Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha

Katika hili kwa haraka haraka ndugai ni mnafiki, kama aliona yuko sahihi zaidi kwanini asingeachia ngazi, akakubali mradi usipite nae kaona una manufaa.

Sasa kama aliangalia tumbo lake, vipi sasa hivi tusiamini anachokiongea ni kwa ajili ya tumbo lake?
 
Kwa kweli spika kasababisha taharuki sana, sisi wananchi wa kawaida tunashindwa kuelewa, mihimili sasa inatwangana, kweli JPM alisema tutamkumbuka kwa Mazuri.R.I.P Jeshi wetu,

Basi waahirishe miradi yote ya JPM tuanze moja kama wanahisi aliamua peke yake, wanatuchanganya sana. Pumzika baba hii ndiyo Tanzania
 
Yaani inakuaje wanasiasa wanakuwa wavivu kusoma mikataba kupitia tenda na kushindwa kutoa hoja na ushauri mzuri kwa maslai ya taifa..
 
Hatuwezi kuwa na mradi wa bandari kubwa Bagamoyo na Zanzibar, miradi hii itakinzana.

Bara kuna Bandari Dar tayari, iimarishwe.

Bagamoyo ilikuwa ni White Elephant project.

Ya Bagamoyo ni muhimu kuliko zote...na itasaidia pia upande wa ajira kwa wananchi
 
Ni lini huo Mkataba ulipelekwa Bungeni, maana mimi binafsi sijawahi kusikia?
Au Wachina washafanya yao, maana hao jamaa kutoa rushwa ili kupush agenda zao ni kawaida.
 
Yale Masharti Magumu yamebadilika, au yamelainika ?
 
Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo huenda ukawa na tija zaidi ya Ujenzi wa uwanja wa ndege,Chato!
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amebadilisha msimamo wake kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) mkoani Pwani akisema awali yeye na wabunge wenzake hawakuyajua masharti ya mradi huo bali waliangalia tu faida zake.

Kauli ya Ndugai imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kupigilia msumari wa mwisho wa zuio la ujenzi wa bandari hiyo, alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara juzi Ikulu jijini Dar es Salaam akisema masharti magumu ya mwekezaji ndiyo sababu inayoufanya usitekelezwe.

Magufuli alisema miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kuwa baada ya ujenzi huo wa bandari kukamilika, Tanzania haitaruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine yoyote Pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia Tanga mpaka Mtwara.

Pia alisema wawekezaji hao walitaka wakishajenga bandari hiyo, Tanzania isiruhusiwe kukusanya kodi katika bandari hiyo. Rais Magufuli alisema sharti jingine katika mkataba wa ujenzi wa mradi huo ni kuwa wanatakiwa kupewa muda wa miaka 33 bila kuwauliza chochote watakapokuwa wamewekeza hapo, pamoja na kuwalipa wale watakaokuwa wanafanya kazi ya kuchimba hiyo bandari.

Rais Magufuli aliwaeleza wafanyabiashara kuwa masharti hayo ni magumu na yalikuwa na lengo la kuua bandari nyingine za Tanzania ambazo zinaendelezwa huku akisema Serikali ilifanya utafiti wa kutosha na kuona uwekezaji huo hautakuwa na tija kwa Taifa zaidi ya kuwaumiza Watanzania.

Machi 13, Spika Ndugai wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano bungeni Dodoma yeye na wabunge waliihoji Serikali kwa nini haitekelezi mradi huo ambao hadi kukamilika kwake ungezalisha ajira zaidi ya 1,000 na viwanda vingi vingejegwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai akizungumza na Mwananchi kwa simu jana alisema awali hawakuyajua masharti hayo.

“Sisi hatukuwa na taarifa ya masharti ya nyongeza ambayo mheshimiwa Rais ameyaeleza. Katika majadiliano kati ya Serikali na wawekezaji, wakati mwingine siyo kwamba tunaangalia mambo yote, huwa tunaangalia faida za mradi,” alisema Ndugai.

Aliendelea, “Lakini Rais ameeleza masharti kwa mfano kuzuia bandari zote kuanzia Tanga hadi Mtwara zisifanye kazi. Sasa masharti kama hayo ni ya kipumbavu sana, ya kijinga, sijui hata. Haiwezekani kutekeleza huo mradi kwa masharti hayo.”

“Kwamba sisi tusikusanye kodi kwa miaka 100 ni vitu vya ajabu sana. Rais akishasema basi. Kwa masharti yake hayo, haufai kabisa. Lakini kwa zile faida tulikuwa tunaangalia, kumbe kuna masharti hasi ambayo wabunge hawakuyajua,” aliongeza Ndugai.

Maoni ya Ndugai pia yameungwa mkono na Mbunge wa Hanang, Dk Mary Nagu ambaye ndiye alitia saini ujenzi wa bandari hiyo alipokuwa waziri katika Serikali ya awamu ya nne, akisema kwa kuwa muda umebadilika hawezi kutofautiana na Rais.

“Sisi tuliona bandari ni eneo muhimu la uchumi ambalo lingekuwa na maeneo ya mengi ya kuzalisha. “Mimi nilikuwa waziri na hata yeye (Rais) alikuwa waziri na mambo makubwa kama yale yalikuwa lazima yapitishwe na Baraza la Mawaziri. Lakini kwa kuwa wakati umebadilika sioni sababu ya kutofautiana naye,” alisema Dk Nagu.

Soma pia Ndugai: Mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Magufuli alishauriwa vibaya

Moja ya kazi ya bunge ni kuishauri serikali ktk mambo ya msingi ya kitaifa, hainingii akilini mkuu wa muhimili uliyekubali kuungana na Rais kutaa mradi ule kwa maslahi ya Taifa baada ya kuangalia side effects,Leo hii utuambie eti alishauriwa vibaya, alishauriwa vibaya na Nani kama nawe sio mmoja wapo?WATANZANIA tupunguze ubinafisi,tumepewa nchi hii tuilinde kwa ajili yetu na kizazi kijacho,mnakula Wala hamshibi ,mkishiba mnaanza kutubeulia usoni.
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amebadilisha msimamo wake kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) mkoani Pwani akisema awali yeye na wabunge wenzake hawakuyajua masharti ya mradi huo bali waliangalia tu faida zake.

Kauli ya Ndugai imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kupigilia msumari wa mwisho wa zuio la ujenzi wa bandari hiyo, alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara juzi Ikulu jijini Dar es Salaam akisema masharti magumu ya mwekezaji ndiyo sababu inayoufanya usitekelezwe.

Magufuli alisema miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kuwa baada ya ujenzi huo wa bandari kukamilika, Tanzania haitaruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine yoyote Pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia Tanga mpaka Mtwara.

Pia alisema wawekezaji hao walitaka wakishajenga bandari hiyo, Tanzania isiruhusiwe kukusanya kodi katika bandari hiyo. Rais Magufuli alisema sharti jingine katika mkataba wa ujenzi wa mradi huo ni kuwa wanatakiwa kupewa muda wa miaka 33 bila kuwauliza chochote watakapokuwa wamewekeza hapo, pamoja na kuwalipa wale watakaokuwa wanafanya kazi ya kuchimba hiyo bandari.

Rais Magufuli aliwaeleza wafanyabiashara kuwa masharti hayo ni magumu na yalikuwa na lengo la kuua bandari nyingine za Tanzania ambazo zinaendelezwa huku akisema Serikali ilifanya utafiti wa kutosha na kuona uwekezaji huo hautakuwa na tija kwa Taifa zaidi ya kuwaumiza Watanzania.

Machi 13, Spika Ndugai wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano bungeni Dodoma yeye na wabunge waliihoji Serikali kwa nini haitekelezi mradi huo ambao hadi kukamilika kwake ungezalisha ajira zaidi ya 1,000 na viwanda vingi vingejegwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai akizungumza na Mwananchi kwa simu jana alisema awali hawakuyajua masharti hayo.

“Sisi hatukuwa na taarifa ya masharti ya nyongeza ambayo mheshimiwa Rais ameyaeleza. Katika majadiliano kati ya Serikali na wawekezaji, wakati mwingine siyo kwamba tunaangalia mambo yote, huwa tunaangalia faida za mradi,” alisema Ndugai.

Aliendelea, “Lakini Rais ameeleza masharti kwa mfano kuzuia bandari zote kuanzia Tanga hadi Mtwara zisifanye kazi. Sasa masharti kama hayo ni ya kipumbavu sana, ya kijinga, sijui hata. Haiwezekani kutekeleza huo mradi kwa masharti hayo.”

“Kwamba sisi tusikusanye kodi kwa miaka 100 ni vitu vya ajabu sana. Rais akishasema basi. Kwa masharti yake hayo, haufai kabisa. Lakini kwa zile faida tulikuwa tunaangalia, kumbe kuna masharti hasi ambayo wabunge hawakuyajua,” aliongeza Ndugai.

Maoni ya Ndugai pia yameungwa mkono na Mbunge wa Hanang, Dk Mary Nagu ambaye ndiye alitia saini ujenzi wa bandari hiyo alipokuwa waziri katika Serikali ya awamu ya nne, akisema kwa kuwa muda umebadilika hawezi kutofautiana na Rais.

“Sisi tuliona bandari ni eneo muhimu la uchumi ambalo lingekuwa na maeneo ya mengi ya kuzalisha. “Mimi nilikuwa waziri na hata yeye (Rais) alikuwa waziri na mambo makubwa kama yale yalikuwa lazima yapitishwe na Baraza la Mawaziri. Lakini kwa kuwa wakati umebadilika sioni sababu ya kutofautiana naye,” alisema Dk Nagu.

Soma pia Ndugai: Mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Magufuli alishauriwa vibaya
Mnakwama wapi
 
Back
Top Bottom