Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Eti anaandika barua kwa katibu wa ccm[emoji36][emoji36][emoji36][emoji36][emoji36]
Sasa unashangaa nini? Hujui fomu Huwa wanachukua kwanza Kwa katibu wao, baadaye wanapigiwa kura huko huko kwenye chama na anayeshinda ndiye anapelekwa bungeni kushindana na wagombea wa vyama vingine/binafsi?
 
Kama kajiuzulu kweli, kwanza ningependa afunguke zaidi anachokijua kuhusu kifo cha ghafla cha John Pombe Magufuli. Pili aangalie namna ya kuirudishia uhai Tanganyika irudi kwenye nafasi yake kama nchi baada ya miaka sitini ya uhuru wake.
 
Kwa hyo anabaki kuwa mbunge wa kawaida? Aibu gani hii
 
Kumbe huyu mgogo muoga namna hii.Hana balls kabisa. Inakuwaje mkuu wa muhimili mwingine akufanye ujiuzulu ?
Haya yote dawa yake ni Muongozo(Katiba Mpya na Imara) thabiti


Pelosi aliwahi kuichana hotuba ya Trump mbele yake na hakuna kilichotokea dhidi ya Pelosi, huo ni mfano wa Uimara wa Mihimili.

Kwetu sasa....!!
 
Kwani amajiuzuru kwa hiari yake au kwanguvu za chama, hata hiyo taarifa uenda nayeye anaisoma tu humu humu, unacheza na state......lazma first citizen ambaye ni raisi alindwe kwa mbinu zote
Mimi nadhani huenda alipokiandikia Chama kuhusu kujiuzulu huenda kukawa na maoni ya kusuluhishana huko ndipo Mgogo akaona autaarifu uma kabisa ili wasimjie kivingine na kuonekana katimuliwa yeye. Timing
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…