GJ Mwanakatwe, japo tunashutumu sana, lazima tuwe fair na kuwa wakweli, huu sio muswada wa katiba mpya, ni muswada wa kukusanya maoni. Ukipita ndipo maoni yakusanywe na ni maoni hayo ndiyo yataamua katiba iweje, Sasa hata maoni bado hizi hoja za kupata katiba mbaya zaidi kuliko hii iliyopo zinatoka wapi?.
Mkuu,
Nadhani Watanzania wengi wanachotaka ni katiba mpya na kwa hali yoyote ile miswada unapoletwa bungeni na kwa wananchi ni lazima ulenge azma hiyo..
JK aliwaahidi wananchi katiba mpya - kwa kauli yake mwenyewe na kasifiwa sana na vyombo vya ki ataifa.
Sasa sielewi huu Muswada unaozungumzia marekebisho ya katiba zaidi badala yakutunga katiba mpya, kuna maana gani zaidi ya kuwachanganya wananchi kwani sehemu zote muhimu zinazosababisha wananchi kudai katiba mpya hazina mjadala.
1: Rais anapotaja yeye kuchagua tume ina maana hatuzungumzii katiba mpya kwani kama ingekuwa na lengo hilo taratibu za muundo wa katiba mpya ni zaidi ya mamlaka ya rais..mwenye akili zake timamu ukiusoma miswada huu utajua haukuwa na malengo hayo hata kidogo..
2. Rais anapotaja sehemu muhimu za katiba zisiguswe ina maana katiba ya zamani inafanyiwa marekebisho zaidi ya utunzi mpya... Kuna tofauti kubwa ktk kuitazama katiba nzima, kisha kuchukua yaliyo bora na mazuri kuliko kuweka mipaka ndani ya katiba hiyo..
JK kama raia na mwananchi angejadili na kuweka mapendekezo yake ktk mjadala kama wanavyofanya viongozi na wataalam wengine lakini hadi hapa yaonyesha muswada huu umeandaliwa kama ni shinikizo la Ikulu ktk kufanya marekebisho..
3. Muswada kuletwa bungeni kwa lugha ya kiingereza ni sehemu nyingine ya kudhihirisha kwamba hii ni sawa na report au muswada wa matumizi ya serikali ukilenga WABUNGE na wataalam zaidi ya wananchi wanaodai katiba mpya na la endelezo la marekebisho ya katiba ya mwaka 1977.
Ndio maana mshirika kasema, kwa mtaji uliopo hatuwezi kuwa na katiba bora zaidi ya tulokuwa nayo..
Nimesema jana mapema sana kwamba chama CCM na viongozi wake watayatumia matukio ya jana kisiasa kulaumu vyama vya Upinzani na wamefanya hivyo kuwabebesha lawama wapinzani kwani wao waliandika muswada huu makusudi ulete vurugu na kutoelewana..
Na maadam vyama vya Upinzani ni kati ya wadau wanaitaka katiba mpya kwa uvunda na ubani kisiasa, CCM imefanya makusudi kuandika muswada huu wakijua wazi kwamba vyama hivyo ndio vitakuwa vya kwanza kuupinga, na hakuna mahala isipokuwa kuwapeleka ktk kumbi za wananchi badala ya kujadiliwa kwa kina bungeni ktk kikao maalum na waalikwa wakiwa wataalam toka fani mbali mbali kulingana na utashi na lugha ya muswada wenyewe, kisha wananchi wakahusishwa baadaye ktk hatua ya pili..
Lakini kwa makusudi kabisa CCM imetaka maoni ya wananchi sii kutaka Katiba mpya bali kushiriki ktk mchakato wa muswada ambao hauna maudhui isipokuwa kuleta mfarakano.. Hadi hapa CCM moja wananchi tumetoka bila na hakika vyama vya Upinzani vitaendelea kuonekana vinataka kuleta vurugu hali wakijua fika kwamba vyama hivyo vinawakilisha mawazo ya wananchi wengi..