naomba kujua kama joseph warioba ni cdm..na kama ni ccm je kwanini hakuzomewa jana..
Wananchi wameamka, hivyo wanaweza kuwapambanua wapenda maslahi ya nchi na wapenda mashabiki wa vyama. Warioba hakuzomewa kwa sababu amesha jipamba nua kuwa yeye ni mpigania maslahi ya taifa.
Huko CCM kuna watu safi, kuna wapambanaji wazuri tuu wa maslahi ya taifa, watu kama kina Warioba, Dr. Salim, Butiku, Peter Kisumo, na hata vijana kama kina Nape Mnauye ni watu wanaosimama na maslahi ya taifa.
Mimi binafsi siamini jana kuwa Tambwe Hiza ndiye aliyetumwa kuwasilisha maoni ya CCM kwenye Kamati ya Bunge, naamini kwa vile lengo la mkutano wa jana, ni public hearing kwa ajili ya wananchi, CCM iliupuuzia mkutano huo na Tambwe Hiza kwa kujipendekeza, alikuja kuhudhuria kama mwananchi tuu, ndio maana jina la mwakilishi wa CCM halikuwepo kwa Mwenyekiti wa kikao, ila Tambwe Hiza kwa kimbembele chake, akajipeleka jina lake na kupewa nafasi.
Sina tatizo na Tambwe na timu yake pale CCM Lumumba wakiongoza kitengo cha Propaganda, kwao propaganda ni kuwa mabingwa wa kupayuka au kujibu mapigo, na ndiocho alichokuja fanya pale jana, alipoanza tuu kupayuka, wananchi waliokuwepo pale wakamkataa na kuvurugika amani ndipo kukafuatia.
Ila pia lazima tufike wakati, viongozi waandilifu wa vyama, wanawajibiki kuwadhibiti wafuasi wao. Mkutano wa jana ilihusu wananchi, ila ile zomea zomea japo ilifanywa na wananchi, kulikuwa na kamkono kidogo ka ushabiki wa baadhi ya watu. Kuna watu walisimama, hata kabla hawajaongea, walishabikiwa kuliko mfano. Walipo changia vipenzi wao ni kushangiliwa tuu mwanzo mwisho hata kama hao vipenzi wao wamechangia pumba, walipigiwa makofi ya pongezi!
Lets be fair, watu wapewe uhuru wa kuchangia mawazo yao hata ziwe pumba vipi?.