Spika Makinda,Ndugai out Bungeni

jamii01

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
1,983
Reaction score
1,423
NAFASI ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na naibu wake imefutwa katika Katipa Mpya ijayo badala yake Spika wa Bunge na Naibu wake hataruhusiwa kuwa Mbunge wala mwanachama wa Chama chochote.
Hayo ni kati mapendekezo ya rasimu ya Katiba Mpya iliyotangazwa hivi punde katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba Mpya Jaji Joseph Warioba huku pia ikimpunguzia Rais Madaraka ya kuteuwa viongozi wa juu wa ngazi ya Serikali.
Tume hiyo pia imefanikiwa kufanya kazi iliyokuwa ikitarajiwa na wananchi hasa baada ya kujibu maswali mengi ya watanzania kuhusu muundao wa Serikali pamoja na masuala ya muungano.
 
Mpaka ntakapoisoma word to work ndipo ntakaporidhika...thanks anyway dude
 
Hivi mkuu heading yako ingesomeka 'rasimu ya katiba mpya spika na naibu wake si wabunge tena' nadhani ingesomeka vizuri, sasa kuwataja dada Makinda na ndugu Ndugai wakati haya ni majina tu ya watu na si cheo unanitia shaka.
 
Ndugai kwisha habari yake alidhani ana hati miliki ya kile kiti sasa akatafute jembe nae asulubike..
 
BA.VI.CHA mmefurahiiiiii
 
Hivi mkuu heading yako ingesomeka 'rasimu ya katiba mpya spika na naibu wake si wabunge tena' nadhani ingesomeka vizuri, sasa kuwataja dada Makinda na ndugu Ndugai wakati haya ni majina tu ya watu na si cheo unanitia shaka.

Umemjibu vizuri.Huo ni ushabiki tu.
 
Kabla ya kwenda huko kooote ningefurahi kusikia nafasi aliyonayo jaji warioba inakuwa scrutinized na kuweka mtu asiye na mrengo,ushabiki,maslahi,wala uhusiano wa moja kw moja na chama chochote,munaweza kufurahi leo kumbe kuna bump kubwa mbele, tukumbuke jopo la watu sita linalolalamikiwa sasa hivi lili inuka katikati ya matumaini na kufifisha kabisa matarajiio chanya kuhusu mchakato wa katiba mpya,wajumbe toka vyama vyote walikuwepo from the roots,sijui wlienda msalani kipengele hicho kilipoingizwa? Kina prof safari nao wakaishia kujiunga na kina sisi kulaumu mchakato mzima!! Bora tuwe wa mwisho kucheka,tutakapoiona furaha ya kweli.
 
Ndugai kwisha habari yake alidhani ana hati miliki ya kile kiti sasa akatafute jembe nae asulubike..

ni heri ungekaa kimya kuficha ujinga wako kuliko hiki ulichofanya.hiyo katiba kama mambo yataenda kama ilivyopangwa itaanza kutumika sana sana kuanzia 2015.so ni kusema bunge lijalo na hata bila katiba mpya uchaguzi wa spika/naibu spika utafanyika upya na sio lazima ndugai apite/agombee
 

kipengele gani hicho mkuu?
 
Hivi mkuu heading yako ingesomeka 'rasimu ya katiba mpya spika na naibu wake si wabunge tena' nadhani ingesomeka vizuri, sasa kuwataja dada Makinda na ndugu Ndugai wakati haya ni majina tu ya watu na si cheo unanitia shaka.
Si unajua tn mambo ya udaku ndugu yangu ni ili watu wakimbilie kusoma
 
Mkuu umemjibu sawa sawa, ndipo mimi naamini nchi hii ina RASILIMALI nyingi tuu si GESI, DHAHABU, WANYAMAPORI n.k. ila na AKILI zetu vilevile ni rasilimali tosha kabisa. Huyu jamaa yaonekana muda wa bunge hafahamu au anachuki binafsi.
 
Wewe una akili sana lazima tu kuna mkenge umefichwa mahali uje kuibuliwa baada ya kila mtu kukenua meno na kushangilia tamaa mbele mauti nyuma
 
Wacha nikapumzige zangu mwendelee kubishana wenyewe...
 
By the way,I guess kamati imefanya kazi nzuri!hawajawa biased as watu wengi walivyokuwa wanaexpect!

Now tutaexpect bunge zuri sana

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
hili ni jambo muhimu sana......
ngoja nijinoe kugombea moja ya hizo nafasi....
wabunge wooote wanaochangia mipasho badala ya hoja nawatoa nje kwa wiki nzima, mbona Bunge litarudisha adabu yake....
 
Ila tusisahau CCM wameteka mabaraza ya Katiba kwa kuweka watu wanao wapenda, hasa wale wasiokuwa na uelewa wowote wa masuala ya sheria na uchambuzi wa mambo.

Nchi hii sasa hivi in wasomi wengi kila eneo, na wapo wasiokuwa na elimu kubwa lakini ni waelewa na wachambuzi wazuri wa mambo yanayo wazunguka. CCM kwa kutumia nguvu ya Chama Dola, wamewaengua wale wote wenye uelewa na kuweka mbumbumbu kama walivyo fanya Kata ya Kalangalala Geita kwa kuokota waganga wa kienyeji na kuwaweka humo! Kwa staili hii sijui kama tuitapata katiba tunayoitaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…