Ni kocha mzuri sema ameingia kwenye nchi yenye maneno mengi mpaka atajuta, angekuwa kocha mbaya leo hii msingekuwa Egypt na msingeleta haya maneno kutoka huko. Chanzo ch kuboronga ni maandalizi hafifu,kuna video zilisambaa humu zikionyesha bondia wetu alivyokuwa anafanya mazoezi kwa kutumia matairi ya gari, tukasema serikali nzima ina kosa budget ya kulipia wana michezo wake gym nzuri ili wanamichezo wakajenga miili na stamina, matokeo yake ndo yale walikuwa wakisumwa wanaanguka wenyewe, hawana nguvu, miguu kama inadegedege kocha afanye nini? misingi mibovu ya michezo.
Kosa la kocha ni moja tu kwangu, kupanga watu wenye lishe duni, mabeki wafupi ambao hawakuweza kuhimili wachezaji wa Senegal, naona tutafungwa 10 za Algeria , Tanzania tunatakiwa tuje na mpango kwanza wa kuimarisha afya bora kwa watoto wetu katika ngazi za familia na mashuleni, tuanzishe programme muhimu ya lishe maziwa kuanzia majumbani, na mashuleni, shuleni iwekwe ratiba ya watoto kunywa maziwa kila siku pakiti mbili, baada ya hapo tuhamasishe michezo katika ngazi zote, baada ya hapo tuchague vijana watakao tuwakilisha vyema katika michezo mbalimbali na tuwaandae vizuri. Hatuwei kuwa na vijana legelege tukatarajia matokeo makubwa tunajidanganya, chukueni Africa mashari ,utagundua ni Tz pekee ndio tuna miili hafifu, programme zetu za lishe majumbani na mashuleni ni 0, na maandalizi yetu ya michezo ni F.
Ushauri ni wa bure, kila mtu akapitie Hotuba ya Prof Lipumba juzi katika mkutano wake Diamond jubilee akizindua sera mpya, ameeleza jinsi report za kimataifa zinaonyesha ni jinsi gani ya kuandaa watoto kwa taifa imara lijalo, Tanzania hatuchachelewa.