Spika Ndugai amtaka Mbowe aache tabia ya kujipima ubavu na Mkuu wa nchi Rais Magufuli, aache kabisa!

Spika Ndugai amtaka Mbowe aache tabia ya kujipima ubavu na Mkuu wa nchi Rais Magufuli, aache kabisa!

Nakazia, Mbowe ajue Mh. Rais ndio Caesar Mkuu, ndio yule Mungu aliyempa madaraka ya kuongoza nchi yetu, inabidi amuheshimu atake asitake, ni Amri ya Mungu
Lakini ni kipi ambacho kinawafanya mseme HAMUHESHIMU rais wetu?!

Hotuba yake ni mawazo yake, na kutokukubaliana kwenye mambo sio kitu kipya.

Sioni ni wapi mnaiona heshima na wapi haionekani?!

Au kwasababu yeye HAJAMSIFU rais wetu hivyo anaonekana Hamuheshimu?!
 
Kipi kimekushinda kuiona hiyo hoja Ndungai? Nani kwenye kundi lenu alishawahi kujibu au kukosoa hotuba/ maagizo ya mwenyekiti wenu Mbowe hadharani mara tu baada ya kuitoa na akabaki salama? Tumeshuhudia hivi karibuni wabunge 11 wakitimuliwa walipokosoa maagizo ya mkuu wa chama chao yaliyowataka wajifungie ndani kwa siku 14. Walitimuliwa kwa ukosefu wa adabu kwa mkuu wao Mbowe. Sasa kwa sababu ipi Mbowe naye asiadhibiwe kwa ukosefu wa adabu kwa mkuu wa nchi yake?

..Hotuba zote za Raisi zinatakiwa zijibiwe na kiongozi wa upinzani nchini.

..huo ni utaratibu wa kawaida kabisa ktk nchi za kidemokrasia.

..Spika Ndugai anapotosha anapodai kwamba kujibu hotuba ya Raisi ni kumvunjia heshima.
 
The last kick from a dying donkey! Ndugai ameishiwa nguvu! Na uchaguzi huu anaangushwa kwenye kura za maoni, lile jamaa alilolipiga fimbo 2015 linarudi kwa nguvu zote! Uspika bye bye!
 
Mbumbubu ni wewe ambaye akili yako ilishatekwa na Mbowe.
angalia hii
Viongozi wakuu wa vyama viwili Nchini wakitimiza majukumu yao katika kipingi hic ( 640 X 640 ).jpg
 
Huyu jamaa ana mambo ya ushamba mno!! This is too much!!

Wengine tunapata maisha haya ukubwani na ndiyo yanaligharimu taifa.

Hakuna jambo la ku address kwa sasa zaidi ya POSHO?
 
Mbowe amejivua nguo hadharani achutame tu

Haiwezekani Mkuu wa Nchi aongee yeye aanze kupinga tu tena bila hoja mathubu

Kazi yake ni kupinga, sio kuunga mkono, ndiyo maana ya upinzani. Sasa kinachobakia ni kazi ya wananchi kuona kilichopingwa na kilichoelezwa, ni kipi kinaleta sense.

Wkat mwingine Ndugai aelewe, siyo kila kitu lazima akitolee ufafanuzi kwa yeye kuwa upande wa serikali. Mwingine atasema, Mwenyekiti wa chama fulani kamkosoa mwenyekiti wa chama kingine kwahiyo haoni shida ilipo, hadi siku kofia ya uraisi itenganishwe na kofia ya uenyekiti wa chama, ndiyo unawaze hoji kuwa Mbowe, ulimjibu rais au ulimjibu mwenyekiti wa chama?
 


Up dates;

Spika Ndugai amesema Mbowe kama KUB ni mtu muhimu sana pale bungeni na ni mjumbe wa kamati zote muhimu ikiwemo ya Uongozi, kamati ya haki, kamati ya kanuni na kamati ya bajeti.
Pia kama KUB Mbowe anaruhusiwa kusimama bungeni wakati wowote na kuuliza au kushauri chochote tofauti na wabunge wengine wote.

Spika Ndugai anasema ni utovu wa adabu na nidhamu kwa kiongozi yoyote kujibu hotuba ya mkuu wa nchi mara tu amalizapo kuhutubia, Mbowe kama alikuwa na maswali au ushauri utaratibu anaopaswa kuutumia anaujua ila kiukweli Mbowe ni mtoro sana wa bunge na hata vikao vya kamati haudhurii kabisa.

Ndugai amesema tatizo lake na Mbowe limeanza pale alipomtaka KUB arudishe posho ya sh 2,040,000 aliyochukua bila kuifanyia kazi baada ya kujiweka karantini.

Ndugai ameapa Mbowe ni lazima atarudisha hiyo fedha liwake jua au inyeshe mvua, wabunge wengine wamesharudisha kasoro Mbowe na wengine wawili au watatu.

Ndugai anashirikiana na Magufuli kufanya bunge liwe la hovyo na dhaifu. Anachowaza ni kwa Mbowe kurudisha pesa tu, kwani Milioni 2 ni pesa nyingi zitarudishwa tu wala asiwe na wasiwasi, ila yeye aache kushirikiana na serikali kuumiza watu. Ndugai ni mgomvi, mpiga watu, mgovi anagombana na kila mtu mpaka CAG aliyepita kwa sababu ambazo si za msingi.
Huyu spika ni wa hovyo.....Ndugai rudisha Mabilioni ya pesa uliyotumia ukiwa India.....Matibabu gani ya Mabilioni. Serikali yetu ya hovyo, bunge la hovyo na mahakama ya hovyo.
 
..Hotuba zote za Raisi zinatakiwa zijibiwe na kiongozi wa upinzani nchini.

..huo ni utaratibu wa kawaida kabisa ktk nchi za kidemokrasia.

..Spika Ndugai anapotosha anapodai kwamba kujibu hotuba ya Raisi ni kumvunjia heshima.

Na kuhusu mabunge mengine kuendelea bila lockdown, angalia hapa UK Parliament to hold virtual debates amid virus lockdown
Senate ilikuwa lockdown, wamerudi hivi karibuni. House of Representatives bado iko kwenye lockdown. Uingereza walikuwa kwenye lockdown na waliporudi wamebadilisha taratibu zao ili wabunge wachache iwezekanavyo ndio wanakuwa bungeni. Wafaransa nao wamepunguza idadi ya watu wanaokuwemo bungeni ili kuwezesha social distancing. Mabunge yote haya yamechukua hatua yenyewe kuhakikisha wanadhibiti ugonjwa huu ndani ya majengo yao. Supreme Court ya marekani sasa hivi inasikiliza kesi kupitia mtandao. Mheshimiwa Spika alitakiwa aseme Bunge lake limechukua hatua gani ili kuhakikisha wabunge, watumishi na wageni wa Bunge hawaambukizwi huu ugonjwa.

Amandla...
 


Up dates;

Spika Ndugai amesema Mbowe kama KUB ni mtu muhimu sana pale bungeni na ni mjumbe wa kamati zote muhimu ikiwemo ya Uongozi, kamati ya haki, kamati ya kanuni na kamati ya bajeti.
Pia kama KUB Mbowe anaruhusiwa kusimama bungeni wakati wowote na kuuliza au kushauri chochote tofauti na wabunge wengine wote.

Spika Ndugai anasema ni utovu wa adabu na nidhamu kwa kiongozi yoyote kujibu hotuba ya mkuu wa nchi mara tu amalizapo kuhutubia, Mbowe kama alikuwa na maswali au ushauri utaratibu anaopaswa kuutumia anaujua ila kiukweli Mbowe ni mtoro sana wa bunge na hata vikao vya kamati haudhurii kabisa.

Ndugai amesema tatizo lake na Mbowe limeanza pale alipomtaka KUB arudishe posho ya sh 2,040,000 aliyochukua bila kuifanyia kazi baada ya kujiweka karantini.

Ndugai ameapa Mbowe ni lazima atarudisha hiyo fedha liwake jua au inyeshe mvua, wabunge wengine wamesharudisha kasoro Mbowe na wengine wawili au watatu.

CDM inaelekea shimoni,Mbowe ndie wakuombewa sio Ndugai.
Aliongea upupu na aliongea kujibu speech ya Mh.Rais .
 
Mbowe amejivua nguo hadharani achutame tu

Haiwezekani Mkuu wa Nchi aongee yeye aanze kupinga tu tena bila hoja mathubu
Wewe uliwahi kusoma mada na kutafakari ujumbe kisha ukatoa majibu ya weledi hata siku moja?
Umekuwa MTU anayeshusha hadhi ya JF na kuonekana ni kijiwe cha wapumbavu wakati mpumbavu ni wewe pekee.
Nafikiri bora watu waku block

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom