Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imekuwa kila leo Spika anaikosoa Serikali. Mara Serikali ipitie upya mkataba wa bandari ya Bagamoyo. Mara Serikali, kupitia TRA, itoze kodi namna fulani. Na sasa Serikali isitoe visingizio kuhusu ubora wa barabara inazozijenga. Kuna Bunge, Mahakama, na Serikali. Kila mojawapo ya mihimili hiyo ina majukumu yake. Kazi ya Bunge ni kutunga sheria tu. Baada ya hapo sheria hizo zinatafsiriwa na Mahakama; na baadaye Serikali inatekeleza yaliyoamuliwa na Mahakama. Spika anayo majukumu ya kutosha kuyafanyia kazi. Kudodosa yanayojiri siku kwa siku Serikalini ni kuingilia muhimili mwingine. Sanasana aweke hoja ya kutunga sheria fulani na kama Bunge litaipitisha Serikali italazimika kulitekeleza suala hilo. Hizo kauli anazozisema sasa hivi Serikali inaweza kuzipuuza tu na hakuna atakachoifanya.Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameitaka Serikali iache kutoa visingizio ambavyo havina msingi kuwa malori ya kampuni ya Dangote yanaharibu barabara za mikoa ya Lindi na Mtwara.
Amesema kinachotokea ni barabara hizo kujengwa chini ya kiwango, kwani ni jambo linalofahamika kwamba malori hayo yanapimwa uzito, hivyo kampuni ya Dangote haistahili lawama.
Kabla ya kauli hiyo ya Spika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Sera na Watu Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama alisema Serikali itapitia upya ujenzi wa barabara hizo ambazo zimekuwa zikiigharimu fedha nyingi.
Awali wabunge wa kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara walilalamikia jinsi Serikali inavyotumia fedha nyingi katika kuikarabati wa barabara hiyo ukarabati ambao hauna tija kwa kuwa imekuwa ikiharibika.
ITV
Sasa yanaharibu vipi kama sio kwa kuzidisha uzito? kama wanazidisha uzito ndio maana wana ambiwa hivyo.maana yake wao ndio wanaongoza kuzidisha uzito na kuharibu barabaraDangote anaambiwa malori yake yanaharibu barabara, kama ni kupima uzito mizani hakuna lori lisilopima uzito, tatizo ni huko kwa hao wapimaji wanaona malori ya Dangote ndio yanafaa "kupiga"
Huyu anatapatapa tu hana lolote. Kaona Mama SASHA hana time nae wala haangaiki nae kama ilivyokuwa enzi za mwendazake. Wakati huo alikuwa akimwagiwa sifa kem kem namna alivyokuwa akiwasakama Wapinzani.Ndungai amezaliwa upya
Hizo barabara zilijengwa kwa kiwango cha lami yaani surface dressing , zijengwe kwa asphalt maana zinazidiwa na mzigoHATA BARABARA YA DODOMA TO IRINGA NITATIZO TU
Faini hazijasaidia?Sasa yanaharibu vipi kama sio kwa kuzidisha uzito? kama wanazidisha uzito ndio maana wana ambiwa hivyo.maana yake wao ndio wanaongoza kuzidisha uzito na kuharibu barabara
🤣 🤣🤣🤣🤣 mambo gani tena haya jamani!!!!!!
Ndungai amezaliwa upya
Mimi naona walivyofanya upembuzi yakinifu hawakuangalia uzito wa magari, walichukuwa uzito wa magari madogo na mabasi tu na siyo wa mizigo kama ya malori ya simentiSi watengeneze barabara imara...
Utakua ulisoma civics ya nchini Burundi au msumbijiImekuwa kila leo Spika anaikosoa Serikali. Mara Serikali ipitie upya mkataba wa bandari ya Bagamoyo. Mara Serikali, kupitia TRA, itoze kodi namna fulani. Na sasa Serikali isitoe visingizio kuhusu ubora wa barabara inazozijenga. Kuna Bunge, Mahakama, na Serikali. Kila mojawapo ya mihimili hiyo ina majukumu yake. Kazi ya Bunge ni kutunga sheria tu. Baada ya hapo sheria hizo zinatafsiriwa na Mahakama; na baadaye Serikali inatekeleza yaliyoamuliwa na Mahakama. Spika anayo majukumu ya kutosha kuyafanyia kazi. Kudodosa yanayojiri siku kwa siku Serikalini ni kuingilia muhimili mwingine. Sanasana aweke hoja ya kutunga sheria fulani na kama Bunge litaipitisha Serikali italazimika kulitekeleza suala hilo. Hizo kauli anazozisema sasa hivi Serikali inaweza kuzipuuza tu na hakuna atakachoifanya.