Spika Ndugai anasema hawezi kuwafukuza bungeni Wanawake kwa maana dunia itamshangaa; lakini hashangai Serikali kuwafukuza shule wanawake

Spika Ndugai anasema hawezi kuwafukuza bungeni Wanawake kwa maana dunia itamshangaa; lakini hashangai Serikali kuwafukuza shule wanawake

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Wakuu amani iwe nanyi

Mwendelezo wa mtifuano mkali, CCM sasa inamtetea mwanamke kwa kila namna.

Ni hivi: Jana spika Job Ndugai alisema kuwa hawezi kuwafukuza bungeni wale akina mama kwa sababu dunia nzima itamshangaa kwa kuwafukuza wanawake bungeni na hali hiyo itapelekea yeye binafsi kuandikwa katika vitabu vya maajabu ya dunia kama spika wa hovyo.

Ikumbukwe pia kuwa wanawake hufukuzwa shule pindi wapatapo ujauzito na hawaruhusiwi kurudi hata baada ya kujifungua.

Sasa swali: Kwanini spika anahisi ni aibu kumfukuza mwanamke bungeni ila ni sawa mwanamke huyohuyo kufukuzwa shule?
 
Huyo Spika ni kituko, katika bunge la 11 alihakikisha huyo Mdee haingii bungeni mwaka mzima. Amejipa kazi ya kuwalinda kwa manufaa ya CCM.
 
Hahaha kinachowachanganya UVCCM ni kuona Waliotokea Chadema ndio wanalindwa na kuthaminiwa kuliko mi ccm yenyewe.
 
Kinachotendwa na ndugai ni aibu kwa taifa.Kiongozi aina ya spika kulumbana na chama Cha siasa kwa kuadhibu wanachama wake ni aibu.spika aheshimu maamuzi ya vyama vingine vilevile hata Kama hayapendi
 
Huyo ndugai anajitekenya mwenyewe.. Halima na wenzake siyo wabunge kwa mujibu wa katiba ya nchi kwa sabb chama chao kimesha wavua uanachama.

Mwaka 2017 Sophia Simba alipovuliwa uanachama na CCM huyo huyo ndugai alikuwa spika, mbona hakumkingia kifua? Au Sophia siyo mwanamke?!

Kama hataki kuheshimu Katiba ya nchi aliyoapa kuilinda, hafai kuendelea kuwa spika
 
"Naagiza Halima popote alipo aje haraka sana mbele ya kamati ya maadili na ikibidi ataletwa hata kwa pingu" punde si punde mtetezi wa wanawake hasa mtetezi wa Halima Mdee na wenzake 18 a.k.a Ndugai anamfukuza Halima bungeni kwa mwaka mzima.
 
kwani Sophia simba alikuwa Mwanaume?, lakini Lipumba aliwatimua pia wabunge na wao CCM wakaridhia tena spika akawa wakwanza kupeleka barua Tume ya Taifa ya uchaguzi kuwa nafasi zipo wazi.

kinachoendelea sasa hata mtoto anajua kuwa ni njama zao serikali na CCM.

Lakini pia ni uvunjaji mkubwa wa waziwazi wa KATİBA.
 
Nafikiri kuna shida mahali. Naomba nimpe ushauri Ndugai.
  1. Jambo la kwanza akatae kupokea barua toka Chadema ya kuvuliwa uanachama wabunge 19.
  2. Ashauriane na Mwanasheria mkuu wa serikali na alete muswada wa dharura wa kubadili kipengele kinachotumiwa na Chadema katika kuwatimua
  3. Kikao kijacho cha bunge mswaaada uwe tabled na upitishe na uanze kutumika mara moja.
Bila hivyo kila siku atajichanganya tu!!
 
Mheshimiwa Ndugai aache lugha za uswahilini. Ana kazi ya kupokea wabunge na pale Katiba ya Nchi inapomtaka awaondoe Bungeni hana budi kuwaondoa, hakuna uswahili; ni kuwaondoa kwa mujibu wa Katiba na Sheria. Dunia itamshangaa Sasa kwamba Spika wa Bunge la Tanzania anawalinda wabunge kwa kuvunja Katiba ya Nchi.
Haikubaliki.
 
Back
Top Bottom