Spika Ndugai amtaka Mbowe aache tabia ya kujipima ubavu na Mkuu wa nchi Rais Magufuli, aache kabisa!

Huyu Job inaonekana katumwa kutoka Chato sio kawaida yake namna hii
 

Aisee, kazi kweli kweli kuwa na viongozi wa namna hii....

Spika ni wazi amepanic kupita kiasi

Sijaona hata sababu ya Spika kuendeleza malumbano haya unnecessarily....

Yaani Spika hata haelewi kuwa Mbowe ni KUB na ni kiongozi wa chama Taifa...
 
Ndugai ni spika wa kushangaza Sana

Imeandikwa wapi mbunge hana haki ya kutoa maoni nje ya bunge eti kwakuwa ni mjumbe wa kamati?

Sheria ipi inamkataza mtanzania yeyote kumjibu au kumkosoa kiongozi yeyote wakati wowote?

Yeye spika ana nidhamu ipi baada ya kumjibu Mbowe dhidi ya hotuba yake?
Alichokifanya Mbowe na yeye Ndugai kuna tofauti gani.!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jumapili tarehe 17 may 2020 viongozi wawili wa kitaifa waliongea na Taifa /wananchi kila mmoja kwa wakati wake.

Mmoja na mwenyekiti wa chama cha upinzani chenye nguvu na ushwishi kwa wananchi na mmoja ni Rais wa nchi mwenye nguvu na mamlaka sana kwa Tanzania ya sasa.

Speech ya Rais ilitolewa mjini chato ambako ndio nyumbani kwake na aliotoa speech hiyo akiwa kanisani KKKT.

Speech ya Mqenyekiti wa chama cha demkrasia na maendeleo (Chadema) ilitolewa online sifahamu alikuwa wapi lakini alikua live.

Kila mmoja aliongea mambo muhimu japo kuna baadhi ya mambo walipishana kimtazamo.

Kuonyesha speech zote mbili zilikua muhimu, vyombo vingi vya habati viliripoti kwa kutukia njia mbalimbali kama social media, tv na redio isipo kuwa TBC pekee yake haikuripoti chochote alicho ongea mbowe.


Kulikua na mijadala mingi na wengi wakitaka kujua nani katoa speech bora yenye kutoa mwanga kwa wananchi?

Wengi walikubali wote wawili walitoa speech nzuri katika mitazamo tofauti hasa swala la corona.


Kituko ni leo huko bungeni, spika badala ya kukazia mambo ambayo Rais ameongea, ametumia katibia nusu saa kuongelea speech ya m/kiti wa chadema mh Mbowe.

Hii inaonyesha ni kiasi gani Mh mbowe anakubalika ndani na nje ya chadena hadi kumtikisa spika kuacha majukumu yake na kutumia muda wa bunge kumwongelea Mbowe.

Nadhani spika angeweza kutumia muda huo kukazia agenda za Mh Rais ili wabunge wazielewe na wazitafakari kwa ajili ya kuishauri serikali.

Kwa maana hii speech ya mbowe ilisikilizwa hadi na spika wa Bunge.

Mungu ibariki chadema
Mungu ipe macho ccm
Mungu ibatiki Tanzania

Amen.

 
Nakazia, Mbowe ajue Mh. Rais ndio Caesar Mkuu, ndio yule Mungu aliyempa madaraka ya kuongoza nchi yetu, inabidi amuheshimu atake asitake, ni Amri ya Mungu
 
Yaani Speaker anakomaa na Posho ya 2M
Moyo wa Ki Maskini sana huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, kazi kweli kweli kuwa na viongozi wa namna hii....

Spika ni wazi amepanic kupita kiasi

Sijaona hata sababu ya Spika kuendeleza malumbano haya unnecessarily....

Yaani Spika hata haelewi kuwa Mbowe ni KUB na ni kiongozi wa chama Taifa...
Mbowe arudishe 2,040,000!
 
Haya ni maneno yanayotoka moja kwa moja kwenye redio, speaker ni kipaza sauti tu.
Maneno yanatoka Redio Magufuli, yanarushwa na SPIKA Ndugu. Hizo spika aina ya Ndugu ni nzuri sana. Zina HIGH FIDELITY, hasa kwa Redio Magufuli.
 
Bado najiuliza kwanini mboe anasakamwa hivi sipati jibu kabisa
 
Mbona mnamkuza sana Mbowe, aongee na taifa yeye ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

spika ongelea bunge ni muhula tofauti. Mbowe ana haki ya kuzungumza wakati wowote. Alivyotaka kuzungumza katikati ya wiki walimpelekea polisi sasa tupinge hoja sio kiongozi wa Chama kuzungumza. Hakuna sheria Mwamba watu wasizungumze kwa sababu raisi amazungumza hatuna mfalme wala malkia Tanzania tuna wanasiasa
 
Mbowe amejivua nguo hadharani achutame tu

Haiwezekani Mkuu wa Nchi aongee yeye aanze kupinga tu tena bila hoja mathubu
Mama watoto nikukumbushe kitu, kusema ukweli hotuba ya Mbowe yajana imekuwa kama imetolewa na kiongozi wa nchi! Jana Mbowe kampiga 3-0 yule mzee wa tocha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…