WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? hapa nilisema
Serikali Imeshindwa Kuwapata Wasiojulikana.
Tukio la Lissu sio la kwanza kufanywa na watu wasiojulikana, hata walimvamia Advocate Kapinga, hawakujulikana hadi leo, waliomdhuru Ulimboka na Kibanda ni wasiojulikana ambao hawajajulikana hadi leo. Waliomdhuru Tundu Lissu ni wasiojulikana na hadi sasa hakuna dalili yoyote. Tusidhani serikali yetu itafika mahali ikasema imeshindwa, bali wenye macho watagundua tuu kuwa hali ikoje, hivyo nashauri wale wenye uwezo, wajitolee kusaidia.
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na ...

Sisi Watu Media Tunawezo wa Kuwabaini Wasiojulikana Hawa hivyo Kusaidia Serikali Yetu Kuwajua.
Sisi watu wa media, kutokana na kuwa na easy access na mtu yoyote, tena hatuhitaji warrant or samansi ya kumfikia yoyote kwa mahojiano, tuna uwezo wa kufanya IJ kuisaidia serikali yetu kuwabaini wasiojulikana hawa, kwanza kwa kuwakabili wanasiasa wote waliowahi kutoa kauli na matamshi ya vitisho na hatarishi yenye kiashiria kuwa mlengwa wa kauli hizo ni Tundu Lissu, hivyo tuwahoji viongozi hawa, walipotoa kauli hizi, walimaanisha nini?. Kama nilivyosema kauli huumba, mtu ukisema, mtu wa aina hii hawezi kuachwa hivi hivi, unabidi uhojiwe ulimaanisha nini, usijekukuta kumbe ni kauli yako ndio imemuumbia kilichompata!. Hili la kuhusu kauli, nimewahi kulizungumza hapa.
Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?

Japo kwa sheria za Tanzania kuna kada fulani ya viongozi katiba yetu iwepa kinga ya kutokushitakiwa Mahakamani lakini hakuna kinga ya kuzuiwa kuhojiwa, wanapotoa kauli tata zenye viashiria vya kufanyika kwa jambo fulani, walimaanisha nini kwa kauli hizo, kwa sababu kuna kauli za viongozi fulani fulani na
hapa natolea mfano tuu, hebu siliza kwa makini kauli hii.
Kama huyu mtu aliyezungumzwa hapa ni Lissu, halafu ni kweli Lissu yamekuja kumtokea mambo mabaya, inawezekana kabisa, aliyetoa kauli hii, alijisemea tuu, bila kuwa na dhamira yoyote ovu, lakini kwa sababu baada ya kauli hii, kuna jambo baya limemfika Lissu, kiukweli kabisa, na jambo hilo sio jambo ndogo la bahati mbaya au uvamizi wa ujambazi, bali ni jambo lililopangwa na watu, na likatekelezwa na watu ambao mpaka mpaka sasa ninapoandika haya, hawa watu bado hawajajulikana, hivyo hakuna ubaya kabisa, kwa mtu aliyetoa kauli hii akaitwa kuhojiwa, nb, kuitwa kuhojiwa sio lazima yeye ndie aende kuhojiwa, bali muhojaji ndio amfuate yeye alipo, amuhoji, tena kistaarabu kabisa, kwa heshima na unyenyekevu, alipo tamka haya kuhusu wasaliti huwa wanafanywa nini vitani, na hii ni vita ya kuichumi, hivyo wasaliti wa vita hii ya kiuchumi wafanywe nini, kwa njia gani, ili kukanusha uhusika wa utekekezaji wa kau;i yake hii!. Kauli kama hii ingetolewa na mtu tuu wa kawaida kama mimi na wewe, inaweza isiwe na impact yoyote, lakini inapotolewa na mtu mwenye mamlaka kuu kuliko zote za nchi, it is different, inaweza kutafsiri kuwa ni amri, hivyo zikiishatolewa ni amri hufuatiwa na utekelezaji tuu. Kisha uchunguzi uhamie Polisi Dodoma kwa nini aliwachukuwa polisi masaa mawili kufika eneo la tukio, kwa nini hawakumhoji dereva au mashuhuda, Then tunakwenda kwenye aneo la tukio kuhoji wote waliokuwepo na mashuhuda wakiwemo askari wa getini, kisha tunamalizia kwa kuelekea Nairobi kwa Lissu na dereva wake.

Kama uliwahi kusikiliza mabunge ya huko nyuma utabaini kulikuwa na element za separation of power, siku hizi Bunge linasubiri maagizo sawa na UVCCM. Mijadala ya mjengoni imebaki kuwa debate za high school
The buck stops with her
Lets give her time.
Kutoa maagizo kabla ya mahakama ilikuwa ku pre empty judgement. Kwa mwanasheria kulikuwa naoption nyingine bora ambazo zingetoa majibu yale yale aliyotarajia.
Hapa ndipo mimi ninapoungana na Dr. Tulia, for the interest of justice, ukijua haki haukutendeka kwenye jambo fulani, licha ya kujua sheria inasemaje, wewe tenda haki, na Dr. Tulia, japo kwenye hili atalaumiwa na wanasheria, lakini atabarikiwa na Mungu kwa kuwatendea haki wanawake hawa!.
Baada ya Baraza Kuu Chadema kuridhia kutimuliwa kwao na CC ya Chadema, taarifa ya Baraza Kuu ikawahishwa Ofisi ya Bunge Dar es Salaam, mpokeaji akagoma kuipokea barua kwa hoja kuwa wahusika wote wako Dodoma, hivyo barua ipalekwe Dodoma. Kisheria from that moment Baraza Kuu la Chadema limethibitisha kuvuliwa uanachama, hao sio wanachama tena na ubunge wao ulikomea pale!. But the interest of justice, Dr. Tulia alisubiri kwanza apate uthibitisho wa kina halima kufungua kesi, ndipo taarifa ya Baraza Kuu ikapokelewa.

The same applies to now, baada tuu ya Mahakama Kuu ku struck out maombi yao, at that very moment, hakukuwa na kesi yoyote mahakamani na hawa sio wanachama walipoteza sifa za kuendelea kuwa wabunge, but for interest of justice, kule Bungeni, taarifa itakafika kwanza mezani kwa Spika ni taarifa ya kufunguliwa kwa shauri jipya, halafu ndio hukumu ya struck out ikafuatia.

Mimi kama mtetezi huru wa haki sio tuu nataka kina Halima watendewe haki, nataka Chadema wajifunze kutenda haki kwa kuzingatia Katiba yao, sheria, taratibu na kanuni katika kufanya jambo lolote.
Mkuu kazi ya mahakama si kuelekeza mteja afanye nini.

Kitu kimoja ninachojua, kilichofanyika ni mchezo kama ule wa hukumu ya Wakurugenzi. Mahakama za chini zilitoa hukumu kwa kusema haikuwa sahihi kwa Wakurugenzi kusimamia chaguzi. Wana harakati na Wapinzani walifurahi sana bila kujua ni trick ya kuisafisha mahakama. Kesi ilipokwenda mahakama kuu uamuzi ukabadilishwa kwamba '' Wakurugenzi wanakula kiapo na hivyo kutenda haki'' ni hukumu ya hovyo sana iliyodhalilisha mahakama lakini kama tulivyowahi kujadiliana mimi na wewe '' mzee wa GPA 4.0 probation period ilimuathiri' tuachie hapo
Ile GPA sio ya 4.0, ni GPA ya 4.9!, ndio a record GPA ya UDSM tangu kianzishwe na haijawahi kufikiwa tena na yeyote mpaka kesho!.
Hii kesi nayo inachezewa hivyo ili COVID19 ionekana mahakama inasimamia haki, guess what dana dana zitapigwa hadi 2025 au la inaweza kutoka hukumu tukashika vichwa

Mkuu pasco , ukikosea procedure ina maana hakuna shauri hadi utakaporekebisha na kuwasilisha tena
Hadi hapo hakuna kesi iliyopo mahakamani na hoja aliyotumia Mwalimu wako Dr Pof Tulia nayo inapoteza mashiko
Hii haitaji kubobea katika sheria ni mambo ya wazi tu.

Jumatatu utamsikia Spika Dkt Tulia akizungumza kwasababu tayari keshaandaa mazingira ya COVID kurekebisha
Tulia anadhalilisha sana taaluma yake, Wanafunzi wake., Bunge n.k.

Suala la COVID19 lipo wazi ni michezo michafu tu na bahati nzuri michezo hiyo inachezwa Tanzania
Ingalikuwa nchi nyingine ufujaji wa kodi kwa malipo ya CIVID ingalikuwa scandal
Hapa nakubalia na wewe ila naungana na Dr. Tulia, kama ili haki itendeke sometimes ni lazima kucheza michezo michafu, then for the interest of justice, mimi Pascal Mayalla, a UDSM LL.B (hons) graduate, naungana na Mwalimu wangu Dr. Tulio Akson Mwansasu, kuhakikisha wabunge 19 wa Chadema, wanatendwa haki!, ikibidi sheria kupindishwa ili haki itendwe, sheria zipindishwe tuu!.
Heee! Miaka 23 tunamtaja Nyerere kila siku kwa mazuri na mabaya yake
Tumemsema Mkapa kwa mazuri na Mabaya yake
JPM hana tofauti na Marehemu wengine wote duniani

Hii habari ya kutaka kuficha mabaya yake wengine hatuikubali, ikiwa ni hivyo tusizungumzie Marehemu yoyote

Otherwise JPM alituachia ubovu mkubwa sana hasa alipochafua uchafuzi wa 2020 na kuweka watu wake pale mjengoni na Mwalimu wetu ni zao lake, tunaishi na ubovu wa mabaya ya JPM kila uchao! hakuna namna tutasema tu !

JokaKuu
Endeleeni kumzungumzia JPM kwa ubaya, sisi wengine mtu akiishatangulia mbele ya haki, we close the chapter na kusongo mbele, sasa tuko na Samia, ila pia nakubali mabaya ya JPM, kuzungumzwa for for sake of lessons ili yasirudiwe na Samia, mimi naamini ni karma ndio imemuondoa Blaza wangu, hivyo ili kumsaidia Samia na yeye asije... namuandalia a tailor made karma class kumtumia JPM kama shamba darasa, kwa kumuonyesha Samia ni karma gani zimesabisha karma ikala kichwa, ili yeye aziepuke karma hizo zisije...
Nimeanza mdogo mdogo Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, Sauti Imeshauri Mama Amkabidhi Kwanza Dr. Mwinyi, Urais wa JMT, Ndipo Aje Mwanamke!

P

P
 
Ukifuatilia mijadala hapo juu utabaini kizazi kijacho kinahitaji mabadiliko makubwa katika kujenga watu wenye mawazo yenye Busara na kujenga.
Mfano Kuna hoja ya wanasiasa waliovuliwa ubunge pamoja na kukata rufaa mahakamani.Swali je,Ilikuwa ni sahihi kama jibu ni hapana je,kunahaja ya kuendeleza uvunjaji huo wa haki?
Chama kinacho Nadi kuwatendea haki wananchi kinashindwaje kutenda haki Kwa watu wao wachache Kwa kufuata haki badala ya chuki na uhasama?

Katiba ya nchi inayo onesha njia ya kupata haki ndiyo matamanio ya wengi inakuwaje sasa Katiba ya chama kinachoshinikiza tuwe na katiba Bora ya nchi inakuwa mfano wa kushindwa kuheshimu mambo ya kikatiba kuanzia Ngazi ya chama?

Naamini Kuna watu wanadai katiba mpya alafu hawajui kama wakiipata watakuwa na wajibu gani katika Katiba.

Wanaweza kufikiria kwamba tukipata Katiba mpya basi watakuwa wamepata nafasi ya kuiongoza nchi kumbe Kuna mchakato zaidi unahitajika ilikufikia malengo hayo na ndani ya katiba nzuri Pia watakuwa na changamoto kama zinazotokea kwenye chama kinachotaka kufukuzafukuza wanachama ambao nao wanalindwa na katiba.
Mkuu Katali , asante sana kwa hoja hii, watu wenye objectivity ya kiwango chako, humu kwenye hii jf ya sasa, ni wa kutafuta kwa tochi!.
Thanks.
P
 
Wanabodi,
  1. Wito wangu kwa wapenzi wa Chadema, seek the truth and the truth will set you free. Iambieni Chadema ukweli, ndio mtaijenga Chadema kuwa ni chama mbadala kuireplace CCM. Kwa haya madudu na maroroso kama haya, Ikulu yetu wangeweza?.
Paskali
Sasa Chadema ndio wamefanya the right thing.
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani
Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Back
Top Bottom