Spika Ndugai: Ajira ziwe zinazingatia usawa wa Kijografia



ametahadharisha endapo ajira zitaelemea kuajiri au hata kuteua watu wa aina mmoja kwa maana ya kimaeneo hata kiimani moja zaidi ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa letu.

Mbona Bungeni wamechaguana watu wa aina moja, imani moja ya CCM na mshikamano haujapata hatari yoyote kwa taifa letu?
 
Ndugai njoo huku ujibu huyu mtu ana hoja
 
Udom ipo jirani na Kongwa, chuo cha mipango, CBE, bado unataka nini mzee? wanaosoma hapo wengi wametoka nje na Dodoma
 
Ila Mwendazake!!!! Aliwafanya watu wasitumie akili zao kabisa maana enzi zile wote walikua wanamuabudu kwa kila jambo... bwana Sabufa asingeongea hivi

Punguza roho la kwanini hilo
 
Hatuwezi kuajiri au kuteua wagogo kwa sababu ya jiogorafia na dini zao tu ilihali hawana elimu na sifa za kuajirika au kuteuliwa.

Unapata wapi muda wa kusikiliza mtu mwenye utindio wa ubongo kama Ndugai ?
 
Nchi ya mihemko hiii Mara kipaumbele Kujitolea,leo kipaumbele kijiografia kesho kipaumbele waliomaliza miaka ya nyuma iliyopita.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hiii nchi
 
Mhe. Ndugai amenena jambo la muhimu sana kwa Taifa letu, jambo ambalo wengi walilifumbia macho kwa makusudi au kwa kujifanya halionekani lkn jambo hilo lina hatarisha umoja wa taifa letu nalo ni mgawanyo wa ajira na nafasi za uteuzi serikalini ulio sawia na wa haki, kimaeneo na hata kiimani, sio sahihi kujaza ktk utumishi wa umma watu wa aina mmoja halafu wengine wengi wakatupwa nje, hilo sio sahihi kabisa kwa ustawi na uzalendo wa taifa letu, lazima jambo hilo.litazamwe kwa kuzingatia sifa, usawa wa maeneo na hata usawa wa imani zote kushiriki ktk ujenzi wa taifa lao utaleta na kuimarisha uzalendo wa kweli.

tuache unafiki tuwe wa kweli kama alivyo sema Mhe. Spika. kuwa nchi hii itajengwa kwa umoja wetu na sio kwa kuwatenga wengine.

tuepuke kujaza aina moja ya watu wa kundi la eneo moja au hata la imani moja, jambo hilo halina ustawi kwa Taifa letu.
 
Wanakubali ndugai wana matatizo...huyu haaminiki, ameshindwa hata kulinda kiapo chake
 
Wanakubali ndugai wana matatizo...huyu haaminiki, ameshindwa hata kulinda kiapo chake
wewe ndio humuamini lkn ndugai ni Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
na anaongoza wabunge zaidi ya 300.

kauli yake ina dhihirisha kuwa yeye si kiongozi mnafiki na wala huwa hatafuni maneneo, na pia huwa hayumbi wala kuyumbishwa.

alicho kisema kinapaswa kifikiriwe na mihimili mingine ya serikali, kwa kujitafakari na kujisahihisha.
lengo ni kujenga na kuimarisha umoja wa Taifa letu zaidi ya miaka 100 ijayo.
sisi sote tutakufa lkn Tanzania itaendelea kuwepo, hivyo hakuna budi kwa viongozi wetu wa sasa kulijenga taifa imara kwa kuwashirikisha watu wote ktk uongozi wa taifa lao.
 
Ndugai kasema kweli, na hilo ndiyo tatizo kubwa lililoasisiwa na Magufuli.
Magufuli alijizungushia na “wa kwao” katka kila sekta.

Hebu waorodheshe hawa wa kanda pendwa ya Ziwa, Kalemani, Biteko, Bashungwa,Gwajima, Ndalichako,Mashimba, Chamuriho .
Hawa wote SABA toka kanda pendwa-LEGACY ya Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…